Prisoner 46664
JF-Expert Member
- Dec 18, 2010
- 1,948
- 1,237
Huko sasa ni kuzidisha na kupitiliza. Meneja/kiongozi unaweza kabisa ukawa firm bila kufokea watu na kuwaadhirisha hadharani. Kufanya hivyo ni kama kutafuta sifa vile. Unataka watu wakusifie...flani mkali bana..flani hana mchezo.
Sijavutiwa kabisa na management na leadership style ya Magufuli.
Lakini jamani,ikiwa kila mtu anayo mapungufu yake,na sisi wote ni binadamu hakuna aliye Mungu kati yetu,...si vema sana kuwa na kiongozi mropokaji lakini anayehakikisha kunakuwa na utekelezaji thabiti wa mipango ya serikali kuliko mtu kama kikwete ambaye ni very diplomatic in public(in fact the best I ever saw)lakini akanyamazia matatizo yetu yote ikiwamo rushwa iliyokithiri??...
sidhani kama sifa ya kwanza ya kiongozi inatakiwa kuwa upole ama huo ukali.sifa ya kwanza ya kiongozi ni uwezo wa utekelezaji wa maazimio ya maendeleo,na uwezo wa kusimamia maslahi ya wengi bila kutetereka...
nikisema hivi,ningewiwa kumuunga mkono maghufuli kama angegombea kupitia ccm ingawa sina mahaba hata chembe na hiki chama..pengine huyu aweza kuwa mtu pekee mwenye guts za kufanya maamuzi magumu na kushughulika na hawa wanyonyaji wetu wa siku nyingi wanaoendelea kuishi kati yetu kama vile wako juu ya sheria.