Magufuli kama wewe ni jasiri, tangaza hali ya hatari, katiba inakuruhusu!

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,063
22,755
Magufuli acha woga wa kujifichaficha nyuma ya vyombo vya usalama, kama wewe ni jasiri tangaza hali ya hatari upate uhalali wa kutawala kiimla.

Kama wewe ni jasiri, achana na udikteta uchwara, watangazie raia wa taifa hili kuwa nchi iko chini ya dikteta hivyo haki zao za msingi zimefutwa.

Achana na amri za kukurupuka na mihemko na hivyo kufanya vyombo vyetu vya usalama kulazimika kuvunja sheria kwa kutii amri batili.

Katiba yetu inakuruhusu, hivyo jipe madaraka kikatiba ufanye unavyotaka na hakuna mwananchi atayekulaumu...
 
Katiba ya nchi iko juu ya Rais na si chini yake hivyo ni lazima ishemiwe na wote hata yeye aliye Ikulu. Vinginevyo hataki kuhwshimu katiba basi atangaze kuifuta, kuvifuta vyama vya upinzani na pia atwambie kwamba awamu hii ataongoza nchi kijeshi.

Acheni kumsifia sifia huyu dikteta uchwara na dharau yake kubwa kwenye katiba ya nchi. Machafuko yakitokea wote tutakuwa roho mkononi bila kujali itikadi zenu. Msimpe kichwa huyu bila kurafakari kwa kina athari kubwa kwa nchi yetu kutokana na huu udikteta wake.

Waliokuja na katiba hawakukurupuka wala kuacha mianya ya aina yoyote ya mtu yoyote yule aidharau katiba hiyo. Viongozi wa namna hii ndiyo huwa cha machafuko katika nchi nyingi za Afrika kwa kujiona wao kama Miungu na kufanya yale ambayo hawana ruhusa ya kuyafanya ndani ya katiba. Tuheshimu katiba ya nchi pamoja na viraka vyake chungu nzima.


Acha kumsakizia Magu. Endeleeni kuleta fujo muone kitakachofuata.
 
FA hatuongelei katiba ile iliyochakachuliwa bali hii ya sasa ambayo inatumika nchini ambayo inavipa RUKHSA vyama vya upinzani kufanya maandamano na mikutano popote pale nchini bila kuingiliwa na yoyote yule. Wanachotakiwa kufanya ni kutoa taarifa tu kwa polisiccm.

Achana na mahaba yaliyopitiliza bila kutafakari kwa kina Tanzania ni yetu sote hakuna mwenye hati miliki. Hebu jiulize kwa nini haya anayoyafanya huyu dikteta uchwara hayakufanywa katika awamu mbili zilizopita!? Ni kipengele kipi ndani ya katiba kinachompa haki dikteta uchwara kuwanyanyasa wapinzani kiasi hiki? Anaogopa nini? Kulikoni!?

BAK, katiba haijiundi; inaundwa. Ukawa mmeigaraza mmekurupukia ukuta then mnasema nini kuhusu katiba? Acha mlizwe ndio mtajua kufocus.
 
Kutoka serikali dhaifu inayokumbatia mafisadi mpaka serikali ya kidikteta inayopambana na ufisadi!

Ama kweli, a week is a long time in politics!

Hizi ni zaidi ya siasa za matukio!

Keyboard solders wa aina yako ni jasiri kweli katika kuandika thread au kutoa comment.

Mwenyekiti wetu ametuambia tutoke kwenye keyboard/keypad tarehe 1 Sept ili tuingie kwenye ground zero inayoitwa UKUTA!
 
FA hatuongelei katiba ile iliyochakachuliwa bali hii ya sasa ambayo inatumika nchini ambayo inavipa RUKHSA vyama vya upinzani kufanya maandamano na mikutano popote pale nchini bila kuingiliwa na yoyote yule. Wanachotakiwa kufanya ni kutoa taarifa tu kwa polisiccm. Achana na mahaba yaliyopitiliza bila kutafakari kwa kinaTanzania ni yetu sote hakuna mwenye hati miliki. Hebu jiulize kwa nini haya anayoyafanya huyu dikteta uchwara hayakufanywa katika awamu mbili zilizopita!? Ni kipengele kipi ndani ya katiba kinachompa haki dikteta uchwara kuwanyanyasa wapinzani kiasi hiki? Anaogopa nini? Kulikoni!?


