Magufuli kwa level yako ni wakati wa kuwa na "big plan Dar - Moro highway"

Miimo

Senior Member
Apr 7, 2012
106
0
Wana JF
Ni siku nyingine tena tukitafakari hotuba ya budget ya mwheshimiwa Makufuli katika wizara yake.
Wengi tulitegemea kuona umahiri wa Makufuli katika kuwasilisha budget yake na kujibu maswali ya waheshimiwa wabunge na kwa hilo sinashaka na waziri Makufuli.

Nimejaribu kutafakari kuhusu swala la serikali kupitia wizara inayoongozwa na Makufuli kuwa na fikra mgando za kuendelea kupanua barabara ya Dar - Moro bila kuja na mawazo endelevu ambayo yatasaidia kupunguza msongamano na kupunguza ajali katika eneo la barabara hii. Mie napenda Kumshauri Makufuli kupitia wizara yake kuwa ni wakati sasa umefika kuanza kujenga barabara ya pili itakayounganisha kati ya Dar na Morogoro (200km). Hii itasaidia sana kuwa na barabara mbili kushoto kuelekea Moro na mbili kulia kuja Dar. Hii itaondoa ajali zote zinazotokea mara kwa mara katika kipande hiki na kupoteza maisha ya ndugu zetu na nguvu kazi ya taifa. Hili linawezekana, tena niabu kwa Taifa letu kwa kipindi cha miaka hamsini tumeshindwa kujenga hiyo barabara ya Dar-Moro katika hicho kiwango licha ya msokamano na ajali zinazotokea katika kipande hicho.

Dr. Makufuli, umetembea sana. Hivi hata hapo Ghana kama wameweza kutengeneza barabara mbili tofauti kutoka Accra hadi Ashanti (Kumasi Town) takribani 800km, kweli sisi tutashindwa kujenga kipande hiki cha Dar morogoro 200km? Mweshimiwa Makufuli naomba tu ujaribu walo kubroaden kidogo ubongo wako na kutumia shule yako katika hili.
Naamini inawezekana hata kwa mapato yetu ya ndani swala nikupunguza tu matumizi ya kawaida katika wizara mbalimbali hasa matumizi ya kawaida ya office ya waziri Mkuu. Mie najua serikali ya CCM ikishindwa kujenga hiyo barabara katika hicho kiwango, serikali yoyote ile itakayotokea out of CCM italiona hilo na kulitekeleza kwa haraka na kwa ufanisi wa hali ya juu.

Nakutakia kila la heri Pombe ukitafakari ushauri niliokupa kwa manufaa ya Taifa.

Nawasilisha.
 
Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
18,939
2,000
Akili zingine sijui ni akili za binadamu gani nani kakwambia kuwa ukubwa barabara ndiyo unaondoa ajali kama umewahi kuendesha gari unaweza kutueleza kwa kina kwa vipi ukubwa wa barabara unaweza kupunguza ajali.

Nimekubedha sana kwa hiki ulichoandika ungeweza kushauli nyongeza au upanuzi wa barabara kwa mtazamo wa kupunguza msongamano wa magari na siyo eti kuondoa foleni make ajali zinatokea kila mkoa ambako gali zenyewe inapita moja baada ya saa moja ndipo ipite nyingine lakini mizinga kila kukicha lakini wewe kwakuwa hujui mambo unaongozwa na mihemuko ya kisiasa na chuki kwa magufuli umekwenda kumdandia magufuli aibu kweli hii.
 
ligera

JF-Expert Member
May 17, 2014
2,650
1,250
hivi huyo makufuli ni nani?mbona huyo mtu ni mgeni ktk masikio yangu
 
kawakama

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
1,300
1,500
aisee huyu mwandishi sijui ni kabila gani maana
magufuli anaita makufuli
mheshimiwa anasema mweshimiwa

unapoandika post tulia usiwe kama unakimbizwa
 
TEKNOLOJIA

JF-Expert Member
Jan 6, 2014
4,306
2,000
Akili zingine sijui ni akili za binadamu gani nani kakwambia kuwa ukubwa barabara ndiyo unaondoa ajali kama umewahi kuendesha gari unaweza kutueleza kwa kina kwa vipi ukubwa wa barabara unaweza kupunguza ajali.

