Magufuli kutumia FFU kubomoa nyumba; Asema hana simile kwa wote wanaojiita matajiri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magufuli kutumia FFU kubomoa nyumba; Asema hana simile kwa wote wanaojiita matajiri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 1, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=3][/h]

  *Atapambana na wanaojenga hifadhi za barabara
  *Asema hana simile kwa wote wanaojiita matajiri
  *Asisitiza kuoneana aibu hakutatufikisha mbali

  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption"]Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana ambapo pamoja na mambo mengine alisema sasa wizara hiyo itawatumia Askari Polisi Kikosi cha FFU kuwakamata watu wote wanatumia hifadhi ya barabara kwa shughuli zao binafsi.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  Na Benjamin Masese

  WAZIRI wa Ujenzi Dkt. John Magufuli anatarajia kufanya oporesheni kali kwa kutumia kikosi cha kutuliza Ghasia (FFU) kupambana na
  watu waliojenga nyumba, gereji, vituo vya mafuta, kufanya biashara, kuegesha magari katika hifadhi za barabara wakati wa ubomoaji wa majengo hayo.

  Pia amesema pia ataanzisha mapambano dhidi ya watu wanaojiita matajiri na kiburi cha kutofuata sheria zilizowekwa na kusainiwa na Rais katika kuendesha shughuli zao kwa kuwa nyimbo za malaika alizoimba zimekwisha na sasa kilichobaki ni kutumia sheria.

  Alisema hayo jijini Dar es Salaam jana wakati akizungumza na wandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru katika sekta ya ujenzi yanayofanyika kwa wiki moja kuanzia leo pamoja na kuelezea mafanikio yaliyopatikana tangu Tanganyika ipate uhuru mwaka 1961.

  Mbali na maadhimisho hayo alisema kuanzia Septemba 5 hadi 7 mwaka huu Rais Jakaya atakutana na wakandarasi wote nchini, wadau wa ujenzi kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kuzungumzia sekta ya ujenzi.

  "Nimeimba nyimbo zote za malaika za kuwataka hawa wanaojenga katika hifadhi za barabara sambamba na wale wanaofanya biashara, kuegesha magari, wauza mbao, gereji, mabango, vituo vya mafuta sasa nimechoka na nimeishiwa nyimbo zilizobaki ni nyimbo za sheria.

  "Tayari nimefanya mazungumzo na IGP na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani wote wamekubali kunipatia askari kutoka FFU na wale wa usalama wa barabarani. Operesheni kali itaanzia mkoa wa Dar es Salaam wakati wowote, wananchi wakae mkao wa kufuata sheria la sivyo ukikamatwa umepaki pasipotakiwa faini ya papo kwa papo sh. milioni moja," alisema.

  Dkt. Magufuli alisema kuwa watendaji wa sasa wamekuwa watu wa ajabu sana kutokana na kushindwa kufuata sheria na kusababisha wananchi wa kawaida kufuata mkumbo hali inayoashiria nchi kutaka kurudi enzi za ukoloni na kuwataka kufuata sheria ya mwaka 1977 ibara ya 26 kifungu cha kwanza na pili ambacho kinamtaka raia yeyote kuwa na wajibu wa kulinda katiba na sheria.

  Pia alisema kuwa sheria inamtaka kila mwananchi kuheshimu hifadi za barabara huku akisisitiza watu kufuatilia historia za sheria za nchi ilivyokuwa tangu enzi za ukoloni mpaka sasa.

  Dkt. Magufuli alisema kuwa sheria zikifuatwa na kila kiongozi na mwananchi bila kulindana na kuogopana, nchi itapata maendeleo makubwa na ya haraka kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali inayoibuliwa pia itaendelea kuwa kisiwa cha amani miaka 50 ijayo.

  "Tukiendelea kupiga kelele za kuoneana aibu hatutafika mbali lazima tufanya maamuzi kama yaliyofanyika Kenya. Kenya majengo marefu yaliangushwa lakini hapa Tanzania ukitaka kubomoa sheli utakiona, watu wanaibuka kutetea maovu na kusimamia kesi mahakamani, itakumbukwa mwaka fulani tulishitakiwa kwa kubomoa nyumba lakini huyo watendaji walioko serikalini leo ndio waliosimamia kesi ya walalamikaji. Sasa tutafika,"alisema.

  Alisema kuwa kutokana na sheria kufuatwa jumla ya wakandarasi 2,008 wamefukuzwa kazi na kufutiwa leseni ya ujenzi akiwemo aliyesimamia ujenzi Barabara ya Kilwa ambayo inatarajiwa kurudiwa upya na tayari ubalozi wa Japani umewaomba radhi Watanzania.

  Dkt. Magufuli alisema kuwa jumla ya wakandarasi 14,000 nchini wamesajiliwa na kati ya hao 7,000 ni wazalendo na kuongeza kuwa ataendelea kufuatilia mmoja baada ya mwingine katika utendaji wao wa kazi ili kubaini udhaifu wao na kuwafutia leseni.

  Akizungumzia mafanikio yaliyopatikana tangu uhuru katika sekta ya ujenzi alisema hakuna asiyeona kuwepo kwa mabadiliko ya maendeleo ambapo hali halisi inajionesha katika barabara, nyumba za serikali na huduma za ufundi na vivuko.

  Dkt. Magufuli alisema juhudi zilizofanywa na serikali zimewezesha mtandao wa barabara kupanda kutoka kilomita 33,600 zilizokuwepo mwaka 1961 hadi kufikia kilomita 86,472 mwaka 2011.

  Alisema mafanikio katika sekta ya barabara yameleta mchango mkubwa katika kuinua uchumi wa taifa kwa jumla na kuongeza kuwa sekta nyingi zinafanya kazi kwa kutegemea barabara.

  Pia alisema kuwa wakati Tanganyika inapata uhuru, serikali ilikuwa na magari yaliyosajiliwa 38,000 yakiwemo ya serikali na watu binafsi lakini sasa yanakadiriwa kuwa zaidi ya milioni 1.5 huku watu wakiwa milioni 9.54 ambapo leo ni zaidi ya milioni 40.

  Alisema wakati huo barabara zilizokuwa za lami zilikuwa kilomita 1,300 sasa ni kilomita 6,500 na zinazotarajiwa kumailika ni kilomita 11,154 na kufanya jumla ya kilomita 17,700 baada ya miaka mitatu. Pia vivuko havikuwepo lakini sasa vipo vivuko 23 na madaraja yamefikia 4,480.

  Dkt. Magufuli alisema bajeti ya kwanza iliyotengwa katika sekta ya ujenzi ikiongozwa na Waziri BwAmir Jamal (1961-1963) ilikuwa sh.bilioni mili lakini sasa sh.trilioni
  1.496.

  Hata hivyo Dkt.Magufuli alizungumzia miradi ya maendeleo inayoendelea ikiwemo ujenzi wa barabara za juu, mabasi yaendayo kasi (DART), ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Mifuko ya Barabara, Wakala wa Ufundi na Umeme, Wakala wa Majengo, Usalama wa Barabara na Mazingira, sera na sheria.
   
 2. regam

  regam JF-Expert Member

  #2
  Sep 1, 2011
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 268
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Demolition of structures erected on road reserves in Dar es Salaam will resume soon, Works minister John Magufuli said yesterday. Briefing journalists on the ministry's participation in activities to mark Tanzania's upcoming 50th independence anniversary, Dr Magufuli said structures built on road reserves would be pulled down to ease congestion in the city.

  He dismissed criticism of the operation, saying the ministry was acting within the confines of the law by clearing road reserves of illegally built structures, adding that he had sworn to uphold the rule of law.

  Dr Magufuli urged Dar es Salaam residents to cooperate with the ministry in its endeavour to stop encroachment on road reserves. "We have good plans aimed at reducing traffic jams on Dar es Salaam roads. People should support us when we start implementing them...it's not our intention to make people's lives difficult.

  On the contrary, we want to improve people's lives." Dr Magufuli said the ministry had asked for the assistance of the feared Field Force Unit (FFU) when carrying out demolitions in Dar es Salaam.

  "We do not plan to use force, but one never knows how these law breakers will react, hence the need to have the police at our disposal," he added. He warned those with businesses or structures on road reserves that ignorance of the law was not an excuse, and those who would be arrested would be penalised, adding that the fine for such an offence was not less than Sh1 million.

  "When you look at our roads you will notice that a lot of space has been illegally taken up by businesspeople, who have been selling their merchandise on reserves, inconveniencing road users." Dr Magufuli urged those who would be involved in the exercise to do their job expeditiously as "they will play a key role in reducing traffic jams in Dar es Salaam".

  "We should all work together to ensure that we do the job as required and take legal measures against all law breakers. Traffic jams in Dar es Salaam cost the economy billions of shillings every day...we can't allow this to continue because we need this money for development," he said.

  On other plans to reduce congestion in Tanzania's commercial capital, Dr Magufuli said the ministry had completed a feasibility study on the construction of a flyover at the junction of Nyerere Road and Mandela Expressway, and the government was looking for investors to partner it in the project.

  "We will soon float tenders so that the project can start as soon as possible...this is among our plans to address chronic congestion in Dar es Salaam," he said. Another plan is the construction of a dual carriageway from Morocco area to Tegeta. Work had already begun on the Mwenge-Tegeta stretch of the road, Dr Magufuli said.

  Construction of the Kigamboni Bridge across the Magogoni Creek would start soon, the minister said, adding that the National Social Security Fund (NSSF) would provide 60 per cent of the funds for the project, with the ministry providing the remaining 40 per cent.

  "NSSF has already provided the funds, and the project is currently in its initial stages."A plan is also underway to use ferries to transport people between Dar es Salaam and Bagamoyo. "The project is set to start soon, and we hope that it will do a lot to reduce traffic jams along Bagamoyo Road and at the city centre," he said.

  Dr Magufuli also put incompetent contractors on notice, warning that the ministry would effectively use the law that empowered it to deregister such firms.
   
 3. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,068
  Likes Received: 6,522
  Trophy Points: 280
  kama watu wamelipwa fidia zao mi naona ni sawa kwani foleni imezidi mno.
   
 4. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #4
  Sep 2, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  FFU tena? Ina maana polisi wa kawaida wameshindwa? Kama kubomoa tutatumia FFU basi maandamano ya CHADEMA tusishangae kusikia jeshi linatumika.

  Tungetumia uhamasishaji kisha zoezi lisimamiwe na polisi wa kawaida FFU tuwaache na virungu vyao huko huko kwao.
   
 5. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #5
  Sep 2, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Na ile kauli ya rais kuwa asuburi hadi miaka miwili anaipotezea? Vipi si rais alisema pia kuwa wale ambao barabara iliwakuta walipwe - hivi wamelipwa?
   
 6. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #6
  Sep 2, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Mia Kwa Mia magufuli chapakazi tumechoka na maneno ya kuwa huyu ni kigogo au huyu ni kibosile au huyu ni tajiri,sema nao kieleweke kama namna gani omba hata jeshi mzee,tumechoka na uvunjaji wa sheria kiasi kuwa imekua mazoea na watu wamekuwa wako juu ya sheria.Pamojjjjjjjjjjjjja kwa sana tu.
   
 7. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #7
  Sep 2, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,984
  Likes Received: 729
  Trophy Points: 280
  Mr. Misifa kazini.Lile jengo la TANESCO pale Ubungo vipi?
   
 8. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #8
  Sep 2, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,292
  Likes Received: 19,446
  Trophy Points: 280
  daraja liko wapi? hajachoka kuimba wimbo wa daraja la kigamboni?
   
 9. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #9
  Sep 2, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mkuu unanufaika na ujenzi holela nini? Mbona malengo ya Dr. Magufuli ni mazuri kwa taifa zima kwa sasa na vizazi vijavyo. Wewe unachoona ni misifa. Na nimegundua kuwa viongozi wazuri ni wale wachapa kazi kwa kuhitaji sifa ndo maana hata shuleni watu hao hupewa ukiranja na umonitor. Upoooooooooo?
   
 10. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #10
  Sep 2, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Tabia za watu wa aina yenu ndio wamechangia kuludisha Nchi hii nyuma,nini Maana ya Neno SIFA.Neno sifa ni neno la kiswahili lenye maana ya pongezi ya zitolewazo kwa mtu aliyetenda jambo au kitu kizuri mbele ya wenzie.

  Tumezalisha utamaduni wa wapumbavu wa kariba na muono wako wametapakaa Nchi nzima ambao wamezuia watu aina ya Mafuguri kuanzia ngazi ya shule za msingi mpaka vyuo kuogopa kujitokeza kufanya mambo au vitu vizuri kwa hofu ya kutafasiliwa na washenzi na waliojaa upumbavu juu ya tafsiri njema kuigeuza kufa tafsiri ovyo kama yako.

  Tabia hii iko miaka nenda rudi kwenye baadhi ya Watanzania kuanzia ngazi za shule za msingi,yoyote mpenda kutenda jema au kujituma anageuzwa kujisikia ni mtu tofauti na asiyefaa kwenye jamii kwa maneno ya kinafiki yenye mabezo na vijembe vya kiswahili visivyotaka maendeleo ya kusonga mbele.

  Maneno kama haya KUTAKA SIFA,ANA KIHELEHELE,ANAJIFANYA ANAJUA,MJUAJI,na mengineyo mengi yenye maana nzuri kugeuzwa kuwa maana mbovu na hatimae kujenga tabia ya baadhi ya Watanzania wenye mioyo ya kujituma [Agressiveness] kuogopa kujitokeza kuonyesha uwezo wao kwenye jamii kwa hofu ya kuambiwa maneno machafu kutoka kwa wanajamii waovu na wapenda majungu wasiopenda kuwajibika na wezi wa mali ya umma na jamii kwa vigezo vya kuficha uwezo wao wa maarifa na ubunifu katika utendaji.

  Kwa waliosoma shule za kayumba shule za msingi na sekondari wanalijua hili, ikitokea mwanafunzi akawa ni mchapa kazi na mwenye kujali mambo yake na kuwajibika kwenye masomo utasikia maneno ya ovyo ovyo kama Buku M,Ametumwa na Kijiji,Anapenda Sifa nk.Na wasema hayo wengi wao wanakuwa na upeo mdogo sana dalasani kimasomo,hivyo ili kujifidia [Compasation] wanageuza maneno mazuri kuwa machafu na yenye tafsiri mbaya kwa mwanafunzi mwenzao ili wamvunje moyo aingie kwenye kundi lao walikojificha la upungufu wa akili [Mask cover].

  Kiasi kuwa toka wakiwa wadogo kwenye shule za msingi wanajifunza kuvunja nguvu mioyo ya wale wenye uwezo na nia njema, wanaanza kuwa wasanii na wabunifu wa kupinda sheria na kuwafanya wenye akili zao kuonekana wa ovyo kwenye jamii.

  Na kwa kuwa jambo hili Serikali yetu aina magwiji wa ufahamu wa mienendo wa tabia za binadamu na mazingira [Think tankers] wanaojituma kujua tabia za wanafunzi na kushiriki kusimamia na kuzizuia zisipate nafasi ya kukua na kutapaka kwenye jamii.Serikali inakosa jicho la tatu kutazama tabia za vizazi na muingiliano wa kitamaduni kutoka kwenye makabila yetu unazalisha aina gani ya tabia ambazo si njema kwa Watanzania na hivyo kuhamasisha kuzipiga vita na kuziondoa na kuongeza ushawishi wa tabia zipi zinafaa kuendelezwa kwa faida na manufaa ya Taifa letu.

  Tembelea majiji yetu na miji yetu mikuu ya mikoa na wilaya,wale wate waliokuwa wakiona Mwalimu anaingia dalasani kufundisha wanaluka dilisha na kusepa leo hii wamekuwa ndio wafanyabishara wakubwa na wanasiasa.Mbinu zile zile walizotumia kuwadhihaka wenzao mashuleni na kujisikia inferior leo hii wameztumia kupata mali na madalaka.Siku hizi mataperi na waghiribu wa tabia kwenye jamii wamekuwa watukuzwaji na kuwa ndio wajanja na wanatumia uadilifu wa jamii kuilubuni jamii.

  Tunalia Taifa halina maadili kumbe chanzo ni tabia mbovu ambazo Serikali imekataa kuzisimamia na kuishia kusema usimamizi wa ujenzi wa tabia ni Jukumu la Familia. Matokeo yake kwa kukosa kushape na tabia za watanzania kwa kuzingatia nyakati na mahitaji ya nyakati husika tumekuwa na Taifa la wasema uongo kugeuzwa kuwa ukweli,wavivu na wachonganishi na wanafiki ambao daima wamekuwa ndio wajanja wa kuwapotosha hata viongozi.

  Leo hii Rais Kikwete, anaonekana ameshindwa kutawala hakika wanathread mtu akipewa kiti cha Kikwete masaa matano tu kusoma mafairi na kupitia yaliyomo,hofu yangu ni kuwa atazimia baada ya nusu saa baada ya kuaanza kuyasoma mafaili hayo.Kwani kwa idadi kubwa jamii imekengeuka sana kitabia.

  Tumeunda taifa la wajanja tukasahau kushape watanzania kwa kuziangatia hata makabila yetu,kuna makabila kitendo cha kuiba ni mwiko mkubwa lakini tumezitumiaje tamaduni au tabia hizo za kikabila kuzuia wizi au kusema uongo.

  Magufuli anaweza muacheni tuondoleeni maneno machafu yasiyokuwa na miguu.Uwa natamani kusikia Rais yoyote yule wa Taifa hili akisimama mara kwa mara kukemea tabia za ovyo kama kama uongo na unafiki majungu na misemo ya ovyo kuwahamasisha wananchi kumzomea yoyote yule kwenye jamii ambae itaonekana kuwa ni kero kwenye jamii kwa maneno ya ovyo ovyo kama huyu.
   
 11. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #11
  Sep 2, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ulimakafu usipopigia thank au like DSN kwa tuition aliyokupa itabidi umlipe kabisa hata kwa kubadilika hiyo tabia yako. Mkuu DSN uliyosema nimeyaunganisha kwenye maisha yetu sisi wanafunzi wa Kayumba na kukuelewa vizuri kabisa. Nimegundua kwamba, katika harakati za serikali kuboresha elimu, wasisahau kuweka mkazo kwenye maadili ya wanafunzi na wazazi wao kwani baadhi ya wazazi wanawahukumu watoto kuwa ni wajinga wakita darasa la kwanza badala ya kuwaencourange na kuwamotivate.
   
 12. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #12
  Sep 2, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Magufuri is an example to the rest of the ministers.
  Nadhani wangempa mwakyembe uwaziri kamili alafu Magufuri wampeleke nishati na madini ingawa kwa wakuu wetu wa sasa its a bitter pill to swallow
   
Loading...