Magufuli, mgombea asiye na agenda kwa taifa (Tanzania) na Watanzania!

KATASAN'KAZA

JF-Expert Member
Jul 24, 2013
3,098
1,345
Tangu uanze mchakato wa kutafuta wagombea urais nimekuwa nikifuatilia kwa umakini wagombea wote wa vyama mbalimbali waliojitokeza kutia nia wakitafuta kuwakilisha vyama vyao kugombea urais.
Kila mmoja.

Kwa leo nikijikita kumtaza mh. John Pombe Magufuri mgombea urais kwa tiketi ya CCM.

Binafsi kwangu magufuri namwona km mgombea pendwa kwa wafuasi wake ila asiye na AGENDA MAALUM KWA TAIFA NA WATU WAKE kubabaika kwa mgombea huyu ni nilianza kumwona tangu alipokuwa anatafuta wadhamini mkoani kiukweli hakuwa na agenda ya msingi.

Kwa mara nyingine kaonekana kukosa agenda wakati wa mchakato wa kumtafuta mgombea wa CCM mjini Dodoma, mara kadha kila alipopata nafasi ya kujiwlezea alionekana kuduwaa na kushia kushangaa na kuzubaa jukwaani akitumia misemo ya michezo ya watoto maarufu kama KHADIJA ALISELEMA...! KHADIJA ALISELEMA...! hii ni aibu kubwa sana mtu anayetafuta dhamana ya ridhaa ya watanzania kuwaongoza huku akionekana hana shabaha/ ajenda mahususi licha ya kuwa na ilani ya chama chake.

Bila shaka ninaposema hana agenda mahususi naeleweka nchi hii ina mambo mengi na changamoto za kutosha nilitegemea kumuona akijipambanua katika kueleza kinaga ubaga nini lengo kuu la yeye kuwania urais. Akisema anataka kuingoza Tanzania na watu wake binfsi haitoshi kuwa agenda mahususi kwa magufuri kunishawishi kuwa ana uwezo wa kuongoza.

Nimalizie kwa kusema watanzania tuwe makini hasa wenye uwezo wa kupambanua mambo kwa weledi wakutosha ili tusaidie kupiga kura halali kwa maana kura yako umpe mtu kwa lengo maalum hasa baada ya kufanya upembuzi na kuwapima wagombea wote. Ili kura yako iweze kuongoza mabadiriko chanya kati ya kura zisizo halali au kura zisizopigwa.

NAMALIZA KWA KUSEMA KAMA KUNA WAGOMBEA WASIO NA AGENDA MAHUSUSI PIA YAWEZEKANA KUWA NA WAPIGA KURA WASIO NA AGENDA MAHUSUSI.

KWANGU AGENDA MAHUSUSI NI MABADIRIKO BAAAASIII...!
 
wewe mgombea wako anafahamika agenda yake ya ufisadi. magufuli utamtambua kuanzia tarehe 22 august.
 
Kwa mara ya kwanza alipewa nafasi ya kutoa japo dira kwenye kuomba kura za wanec akanifanya nimuone bado sana. Badala ya kushawishi anatafuta kura za huruma. Huku akijinyenyejesha bila sababu za msiingi. Mama migiro alimzidi kujieleza. Scientist wangu aliniangusha hadi leo sina imani nae ktk mabadiliko.

Bora kuunga mkono furiko . Ccm wakaretreat wenda watarudi wakiwa na akili za kidigitali.
 
Anayo agenda bhana SITAWAANGUSHA SITAWAANGUSHA SITAWAANGUSHA SITAWAANGUSHA SITAWAANGUSHA SITAWAANGUSHA SITAWAANGUSHA SITAWAANGUSHA
 
Napenda kuwahakikishia. Sita waangusha. Napenda kuwathibitishia. Ukimwambia asiseme hayo maneno. Ataomba mwenyew kushuka jukwaanis
 
Umeeleza kweli tupu na wala sio chuki.

Hawezi kueleza wazi na kupambanua malengo yake.

Kikubwa utamsikia akisema "sitawaangusha, niaminini, nitumeni"
 
Teh teh teh mkinichagua nitasimamia ilani ya chama.....nawahakikishieni sitawaangusha....

Yaan hiyo ya ilani ya chama mm huwa napata hofu juu ya watanzania na uelewa wao km hadi leo mtu anasimama na kusema atailinda na tena kwa ghalama yoyote ambayo ni KODI zetu ILANI ya ccm na bado wanashabikia SHAME itakuwa hili taifa watu wake ni wehu na hawajui nn kinaendelea kwenye hizo ilani zao . maendeleo hayahitaji ilala ya chma bali ilani ya TAIFA ili kuwa na usawa na ugawanywaji wa lasirimali za taifa kwa maslai wa watanzania wote sio kundi la wana ccm tu . eleweni hiloooooooo
 
Back
Top Bottom