CCMkuelekeaUchaguzi
Senior Member
- Aug 18, 2015
- 179
- 77
Katika kipindi cha miaka 5 tumefanya mengi, hata kuhamishia Makao Makuu Dodoma halikuwa jambo dogo. Miaka 47 haijawezekana ila miaka 5 tumeweza. Makao Makuu yanamaanisha ustawi wa eneo hili unakuja kwa nguvu.
Tunajenga Uwanja wa Ndege mkubwa huko Msalato ili ndege za kimataifa zije. Tumeleta stendi ya kisasa, soko la kisasa n.k. Tunatimiza ndoto ya Mwl. Nyerere.
Uongozi sio madegree ni kipaji toka kwa Mungu, Lusinde ni kijana mzuri na anafanya kazi nzuri ndio maana ni mjumbe wa NEC. Nyie wananchi mnajua kuchagua.
Natoa ahadi kwa watani zangu Wagogo, niliahidi km 16 toka Mlowa hadi Mvumi zitengenezwe kwa lami.
Anamuita Mkuu wa Mkoa...
"Nataka umuagize RM wa TANROADS Dodoma ndani ya miezi 2 barbr ya Mlowa kwenda Mvumi itangazwe tenda kwa ajili ya kujengwa kiwango cha lami.
Nataka wagonjwa wanaougua macho hapa wawe wanapelekwa kwa haraka Mvumi. Tunataka jombi lililo karibu na Makao Makuu lifanane na hadhi hiyo. Tunataka tubadilishe Wilaya ya Mvumi. Nina hiostoria nayo, nilikuwa na kaka yangu hapa alishafariki. Nilishawahi kuleta mzee mmoja kutoka Chato ameshatangulia mbele za haki.
Ndugu zangu wa Mvumi, mna mbunge mchapakazi. Narudia ubunge sio Degree ni kuwakilisha mawazo na shida za wananchi anaowaongoza. Lusinde anaweza mumpe kura nyingi. Au kapita bila kupingwa au wapo wanaompinga? Wanaompiga waonesheni tarehe 28 lakini pia mniletee madiwani wa CCM ili kazi ifanyika vizuri
Nitashangaa sana tumeleta Makao Makuu hapa halafu shukrani iwe ni kutunyima kura? Kweli watu wa hapa hamfaidiki na Makao Makuu ya Dodoma?
Kabla ya miaka 2 kupita, vijiji 30 vilivyobaki vitakuwa na umeme. Mimi nakaa hapa, haiwezi kunishinda"
Dkt. Magufuli anasisitiza madiwani wote wawe wa CCM ili Halmashauri ya Wilaya itakayoundwa pesa zitakazoletwa zitumiwe vizuri na wa CCM sababu nina uwezo wa kuwatumbua. Mkileta wengine (vyama vingine) sitoweza kuwatumbua, wakila msinilaumu
Kisha Dkt. Magufuli anatania kuwa anawapenda sana Wagogo, "Inawezekana Lusinde akanitaufutia kasichana kazuri ka kigogo"