Magufuli kwa nini hakemei kukamatwa hovyo kwa viongozi wa upinzani au ndiye anayewatuma?

TL. Marandu

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
3,625
5,810
Mimi siwaelewi na Naaza Kuwadharau sana, Watu ambao Kila akitokea Mkuu wa Wilaya au Mkoa Kufanya Jambo la Kishenzi dhidi ya Wapinzani au Wananchi moja kwa moja, Basi watu hawa Wanasema Kuwa Rais hahusiki, hajawatuma.

Hawa Wakuu wa Wilaya, na Wakuu wa Mikoa wanateuliwa na Rais, Na Rais Mwenye akili Timamu hawezi Kunyamazia Wateule wake wanapofanya Mambo ambayo ni Uvunjifu wa Sheria. Kuna Matukio Mengi ya Kukera, ya Kihuni na Kihalifu yamefanywa na Wakuu wa Wilaya na wa Mikoa! Kama Kupora Rambi Rambi, Kuvuruga Misiba, Kuingilia Kihamba cha asili cha Mtu na Kuharibu Mazao tena bila hata amri ya Mahakama! Unamwingilia Mtu kwenye shamba la Asili! Ni kama Kumwingilia Magufuli Shambani kwake Chato! Kumkamata meya wa Ubungo, Kuvamia Clouds!

Rais Magufuli Kama hawatumi hawa , Yeye au Mtetezi wake yeyote hapa anieleze ni lini alishawahi Kukemea tabia hizi au kumwajibisha angalau mmoja wa Watu wake hawa Washenzi na wahalifu, maana siwezi kuwaita wahuni viongozi!

Nani Kawaloga Watanzania Mpaka wanaheshimu watu Wanaobeba Mbeleko uhuni wa aina hii?
 
Kutumia lugha nzuri hamuwezi???? Kwanini mnatukana viongozi wetu kama hamuwataki???? Lugha iliotumiwa na mleta mada kuwa RCs na DCs ni wahuni na washenzi haikubaliki....mods hawa watu wanatuharibia jukwaa letu na forum yetu kwa ujumla....
 
Mzee Magu Ana nia njema ya kukomesha wezi na wabadhilifu lakini kwa kuwa anshindwa kusimamia haki ya watu wake nina imani iko siku ataangukia pua , na nyie timu Magu unaoshabikia uoza huu eleweni mnaingamiza Tanzania
 
ww umeyaona ya upande wako he ujinga wanaofanyiwa upande as pili ni sawa au?ni sawa? Mtu mzima mwenye uelewa akikudharau kuna faida gani kumheshim?unafikiri kuwaweka ndani kunasidia? au ndo kuwatengeneza watu kuwa na ngozi ngumu hata kusema liwalo na liwe?popo ww.
 
Mzee Magu Ana nia njema ya kukomesha wezi na wabadhilifu lakini kwa kuwa anshindwa kusimamia haki ya watu wake nina imani iko siku ataangukia pua , na nyie timu Magu unaoshabikia uoza huu eleweni mnaingamiza Tanzania

Nia njema ni ile ya kuwasaidia wanyonge,nia njema siyo kujenga uwanja wa ndege Chato ambao hauna faida yeyote matumizi mabaya ya raslimali pesa.

Hana nia njema,nia yake hata yeye ni kujilimbikizia mali kama hao wengine.

Hana nia yoyote njema nia yake kuendelea kutawala bila mwisho.
 
lugha ya staha ni bora kwa kiongozi wako zaidi ya hivi ulivyoandika kati ya wewe na wao nani mhuni na mshenzi

Kiongozi anayestahili kuheshimiwa ni yule anayejiheshimu.Hawa wengine w anastahili kuitwa vyovyote vile.

Hivi hujiulizi kwanini Meck Sadick aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro haijawahi kutukanwa?

Hawa wote na aliyewateua wote ni wale wale.Majambazi na wauaji wa raslimali zetu.
 
tuache utani rais wetu mengi yansmshinda hasa kuenzi umoja na mshikamano wa taifa letu.hali inazidi kuwa mbaya....
Hata ya Kibiti ni dalili tosha. Zile kauli kuwa Polisi lazima aogopwe na RAIA hajajua zinatumika vibaya na kujenga chuki.
Kwa nini Mimi RAIA mwema nimuogope polisi? Natakiwa nimuone ni mtumishi wa umma na hata kama nimepotea mtaa kwenye mji nisioujua napaswa kumsimamisha polisi na kumwambia naenda mtaa X nionyeshe nafikaje. Lakini hawa wetu unaweza kuwa umempa sababu ya kukubambika kitu ili ikutoke hela
 
Mimi siwaelewi na Naaza Kuwadharau sana, Watu ambao Kila akitokea Mkuu wa Wilaya au Mkoa Kufanya Jambo la Kishenzi dhidi ya Wapinzani au Wananchi moja kwa moja, Basi watu hawa Wanasema Kuwa Rais hahusiki, hajawatuma.

Hawa Wakuu wa Wilaya, na Wakuu wa Mikoa wanateuliwa na Rais, Na Rais Mwenye akili Timamu hawezi Kunyamazia Wateule wake wanapofanya Mambo ambayo ni Uvunjifu wa Sheria. Kuna Matukio Mengi ya Kukera, ya Kihuni na Kihalifu yamefanywa na Wakuu wa Wilaya na wa Mikoa! Kama Kupora Rambi Rambi, Kuvuruga Misiba, Kuingilia Kihamba cha asili cha Mtu na Kuharibu Mazao tena bila hata amri ha Mahakama! Unamwingilia Mtu kwenye shamba la Asili! Ni kama Kumwingilia Magufuli Shambani kwake Chato! Kumkamata Mbunge wa Ubungo, Kuvamia Clouds!

Rais Magufuli Kama hawatumi hawa Wahuni, washenzi, na Wahalifu, Yeye au Mtetezi wake yeyote hapa anieleze ni lini alishawahi Kukemea tabia hizi au kumwajibisha angalau mmoja wa Watu wake hawa wahalifu, maana siwezi kuwaita wahuni viongozi!

Nani Kawaloga Watanzania Mpaka wanaheshimu watu Wanaobeba Mbeleko uhuni wa aina hii?
Achana nao sisi tunaendelea na Kilimo kwanza cha mihogo kule pwani kibiti siku watakapodhitukia sisi tunavuna.
 
Back
Top Bottom