Magufuli: Lipumba amevunja sheria kupanda punda kwenye lami

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,080
Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, jana alitumia mkutano wa kampeni kumpiga vijembe Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba kuwa alivunja sheria za nchi alipopanda punda na kumtembeza kwenye barabara ya lami katika uzinduzi wa kampeni za chama hicho wakati wa maandamano yaliyoishia Uwanja wa Sokoine.

Dk Magufuli ambaye hakumtaja kwa jina Profesa Lipumba alisema kitendo hicho kilikuwa ni kinyume cha Sheria namba 13 ya mwaka 2007 na Sheria namba 18 ya mwaka 2008 ya Mambo ya Ngozi.

“Hata sheria namba 19 ya mwaka 2008 ya Ustawi wa Wanyama huwezi ukampanda punda anavuja damu eti unakwenda kwenye kampeni… msichague watu ambao hawajui hata sheria,” alisema Dk Magufuli.

Cuf.jpg

Source: Mwananchi
 
Bigirita

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
15,866
7,161
kama anataka sarakasi za siasa uchwara, aendelee tu!!!
tutamwambia aturudishie nyumba zetu za serikali na zile alowauzia mahawara zake na ndugu zake!!!
 
Madcheda

JF-Expert Member
Feb 18, 2009
422
68
Ndugu yangu Dkt. Magufuli umebaki wewe tu msafi ndani ya Chama cha Magamba uwe makini tusije tukakuona na wewe "gamba". Tulia

Magufuli ana usafi gani?me namuona mnafiki kma sitta tu,mana huyu huyu ndo aliuza nyumba za serikali bei ya kutupa mpk saiv tunalipia mawaziri kukaa hotelin, hana usafi huyu ni mpenda sifa tu
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,339
38,982
are you serious yaani Magufuli naye ameingia this low? Really? Hivi msimamo wake kuhusu ufisadi nchini ukoje? anasimama wapi kwenye ufisadi wa EPA, Kagoda, Meremeta? Niliwahi kusema mahali pengine kuwa bila madaraka he is silent, with power ana sauti sana..
 
Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,877
6,831

Unashangaa nini wakati tunajua wazi hata ungekuwa na akili ya kuvumbua dawa ya kuotesha nywele kwenye vipara ukishaingia CCM jua umeshazama ndani ya dimbwi la maji machafu lililojaa viluilui vya vyura na utaishia kujaza maji kooni na kuyatapika nje ya dimbwi na wastaarabu wanapita na kushangaa uchafu unaotokamo.
 
Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,877
6,831
Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, jana alitumia mkutano wa kampeni kumpiga vijembe Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba kuwa alivunja sheria za nchi alipopanda punda na kumtembeza kwenye barabara ya lami katika uzinduzi wa kampeni za chama hicho wakati wa maandamano yaliyoishia Uwanja wa Sokoine.

Dk Magufuli ambaye hakumtaja kwa jina Profesa Lipumba alisema kitendo hicho kilikuwa ni kinyume cha Sheria namba 13 ya mwaka 2007 na Sheria namba 18 ya mwaka 2008 ya Mambo ya Ngozi.

"Hata sheria namba 19 ya mwaka 2008 ya Ustawi wa Wanyama huwezi ukampanda punda anavuja damu eti unakwenda kwenye kampeni… msichague watu ambao hawajui hata sheria," alisema Dk Magufuli.

Cuf.jpg

Source: Mwananchi

Sijapata kushuhudia mshamba kama Magufuli. Akitembea miji Majiji makubwa kama New York, London na miji mingine atashangaa kuona polisi wanatumia farasi ndani ya mitaa yenye msongamano mkubwa wa magari na watu kufanya doria majira ya mchana.

Polisi Tanzania kuna kikosi cha farasi ambao hufanya kazi ya doria mijini, Pombe hajui na sheria hiyo ni kwa ajili ya Igunga tu?

Akifika jiji alilokuwa Star wetu wa NBA Hashim Memphis ndio atapotewa na kumbukumbu kabisa atakapoona train ya abiria na magari ya kawaida wanapita njia moja, taa za barabarani na sheria nyingine za usalama train na magari vinatii pamoja na kuwapisha wapita njia na wakati huo train na magari yanaenda sambamba na train huku train na magari kusimama kuyapisha yanayokatiza.

Huyu Pombe ni pombe kweli, sikufikiria ni mmoja aliye kwenye ile list.
 
Gaijin

JF-Expert Member
Aug 21, 2007
11,815
5,230
"Amburuze mahakamani" kama CCM wanavyotumia kauli hiyo kwa vyama vya upinzani
 
Anheuser

JF-Expert Member
Mar 23, 2011
1,946
661
huyu huyu ndo aliuza nyumba za serikali bei ya kutupa mpk saiv tunalipia mawaziri kukaa hotelin
Magufuli ndie aliyeamua nyumba ziuzwe? Na yeye ndie alipanga bei?

Sijapata kushuhudia mshamba kama Magufuli. Akitembea miji Majiji makubwa kama New York, London na miji mingine atashangaa kuona polisi wanatumia farasi ndani ya mitaa
Magufuli amesema Lipumba amevunja sheria za "New York, London na miji mingine"?
 
Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
10,942
5,886
Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, jana alitumia mkutano wa kampeni kumpiga vijembe Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba kuwa alivunja sheria za nchi alipopanda punda na kumtembeza kwenye barabara ya lami katika uzinduzi wa kampeni za chama hicho wakati wa maandamano yaliyoishia Uwanja wa Sokoine.

Dk Magufuli ambaye hakumtaja kwa jina Profesa Lipumba alisema kitendo hicho kilikuwa ni kinyume cha Sheria namba 13 ya mwaka 2007 na Sheria namba 18 ya mwaka 2008 ya Mambo ya Ngozi.

“Hata sheria namba 19 ya mwaka 2008 ya Ustawi wa Wanyama huwezi ukampanda punda anavuja damu eti unakwenda kwenye kampeni… msichague watu ambao hawajui hata sheria,” alisema Dk Magufuli.

Cuf.jpg

Source: Mwananchi

Hivi mbona punda ndio kazi yake kukokota gari (cart) huko vijijini. Hivi watu wa Igunga watamwelewa kweli wakati huo ndio usafiri wao? Hivi ameitafsiri kweli vizuri hiyo sheria? Je, kwa nini punda hatakiwi kutembea kwenye lami? Au hatakiwi mjini? Na kama amevunja sheria si ampeleke mahakamani. Kama punda hatakiwi kupita kwenye barabara ya lami kwa nini waliijenga huku wakijua wakazi wa Igunga ndio usafiri wao? Hivi punda wana-cross vipi hiyo barabara?
 
Tony Almeda

JF-Expert Member
Sep 18, 2011
397
122
Watu wengine hawajui kuwa wanavyoongea wanazidi kukipunguzia ushindi chama chao, Huku vijijni wapi na wapi na sheria yenu ya wanyama?
 
Mvaa Tai

JF-Expert Member
Aug 11, 2009
6,161
4,434
Ndugu yangu Dkt. Magufuli umebaki wewe tu msafi ndani ya Chama cha Magamba uwe makini tusije tukakuona na wewe "gamba". Tulia
Hizi ni mbinu za Kikwete kwasababu yeye kachafuka sana, anatamani kila mtu achafuke ili yeye aonekane ni mtu wa kawaida. Kikwete ni Boss wa Magufuli lakini magufuli asikubali kila anachotumwa na Kikwete atachafuka pia.
 
BPM

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
2,761
572
kwa hili ndugu yetu magufuli anajidhalilisha ... naelewa alienda kule kwa shinikizo la magamba ili aonyeshe na kuelezea ujenzi wa madaraja na barabara kama ilani ya chama cha magamba watu wakichague
 
Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,877
6,831
Magufuli ndie aliyeamua nyumba ziuzwe? Na yeye ndie alipanga bei?

Magufuli amesema Lipumba amevunja sheria za "New York, London na miji mingine"?

Bado hujui kuwa Tanzania katika jeshi la polisi kuna kikosi cha farasi, na kikosi hicho kinafanyakazi kwenye miji mikubwa kama dar ambako kuna lami. Hii sheria ya magufuli ni kwa ajili ya lami ya Igungatu?
 
SEAL Team 6

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
655
118
Siyo kawaida kuku kuishi akiwa hana manyoya mwilini mwake. Ukiona hivyo basi ujue kaliwa, hapa CCM kwishney.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom