Magufuli: Mimi ndio Rais, ninajua siri zote za nchi

HOTUBA YA JPM ITAKAYOISHI MILELE NA KUREJEWA NA VIZAZI VIJAVYO

Nanukuu

Mimi ndio Rais ninajuwa siri zote za Nchi hii. Linisingeweza kuzungumza haya kama haya ninayozungumza siyajui,ni kuguswa tu na roho mtakatifu nashindwa kuwataja, tumechezewa mno ndiyo maana nayasema haya hadharani ndugu zangu kwamba tumechezewa mno.

Nataka niwahakikishie ndugu zangu katika awamu hii ya 5 chini ya Uongozi wangu HAKUNA KUCHEZEWA. Waje wanalia, Waje wanazunguka, Watajitahidi kutuchonganisha lakini tuseme hakuna kuchezewa. NI AIBU! Tanzanite zilikuwa zinasombwa tu?

Ndio maana nchi inayoongoza kuuza Tanzanite Duniani sio Tanzania! 🇹🇿 Nchi ya pili inayoongoza kuuza Tanzanite sio Tanzania! 🇹🇿 Wakati Madini ya Tanzanite yako Tanzania tu😣 🇹🇿. Na ndio maana yaliitwa Tanzanite kutokana na neno Tanzania 🇹🇿.

Fedha zote zilizokusanywa za Tanzanite duniani,Tanzania imepata asilimia tano (5.%) Asilimia tisini na tano (95.%) zimeliwa na wengine wa nje, mnataka ndugu zangu niache kulizungumza hili? sasa nilichaguliwa kuwa Rais wa nini? kama sitazungumza huu uozo hadharani? Nikakae kimya tu kwa kumuogopa nani? Sababu ya maisha yangu?

Si nafuu nizikwe kaburini lakini niuseme ukweli Watanzania waujue? Kwa hiyo ninataka kuwaambia ndugu zangu vita ya uchumi ni ngumu zaidi kiliko vita ya kawaida, kumnyang'anya Mtu alichozowea kukipata bure! Na kuwadharau watanzania ni mambumbumbu, wapumbavu Wajinga, si jambo rahisi, ndio maana nawaomba sana wote tusimame kwa pamoja tuwe wa moja tupiganie haki zetu.

Siku zote nawaambia ndugu zangu sio kwamba sina damu, au sio kwamba mimi sipendi hela. NAJUA MKIAMUA TUTAFIKA.
R.I.P. JPM🙏🙏🙏 😭😭😭,MWAMBA, SHUJAA SIMBA WA VITA🇹🇿

PUMZIKA KWA AMANI MWANA WA AFRIKA
Ndio maana alishindwa kuongeza elfu 20 kama za Sir-100
 
Back
Top Bottom