Magufuli mizigo anaiona ya wanasiasa kuhama vyama tu, hivi kupanda kwa bei bidhaa, hakuna ajira, elimu mbovu, madawa hakuna,sio mizigo kwa wanyonge

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
ANANDIKA Dotto Bulendu

Jana wakati akitangaza majina ya wateuliwa kuwania nafasi za ubunge kupitia CCM kwa ajili ya uchaguzi mdogo,

Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Magufuli alisema chama kitaendelea kuwapokea wanasiasa wote wanaotaka kurejea CCM na kuwaahidi pumziko lenye furaha.

Mh Rais alisema wale wote wenye mizigo huko walipo wahamie CCM ili waishushe mizigo waliyonayo na akasema wengi waliondoka CCM kutokana na figisu walizokutana nazo lakini wamekutana na figisu zaidi.

Sasa Mh Mwenyekiti na Rais wa chama,na sisi ambao hatupo kwenye siasa na hasa si wabunge na madiwani,mizigo yetu tukaitue wapi?maana

1.Huku mtaani tunaelekewa na mzigo wa kupaa kwa bei ya simenti,bei ya sukari ilivyopanda haijawahi kushuka,bei ya mafuta ya taa,Petrol na diseli nayo haikamatiki siki hizi,huu mzigo umetuelemea tukautue kwa nani Mh Rais?

2.Watumishi wa umma wameelemewa na mzigo wa kutokupandishwa madaraja(baadhi),miaka mitatu sasa hakuna nyongeza ya mshahara Mh Rais,huu ni mzigo umeaelemea watumishi wa Umma,wakautue wapi Mh Rais?usipoutua mzigo huu Mh Rais kuna hatari ya "Go slow strike".

3.Sekta binafsi zimeelemewa,sasa hivi wafanyakazi kwenye sekta binafsi wanahenya na maisha ya bila mishahara,waliowekeza huko wanalia mazingira ya biashara kiujumla hayawapi faida baadhi wanapunguza tu wafanyakazi,huu nao ni mzigo,kama ulivyo nukuu kitabu kitakatibu (Biblia),kwamba wote wenye mizigo iliyo waelemea waje kwako,wenye hii mizigo nao waje?

4.Mh Rais,vijana waliomaliza masomo yao vyuoni,shuleni ma vyuo vikuu kuanzia mwaka 2015 ulipotangaza oparesheni saka watumishi hewa na wasio na vyeti,asilimia kubwa hawajaajiriwa mpaka leo,wapo mtaani hawajui hatma yao,wameelemewa na mzigo wa ukosefu wa ajira na ukali wa maisha,Mh Rais watoto wako hawa unawasaidije kuutua huu mzigo,na jana ulisema wote walioelemewa na mzigo waje kwako Mh Rais,hawa nao waje?

5.Mh Rais yalifanyika mabadiliko ya kisheria ya mifuko ya jamii kwa kuzuia wastaafu kulipwa mafao yao mpaka watakapofikisha umri uliopotishwa,Mh Rais kuna kundi la watu wapo kwenye umri wa kati na wameamua kuacha kazi ili wakafanye mambo mengine,sasa wanapoambiwa wasubiri
mpala wafikishe umri uliopotishwa kisheria wamebaki njia panda,mzigo sasa umewaelemea hawajui pa kuutua,sijui tunawasaidiaje?

6.Mh Rais familia na ndugu wa Azory Gwanda,Ben Saanane wamelia sana kuwasaka ndugu zao,wanaelewa na mzigo wa mawazo walipo wapendwa wao,Mh Rais kama ulivyosema wote walioelemewa na mizigo waje kwako,kwa kutumia vyombo vyako,wasaidie familia hizi kuutua mzigo unaowaelea,hakuna mzigo mzito kama mzigo wa mawazo Mh.

7.Mh Rais,kule vijijini katazo la kusafirisha mazao nje,liliporomosha bei ya mazao,Maeneo mengi wanavijiji wamejikuta wamekaa na mazao ndani kwani soko la ndani limetengeneza hasara kubwa kwao,hawa nao wameelemewa na mzigo huu Mh Rais.

8.Mh Rais nadhani umesikia jana kuwa Ligi kuu msimu huu haitakuwa na mdhamini mkuu,na nimeona kuna mdhamini eti atadhamini kwa kuvipa vilabu shilingi milioni 15 kila kimoja,Mh Rais sekta binafsi iliyokuwa imewekeza huku waliowengi wanalia na faida kiduchu,wanadai mazingira ya biashara yamebadilika sana,sasa hata kwenye michezo taasisi za michezo zimeelemewa na mzigo,kuna kila dalili kwa sekta hii kuyumba huko mbele,hawa nao wameelemewa na mzigo hawa,wasaidie kuutua.

9.Mh Rais huko halmashaurini huko,hawezekana hawasemi ila sisi tunawasikia wakilalamika kuwa wameelemewa na mzigo wa miradi isiyotekelezeka kwani pesa nyingi wanazoomba hazipelekwi na zinazopelekwa hazipelekwi kwa wakati,Mh Rais wakurugenzi unaweza dhani hawafanyi kazi kabisa,hapana
mabadiliko ya kisera yamewabebesha mzigo mkubwa na umewaelemea,huu mzigo nao wanautuaje?

Mh Rais,walioelemewa na mizigo ni wengi na siyo wale tu waliokuwa CCM na kwenda upinzani,mizigo haipo kwenye siasa pekee.
 
Yeye anadhani kuua vyama vya upinzani ndiyo atapata credit??

Anachosahau yeye ni kuwa kwake ni rahisi kuua vyama makini vya upinzani, kwa kuwa kwa kutumia uKamanfaa in Chifu wake atayaagiza majeshi yake yatangaze matokeo anayoyataka yeye!

Pamoja na yeye kuwa supported na NEC+DED's+Jeshi la Polisi+ Immigration

Lakini akumbuke kuwa upinzani upo ndani ya mioyo ya mamilioni ya watanzania na siyo kwenye vyama, kama "institutions" kama anavyodhani yeye!
 
Mizigo ni mingi sana ila yeye anaiyona ya kisiasa tu.o_Oo_O
 
Mtu usiyejua bei ya chakula unachokula, juice unayokunywa, matibabu unayotumia, malazi uliyolalia, maji unayokunywa na kuogea, umeme na hata suti uliyovaa, ni ngumu sana kuelewa mizigo walioyobeba wanchi.
 
Huo ndio ukweli huku mtaani hali ni ngumu mno...kweli mwenye shibe hamjui mwenye njaa,bei zabidhaa zinatisha wala hakuna MTU anajali wako bizzy na kiki.Sio kila msomi ni kiongozi,wengine ni makapi tu ya wasomi serikali imejaza PhD holders kwenye uongozi mambo yako hovyo kiasi hiki!!hakyaMungu sitakaa niwaamini wasomi WA nchi hii tena.
 
Mungu akubariki Dotto Bulendu,hakika umeiongelea 78% mizigo inayowaelemea 80% ya Watanzania.
Mizigo ya wanasiasa imeelekezwa kwa kuitua,je kwa hawa 80% ya Watanzania ambao si wanasiasa na wana mizigo imewaelemea wakaitue wapi?
Nasubiri jibu.
 
Wana JF mm huwa najiuliza sana swali bila majibu hii hama hama ya wanasiasa inayofanyika bara chanzo nn mbona zanzibar hamna hali kama hiyo ya viongozi kuhama je Zanzibar siasa imekuwa sana au viongozi wanajali wananch kuliko maslahi yao?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom