Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli mrudishe January Makamba na Nape wajibu hoja, Polepole anakihujumu chama

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,099
Humprey Polepole tambua Rais anategemea taarifa sahihi toka kwenu lakini wewe unamdaganya na kumsababishia kampeni kuwa ngumu kwake sana.

Mimi ni mwana CCM na sihami CCM, Ni dhahiri Humphrey Polepole anamuhujumu Magufuli kwa ushauri wake mbovu na wa kizamani enzi za ukoloni.

Polepole anafikiria mambo ya kizamani sana wakati yeye ni kijana ambaye ilibidi amwambie Rais kuwa wananchi wanataka pesa na maisha yao yameyumba

Polepole alishauri watu wa upinzani kuhamia CCM,Hii plan imeshindwa vibaya sana

Polepole ameigawa CCM pande mbili CCM mpya na CCM asilia huku akimshauri Rais kuwaadhibu CCM asilia sasa yupo yupo tu

Polepole sasa ameanza kuongea matusi kwenye television mbele za watoto wetu sebuleni anatudhalilisha watu wazima. Anashindwa kujibu hoja kabisa.

Kikwete aliwateua Nape na Makamba kwa ajili ya propaganda kujibu hoja za Dkt Slaa.

Nape na Kinana wakati wa mambo ya ufisadi waliwakana wezi wote na kuongea ukweli.

Humprey polepole ni wa kuwa nae makini sana wakati huu ni ndumilakuwili na hafai.
.
Kwa kuwa Nape yupo na January yupo ni muda wa kuwatumia kujibu hoja.

Ni wakati wa Rais Magufuli umuulize polepole kwa kipindi chake amefanya kitu gani kwa chama,kwanini wananchi wanaunga mkono upinzani wakati alituaminisha upinzani umekufa?

Amechanganyikiwa sasa anaanza kutukana matusi,Huyu anachochea fujo ni wakati wa ccm kukubali polepole hana ushawishi wa kukiunganisha chama
 
Rais amefanya kazi nzuri sana ndani ya chama kwenye serikali na Taifa kwa ujumla.

Tumuache Magufuli afanye kazi.
 
Niliposikia tu kuwa Polepole ana press nyingine ndani ya muda mfupi hivi, nilijua wazi hana jipya, na kwa kiwango kikubwa nilitegemea press ya kuchanganyikiwa. Alichokionyesha Polepole leo ni jazba na wala sio hoja.

Nadhani kikao walichokaa safari huu Magufuli atakuwa ameongea kwa jazba, na huyo Polepole kaja kuweka wazi chuki ya mwenyekiti wake hadharani. Narudia tena kusema, iwapo wapinzani watasimamia mgombea halali kutangazwa, tutegemee umwagaji mkubwa wa damu.
 
Polepole ni tunu ya taifa, anaweza kuingia kwenye vitabu vya historia kama mwanasiasa mahiri aliyechangia mabadiliko makubwa ya kisiasa nchini Tanzania, mwacheni afanye kazi yake
Kwa taarifa yako hakuna anaye kiua CCM kama huyu jamaa mtashangaa yatakayotokea mwaka huu.
 
Kuwa CCM sio kwamaba ukawa msafi, unadhani hiyo pesa unayotaka iachiwe kwa mtindo gani?
Mlipane posho hovyo na kuachwa mpige madili au?

Twambie hapo zamani pesa ilikuwa inatoka wapi kwa njia halali, na kama hiyo. Njia halali imefungiwa?

Kam una akili tafuta vyanzo wewe uajiri. Wengine wapate kutoka kwako, usitegemee wewe uletewe, niwakati wa watanzaia kujenga uchumi wao wenyewe, tumia akili kutafuta vyanzo.
 
Ni wakati wa Rais Magufuli umuulize polepole kwa kipindi chake amefanya kitu gani kwa chama,kwanini wananchi wanaunga mkono upinzani wakati alituaminisha upinzani umekufa?
Duhh hii tu umeona mkuu

Mambo magumu
 
Back
Top Bottom