Magufuli/Lukuvi hamisheni watumishi wa iliyokuwa CDA Dodoma

IGUDUNG'WA

JF-Expert Member
Oct 22, 2011
2,071
1,314
salaam,

Nipo hapa ofisi za manispaa ya dodoma kitengo cha ardhi zamani ikifahamika kuwa ni CDA dodoma. Ninachokiona hapa hakuna kilichobadilika tangu rais magufuli aivunje hii cda, migogoro na malalamiko ya walala hoi bado ni vilevile.

Nimekuwa nikifatilia hati kwa muda wa wiki mbili sasa lakini naambiwa file langu halionekani na kama nataka litafutwe basi nitoe ya chai apewe mtu alitafute maana wafanyakazi waliokuwa wakitafuta mafaili walikuwa wakujitolea na sasa hawapo.

wananchi wanapata shida sana na hii ofisi wanashinda hapa wakipewa majibu kuwa hakuna network sasa najiuliza hivi network ya selikali huwa ni ya mtandao gani kiasi kwamba kila siku hakuna network?

Ombi langu kwa waziri, ili kuondoa ukiritimba wa cda dodoma hamisha watumishi wote waliopo maana jina limebadilika tu kutoka cda kwenda manispaa lakini urasimu ni ule ule
42c82ff45b011faafdaf4d32373640ad.jpg
2ed21a18a9bed756edcaa8734066c88b.jpg
84dfa2985326f38b6e47540e6e8ddff3.jpg
 
Back
Top Bottom