Uchaguzi 2020 Magufuli(Mlowa): Ubunge sio 'madigrii' ni kipaji kutoka kwa Mungu; mkichagua Wapinzani nitashindwa kuwatumbua wasipofanya kazi

View attachment 1583483

Katika kipindi cha miaka 5 tumefanya mengi, hata kuhamishia Makao Makuu Dodoma halikuwa jambo dogo. Miaka 47 haijawezekana ila miaka 5 tumeweza. Makao Makuu yanamaanisha ustawi wa eneo hili unakuja kwa nguvu.

Tunajenga Uwanja wa Ndege mkubwa huko Msalato ili ndege za kimataifa zije. Tumeleta stendi ya kisasa, soko la kisasa n.k. Tunatimiza ndoto ya Mwl. Nyerere.

Uongozi sio madegree ni kipaji toka kwa Mungu, Lusinde ni kijana mzuri na anafanya kazi nzuri ndio maana ni mjumbe wa NEC. Nyie wananchi mnajua kuchagua.

Natoa ahadi kwa watani zangu Wagogo, niliahidi km 16 toka Mlowa hadi Mvumi zitengenezwe kwa lami.

Anamuita Mkuu wa Mkoa...

"Nataka umuagize RM wa TANROADS Dodoma ndani ya miezi 2 barbr ya Mlowa kwenda Mvumi itangazwe tenda kwa ajili ya kujengwa kiwango cha lami.

Nataka wagonjwa wanaougua macho hapa wawe wanapelekwa kwa haraka Mvumi. Tunataka jombi lililo karibu na Makao Makuu lifanane na hadhi hiyo. Tunataka tubadilishe Wilaya ya Mvumi. Nina hiostoria nayo, nilikuwa na kaka yangu hapa alishafariki. Nilishawahi kuleta mzee mmoja kutoka Chato ameshatangulia mbele za haki.

Ndugu zangu wa Mvumi, mna mbunge mchapakazi. Narudia ubunge sio Degree ni kuwakilisha mawazo na shida za wananchi anaowaongoza. Lusinde anaweza mumpe kura nyingi. Au kapita bila kupingwa au wapo wanaompinga? Wanaompiga waonesheni tarehe 28 lakini pia mniletee madiwani wa CCM ili kazi ifanyika vizuri

Nitashangaa sana tumeleta Makao Makuu hapa halafu shukrani iwe ni kutunyima kura? Kweli watu wa hapa hamfaidiki na Makao Makuu ya Dodoma?

Kabla ya miaka 2 kupita, vijiji 30 vilivyobaki vitakuwa na umeme. Mimi nakaa hapa, haiwezi kunishinda"

Dkt. Magufuli anasisitiza madiwani wote wawe wa CCM ili Halmashauri ya Wilaya itakayoundwa pesa zitakazoletwa zitumiwe vizuri na wa CCM sababu nina uwezo wa kuwatumbua. Mkileta wengine (vyama vingine) sitoweza kuwatumbua, wakila msinilaumu

Kisha Dkt. Magufuli anatania kuwa anawapenda sana Wagogo, "Inawezekana Lusinde akanitaufutia kasichana kazuri ka kigogo"

Ndio maana hata sisi Chadema Mbowe ndio Mwenyekiti wetu, Mnyika, Katibu Mkuu, Kigaila Naibu Katibu Mkuu. na tunaendelea.

Cha Ajabu nini CCM kupata mbunge amemaliza darasa la Saba?
 
Uongozi ni talanta
Ni kweli kipenzi, si unaona Talanta ya Lissu, akiongea tu neno unajua kabisa leadership lies within his blood, ila kuna yule mwingine akiongea ni anatufokea mpaka tunaficha uso, hachagui nini cha kuonea na wapi pa kuongea, mbaya zaidi maneno yake hayana matumaini kabisa
 
Kampeni za huyu mtu hazinivutii hata kidogo, labda hili tatizo ni langu mimi binafsi na siyo kwa watu wengine. Kwa maana kila anachokiongea ni kile kile tu ambacho tumemisikia akikiongea toka mwaka 2016.
 
Ulitaka ijengwe kwa siku, au wiki moja au mwezi au mwaka moja tuu eeeh
Wewe nyumba yako umeijenga kwa muda gani??? Kama umeshamaliza ujenzi

Unaijua Dodoma vzur?Unajua CCM imeyakalia kwa mda ganI hayo majimbo?
 
Ni kweli kipenzi, si unaona Talanta ya Lissu, akiongea tu neno unajua kabisa leadership lies within his blood, ila kuna yule mwingine akiongea ni anatufokea mpaka tunaficha uso, hachagui nini cha kuonea na wapi pa kuongea, mbaya zaidi maneno yake hayana matumaini kabisa
28102020
 
Unaijua Dodoma vzur?Unajua CCM imeyakalia kwa mda ganI hayo majimbo?
Kuna majimbo yamekaliwa na upinzani pia kwa miaka na hakuna jipya. Dodoma miaka hii mitano ya CCM chini ya Magufuli wamepiga hatua kubwa sana kama ilivyo kwa mikoa mingine

💥

Wapinzani sijui wana nini😆😆😆😆
 
Mnatumbua bila kufuata sheria na kanuni za ajira!
Visa na visasi vinatawala!
Ukanda na ukabila umejaa na kutamalaki!
Utawala bora hauna nafasi kabisa ktk kipindi hiki.
 
Kuna majimbo yamekaliwa na upinzani pia kwa miaka na hakuna jipya. Dodoma miaka hii mitano ya CCM chini ya Magufuli wamepiga hatua kubwa sana kama ilivyo kwa mikoa mingine

💥

Wapinzani sijui wana nini😆😆😆😆

Mkuu naomba unipatie orodha ya mambo yaliyofanywa na CCM ambayo hayakuwepo Dom hasa nje ya jiji.
 
Back
Top Bottom