Nimekubedha sana kwa hiki ulichoandika ungeweza kushauli nyongeza au upanuzi wa barabara kwa mtazamo wa kupunguza msongamano wa magari na siyo eti kuondoa foleni make ajali zinatokea kila mkoa ambako gali zenyewe inapita moja baada ya saa moja ndipo ipite nyingine lakini mizinga kila kukicha lakini wewe kwakuwa hujui mambo unaongozwa na mihemuko ya kisiasa na chuki kwa magufuli umekwenda kumdandia magufuli aibu kweli hii.

Wewe nawe kwa ubishi!Ina maana hujui kwamba uwembamba wa barabara zetu zinachangia kwa kiasi kikubwa kutokea ajali za magari hapa nchini?Hata mtoto wa darasa la pili analijua hilo.Nyinyi ndiyo mnaoamini kuwa mkijenga barabara za juu eti msongamano wa magari utapungua Dar jambo ambao siyo kweli hata kidogo.Jaribuni kufikirisha akili zenu kidogo siyo mnalala lala tu shwaini nyie!!!
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,292
2,000
Mleta mada, nijuavyo, Magufuli amesema kuna mpango wa kujenga barabara kubwa ya njia sita, Dar - Morogoro kwa mpango wa barabara ya toll na wawekezaji.
 
TEKNOLOJIA

JF-Expert Member
Jan 6, 2014
4,306
2,000
Mleta mada, nijuavyo, Magufuli amesema kuna mpango wa kujenga barabara kubwa ya njia sita, Dar - Morogoro kwa mpango wa barabara ya toll na wawekezaji.

Aliizungumzia hiyo Jana Bungeni au bado inabakia kuwa kama tetesi?If that's true then are we going to get e-tolled (taxed) for using such roads just like Gauteng Province and now KwaZulu Natali is doing in South Africa?
 
kasharunga

Senior Member
Feb 28, 2013
128
0
Wewe nawe kwa ubishi!Ina maana hujui kwamba uwembamba wa barabara zetu zinachangia kwa kiasi kikubwa kutokea ajali za magari hapa nchini?Hata mtoto wa darasa la pili analijua hilo.Nyinyi ndiyo mnaoamini kuwa mkijenga barabara za juu eti msongamano wa magari utapungua Dar jambo ambao siyo kweli hata kidogo.Jaribuni kufikirisha akili zenu kidogo siyo mnalala lala tu shwaini nyie!!!
Yote sawa lakini maamuzi yetu yamekuwa ya kukulupuka ambapo mwisho wa siku mipango inakuwa vichekesho.Hivi kweli wakati wa sasa kuondoa kero Jijini Dsm ni kujenga barabara kutoka Kimara hadi kivukoni kwa stahili hiyo. Moja vituo kama maghara kama havingekuwepo naamini kulikuwa na uwezekano wa kujenga barabara ya njia sita.Tatizo la foleni halitaisha kwa sababu mkondo wa barabara ni finyu na kama gari ya mbele ikiharibika ina maana hawatapishana.Pili mfumo wa vituo/maghala ni lazima magari yenye ghorofa ndio yatumike ina maana bila hivyo magari tuliyozoea hayatafaa. Hii ina maanisha tunafunga ndoa ya kudumu na wachina ambao wanaunda mabasi hayo.Hata kama ni msaada lazima tuwe na misaada yenye tija kwa sababu Benki ya Dunia hata km wametoa Msaada tutaulipa kwa njia nyingine.Msongamano Dsm unaweza kupungua ikiwa serikali na mamlaka nyingine zikijenga barabara za michepuko zilizo imara.Wakati wakiangazi barabara hizo zinakarabatiwa lkn masika zinabomoka,Wazalendo makandarasi tumefeli sana
 
Kuna mambo muhimu lazima yafanyike ili kusaidia kupunguza traffic congestion hapo Dar:Moja,Serikali lazima ifanye maamuzi magumu ya kubomoa majengo yote yaliyojengwa kwenye mikondo ya barabara na kisha kujenga barabara hapo sambamba na zile barabara za ziada za pembeni ya jiji (bypass).Pili,Serikali ianze kujenga miundombinu ya barabara za kisasa pia katika mikoa mingine ili kusaidia kuchochea kukua kwa haraka kwa shughuli za kiuchumi kwenye mikoa hiyo na hivyo kutoa fursa za ajira kwa vijana pamoja na mambo mengine mengi ambayo kwasasa yanapatikana Dar pia yatapatikana huko kama vile ujenzi wa kumbi za starehe,mahoteli, nk as long as shughuli za kiuchumi zimechanganya,mzunguko wa fedha ni mkubwa na idadi ya watu ni kubwa sana,Pia baadhi ya miradi ingekuwa inapelekwa mikoani badala ya kuijaza hapo Dar.Haya yakifanyika yatasaidia kuondoa presha ya Dar kuwa kimbilio pekee la watu and in the long run,the traffic congestion problem in Dar will be minimized if not eradicated completely!
 
kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,157
2,000
Wizara ya Ujenzi imepanga kujenga barabara
41 na madaraja 13 nchini kwa kiwango cha
lami zenye urefu wa kilomita 3,074, ikiwa ni
pamoja na upanuzi wa barabara ya Dar es
Salaam-Chalinze yenye urefu wa kilomita 100
kwa mwaka 2014/15.
Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli,
akiwasilisha bajeti ya Wizara yake kwa mwaka
wa fedha 2014/15, alisema ujenzi wa
barabara na madaraka hayo utagharamiwa na
serikali na wahisani.
Alisema barabara ya Dar es Salaam-Chalinze-
Morogoro (km 200) kwa kiwango cha
'Expressway' utagharimu Sh. milioni 750 na
kwamba maandalizi ya utekelezaji wa mradi
huo yanaendelea na utatekelezwa baina ya
serikali na sekta binafsi.
Dk. Magufuli alisema awamu ya kwanza
itakuwa kilomita 100 kutoka Dar es Salaam
hadi Chalinze na kiasi cha Shilingi milioni 100
zimetegwa.
Alisema barabara nyingine ni Wazo hill-
Bagamoyo itakayogharimu shilingi milioni
10,885.24 ikiwa ni pamoja na kujenga kwa
kiwango cha lami sehemu ya Bagamoyo-
Makofia-Msata kilomita 64 na ujenzi wa
daraja la Ruvu Chini.
Barabara nyingine ni Usagara-Geita-
Kyamyorwa kilomita 422, kigoma -Kigahwe-
Upinzani-Kaliua -Tabora, Marangu -Tarakea-
Kimwanga-Bomong’ombe- Sanya Juu yenye
urefu wa kilomita 173, Arusha -Moshi-Holili
kilomita 140, lengo ni kuchochea ukuaji wa
Utalii katika Mlima Kilimanjaro.
Nyingine ni Same -Himo –Marangu- Rombo -
Lushoto kilomita 132, Kia-Mererani kilomita
26, Kwa Sadala Machame-Masama-Machame
kilomita 15.5 na Kiboroloni Kiharara-Tsudini-
Kidia kilomita 10.80 zote zikigharimu Sh.
milioni 13.133.63.
Barabara ya Nangurukuru-Mbwemkulu
kilomita 95, Dodoma - Manyoni Kilomita 127,
Mbwemkuru-Mingoyo kilomita 95, Dumila -
Kilosa kilomita 78, Sumbawanga -Matai-
Kasanga kilomita 112.
Nyingine ni Kayka-Bugene-Kasulu kilomita
178, Isaka-Lusahunga kilomita 242 na
Lusahunga-Rusumo na Nyakasanza -Kobera
kilomita 150, Manyoni-Itigi -Tabora na
Korogwe -Handeni.
Madaraja yatakayojegwa ni ya Kirumi,
Nangoo, Sibiti, Maligisu, Kilombero, Kavuu,
Mbutu, Rehekei, Ruhuhu, Mombo, Simiyu,
Wami na Lukuledi II. Hata hivyo, urefu wake
haukutajwa.
Alisema baadhi ya barabara ilishaanza ujenzi
na nyingine ndiyo zitaanza huku madaraja
yakiwa katika hatua mbalimbali ya ujenzi na
mengine yakihitaji upanuzi.
Barabara za mikoa zitakazokarabatiwa ni za
kilomita 685 za changarawe na za lami
kilomita 78.
CHANZO: NIPASHE
 
Mwakyonde

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
244
170
Akili zingine sijui ni akili za binadamu gani nani kakwambia kuwa ukubwa barabara ndiyo unaondoa ajali kama umewahi kuendesha gari unaweza kutueleza kwa kina kwa vipi ukubwa wa barabara unaweza kupunguza ajali.

Nimekubedha sana kwa hiki ulichoandika ungeweza kushauli nyongeza au upanuzi wa barabara kwa mtazamo wa kupunguza msongamano wa magari na siyo eti kuondoa foleni make ajali zinatokea kila mkoa ambako gali zenyewe inapita moja baada ya saa moja ndipo ipite nyingine lakini mizinga kila kukicha lakini wewe kwakuwa hujui mambo unaongozwa na mihemuko ya kisiasa na chuki kwa magufuli umekwenda kumdandia magufuli aibu kweli hii.
Hata upana wa barabara unasaidia kupungua ajali, na kuondoa foleni pia acha kushutumumu wenzio hawajui wakati ndio unaonekana kutokujua zaidi
 
mshamu

JF-Expert Member
Aug 5, 2011
417
250
Akili zingine sijui ni akili za binadamu gani nani kakwambia kuwa ukubwa barabara ndiyo unaondoa ajali kama umewahi kuendesha gari unaweza kutueleza kwa kina kwa vipi ukubwa wa barabara unaweza kupunguza ajali.

Nimekubedha sana kwa hiki ulichoandika ungeweza kushauli nyongeza au upanuzi wa barabara kwa mtazamo wa kupunguza msongamano wa magari na siyo eti kuondoa foleni make ajali zinatokea kila mkoa ambako gali zenyewe inapita moja baada ya saa moja ndipo ipite nyingine lakini mizinga kila kukicha lakini wewe kwakuwa hujui mambo unaongozwa na mihemuko ya kisiasa na chuki kwa magufuli umekwenda kumdandia magufuli aibu kweli hii.

Ndugu kwa kujibu hivi umekurupuka sana tu yani wewe ndo umeleta siasa hapa jamaa kasema kupunguza ajali siyo kumaliza kabisa ajali na siyo kutanua barabara bali kujenga nyingine kabisa wanaokwenda moro barabara yao na wanaotoka moro barabara yao. Sijui na mimi umenielewa au unasikia harufu ya siasa pia kwenye maelezo yangu.
 
Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
23,300
2,000
Mimi ningeshauri ile Pugu Road kuanzia Tazara hadi Ukonga iongezwe lane moja zaidi kwa ajili ya malori, yasipite tena Ubungo. Kutoka Ukonga wapanue njia mbili mpaka Pugu-Kisarawe-Kibaha Mizani
 
Eliphaz the Temanite

JF-Expert Member
Jan 19, 2010
3,016
2,000
Akili zingine sijui ni akili za binadamu gani nani kakwambia kuwa ukubwa barabara ndiyo unaondoa ajali kama umewahi kuendesha gari unaweza kutueleza kwa kina kwa vipi ukubwa wa barabara unaweza kupunguza ajali.

Nimekubedha sana kwa hiki ulichoandika ungeweza kushauli nyongeza au upanuzi wa barabara kwa mtazamo wa kupunguza msongamano wa magari na siyo eti kuondoa foleni make ajali zinatokea kila mkoa ambako gali zenyewe inapita moja baada ya saa moja ndipo ipite nyingine lakini mizinga kila kukicha lakini wewe kwakuwa hujui mambo unaongozwa na mihemuko ya kisiasa na chuki kwa magufuli umekwenda kumdandia magufuli aibu kweli hii.

Mitanzania ndinyo tulivyo ubishi na ujuaji mwingii ...Ushamba tu
Nani asiyejua highway ndio mwarobaini wa mafoleni yasiyo na kichwa wala miguu, magufuli anakuja na proposal za kupanua barabara kweli ???? Hivi inahitaji uwe genius kwa mfano kujenga barabara itakayo divert malori yanayopita mandela -morogoro road ???????? Ni kiasi gani utapunguza foleni ukiondoa malori yanayojazana morogoro road kuja bandarini ?????
Kutwa kukariri km za barabara planing zeroooo sijui barabara ya Nangurukuru....Mchambawima km 500, pesa inayoengwa 1b wizi mtupu
Solution ya matatizo ya foleni na misongamano hasa kwa jiji la Dar ambalo ndio injini ya uchumi wa nchi
1. Highway angalia za wenzetu hiii iko Nairobi tu hapo
131963782_31n.jpg

2. Feeder Roads (Barabara za michepuko)
3. Kuimarisha mtandao wa public transport BRT, tram ect
4. Fly overs
Tuambie hayo tutakuelewa sana, Huu ----- tunaoelezana hapa sijui kupanua Bagamoyo road ni kupoteza muda na rasilimali za nchi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom