Decree Holder
JF-Expert Member
- Jul 19, 2015
- 2,556
- 3,741
Pamoja na Mahakama Kuu ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kuzuia uchaguzi wa serikali ya wanafunzi ya chuo kikuu cha Dodoma (UDOM), serikali ya UDOSO katika kitivo cha sanaa ya lugha na sayansi ya jamii mpaka pale kesi ya msingi iliyofunguliwa na aliyekuwa makamu wa Rais wa college hiyo Rose Maruchu itakapokamilika.
Cha ajabu uongozi wa chuo wakishirikiana na tume ya uchaguzi katika college hiyo wameendelea na uchaguzi leo hii huku wakiwatisha watu kuwa Agizo limetoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli kuwa uchaguzi huo lazima ufanyike na yeyote anayepinga afukuzwe chuo.
Hivi ninavyozungumza wanafunzi wanaogopa hawajui wafanye nini. Wapige kura au wafuate amri ya mahakama!