Magufuli Kweli Una Kazi Nzito, Hata CCM Chato Wana kudanganya!!!

Maseto

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
944
545
Jana ilikuwa sherehe za kumpongeza Magufuli na kujipongeza kwa washindi wa ubunge na udiwani nyumbani kwa Magufuli Wilayani Chato. Sherehe hizo zilianza na baraka ya mvua.
Wanachama wa CCM walifika kwenye sherehe hizo kwa njia ya miguu na magari. Wale wa mbali kama Buseresere walifika kwa magari. Nilichojifunza ni kwamba bado CCM hawajawa na mshikamano wa kutosha mkoani Geita. Kwa mfano katika sherehe hizo Mwenyekiti wa CCM Mkoa MSUKUMA hakuonekana bila maelezo yoyote ya nini kilichosababisha asiwepo.
Lakini jambo lililo nifanya niandike ni uongo uliotaarifiwa na radio RFA. Kuwa watu walitembea kwa miguu kilometa 72 kwenda kwenye sherehe hizo. Wakati watu wote waliotoka kuanzia kilometa 5 walifika kwa magari. Hakuna mtu aliyetembea kwa miguu kutoka Buseresere.
Hili ni jambo dogo lakini ndiyo utamaduni wa CCM kudanganya hata kwa mambo ambayo hayahitaji uongo.
Magufuli kama kweli anataka aondoe unafiki aanze na kuwathibiti matapeli na wababaishaji kama Viongozi wa CCM Mkoa wa Geita na Wilaya ya Chato.
Pia awathibiti mafisadi kama akina Madabida Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar.
 
Huwezi kusukuma gar ukiwa ndani yake. Unajua ni mabilion ya nani yaliyotumika kwenye kampeni yake iliyo vunja rekodi tangu chaguzi zianze tz.
 
ni ngumu sana maghufuli kupambana na ufisadi ndani ya ccm. maana kuna wengine wamemsaidia kufadhili kampeni zake...
 
[QUOTE=maseto kwani wakitembea au kupanda magari Kuna kitu kinaharibika? Tuacheni kukuza vitu visvyo na msingi tuongee Hoja za msingi Sasa
 
Back
Top Bottom