Rais Magufuli anaiogopa safari ya matumaini iliyoishia njiani ya Urais wa Monduli!

jf-comments6-jpg.375112
 
Acha kumsakizia Magu. Endeleeni kuleta fujo muone kitakachofuata.
Mfikishie ujumbe aache woga...kama ni jasiri afute Katiba, ni hilo tu. Asivipe taabu vyombo vyetu vya usalama.
Kama haki
za msingi zingelikuwa zimefutwa, wewe ungelipata nafasi ya kuandika upuzi wako hapa?
huna tofauti na wale wa Togo waliokuwa wakimsifia Rais wao kwa kuwaletea mvua! Magufuli hana ubavu wa kufungia internet! Kufungia Jamii Forum hakutasaidia kitu, ni kama kuzuia tsunami kwa kiganja cha mkono. Yeye atamke tu kwamba nchi sasa inatawaliwa kijeshi na hakuna mtanzania atamzuia, ila ajue atakuwa anajipalia mkaa wa moto.
 
Magufuli acha woga wa kujifichaficha nyuma ya vyombo vya usalama, kama wewe ni jasiri tangaza hali ya hatari upate uhalali wa kutawala kiimla.

Kama wewe ni jasiri, achana na udikteta uchwara, watangazie raia wa taifa hili kuwa nchi iko chini ya dikteta hivyo haki zao za msingi zimefutwa.

Achana na amri za kukurupuka na mihemko na hivyo kufanya vyombo vyetu vya usalama kulazimika kuvunja sheria kwa kutii amri batili.

Katiba yetu inakuruhusu, hivyo jipe madaraka kikatiba ufanye unavyotaka na hakuna mwananchi atayekulaumu...
Tangu msikie neno dikteta uchwara ndio umekuwa wimbo wako..
Kwan unafikir inashindikana kutangaza??
Watu wengne akili zenu ajabu kweli au rais unamfananisha na balozi wako wa nyumba kumi???
 
Mfikishie ujumbe aache woga...kama ni mwanamme afute Katiba, ni hilo tu. Asivipe taabu vyombo vyetu vya usalama.

Mjinga waahedi, huna tofauti na wale wa Togo waliokuwa wakimsifia Rais wao kwa kuwaletea mvua! Magufuli hana ubavu wa kufungia internet! Kufungia Jamii Forum hakutasaidia kitu, ni kama kuzuia tsunami kwa kiganja cha mkono. Yeye atamke tu kwamba nchi sasa inatawaliwa kijeshi na hakuna mtanzania atamzuia, ila ajue atakuwa anajipalia mkaa wa moto.

Wewe unaonekana hata haki za msingi huzijui. Nyie ndiyo wale mnaojua haki za msingi ni kula tu, na kwenda chooni kujisaidia.

Wewe ulichokifanya hapa ni kutoa maoni, kutoa maoni hiyo ni haki ya msingi halafu ulivyo unaenda mbali eti Magufuli hawezi kufungia internet kwa sababu haisaidii kitu...wewe unaonekana hujui hata matumizi ya internet. Hivi zile nchi zinazozuia matumizi ya internet kwa raia wake, utasema hawa raia wamepewa haki ya msingi?
 
Kutoka serikali dhaifu inayokumbatia mafisadi mpaka serikali ya kidikteta inayopambana na ufisadi!

Ama kweli, a week is a long time in politics!

Hizi ni zaidi ya siasa za matukio!

Keyboard solders wa aina yako ni jasiri kweli katika kuandika thread au kutoa comment.

Mwenyekiti wetu ametuambia tutoke kwenye keyboard/keypad tarehe 1 Sept ili tuingie kwenye ground zero inayoitwa UKUTA!
Kule zimbabwe watu wa namna hii hata rais Mugabe hahangaiki nao ni wananchi tu wanawatawanya wenyewe kwa viboko, kuna haja ya wananchi wenye mapenzi mema na nchi hii kuingilia kati ujinga huu
 
In case you are Mrs Mug Full
Just tell him this; This Is Not Rwanda!! Full stop
Na huyo Kagame wewe na wenzako mlikesha humu kumsifia, leo amekuja wa aina hiyo mmegeuka..only in Tanzania! Ukuta wa tofali za tope ukiambatana na mafuriko, ama ukuta wa mnara wa babeli?
 
Back
Top Bottom