Ndugu wanajamvi.
Ninapenda kueleza kuwa nia ya serikali ya kuwa nchi ya viwanda vya kati inwezekana kabisa hasa akianzia na kuweka mkazo wa kuzalisha sukari nchini. Tukizalisha sukari Nchini tutapunguza kupeleka pesa za kigeni nje lakini pia Tutakuja afya na uchumi wa Ndani.
Wakati wa Big Results Now, wataalamu wetu walifanya upembuzi yakinifu kujua maeneo yanayofaa kwa kilimo cha miwa kwa ajili ya sukari. Ilibainika kuwa Tanzania ina ameneo 17 yenye Hekta500,900 zinazofaa kwa kilimo cha miwa na sukari (Angalia kiambatanisho).Hivyo tukiweza kunadi hayo Maeneo na watu wakaanza kuzalisha Sukari mbona nchi hii itafurahia uchumi kukua.
Ili kuhakikisha viwanda vya sukari vinashamiri na wakulima wadogo hawanyanyaswi basi nashauri yafuato:
1.Viwanda lazima viwe na uwezo mkubwa wa kula miwa kuliko wanacholima. Hii itasaidia kiwanda kutaka miwa ya wakulima wadogo
2. Serikali lazima iweke mkakati uliowazi wakuhakikisha viwanda hivi vinaanza. Watu wnaokwamisha sana kuanzisha viwanda ni NEMC. Hawa wanachukua hadi miaka 7 kutoa kibali (Wakiritimba kupita kiasi)
3. Serikali iweke miundo mbinu ya mmsinga kama Barabara na Umeme kuelekea maeneo ya uwekezaji.
4.Wakulima watakao chukuliwa ardhi yao basi wapewe hisa katika kiwanda.Mfano mzuri angalia concept ya inclusiveness ya ECoenergy Bagayomo. Hii itasaidia mkulima husika kuendelea kupata kipado milele.
5.Weka kodi ndogo kwa bidhaa hii inayozalishwa ndani na weka kodo kubwa kwa sukari kutoka nje.
Bahati mbaya sana, hii dhana ya kufanya Tanzania kuwa nchi ya kuzalisha sukari nchini, inapigwa na itaendelea kupigwa vita kwa njia moja au nyingine na watu wafuatao.
1.Watendaji wengi ndani ya serikali hasa wale wanaopata migao kutoka makampuni yanayoagiza sukari nje bila kulipa kodi. Hawa utawajua kwa kukwamisha jitihada za kuwekeza badala ya kuonyesha njia sahihi ni ipi ili nini kifanyike. NEMC wanaongoza wakisaidiana na PPP unit
2.NGOs za kitanzania au kimataifa zinazofadhiliwa na nchi ambazo soko lao la Sukari ni Tanzania. Hawa ni kama Haki ardhi. wao wanaanza kusema eti kulima muwa kutafanya watanzania waaje kuzliasha chakula, lakini hawaoni athari za kuagiza sukari nje
Magufuri uliza watu wa wizara ya kilimo, SAGCOT centre and Presidential Delivery Beureau. Ni kwanini ayo maeneo yaliyoanishwa wakati wa kipindi cha Big Results Now mbona hakuna kianchoendelea wakati wao wanakula mishahara minono. Majibu yao yatakusaidia ujue pakuanzia. Wape deadline kuhakikisha maeneo mazuri kwa kuzalisha sukari yanaanza kuwekezwa kwani wawekezaji wapo ila ukiritimba ndani ya Serikali umekuwa ni wimbo unaofurahisha badala ya kukerekesha.
Mh Rais, naamini ukipitia haya na ukayafanyia kazi, utajua kwanini Tanzania tuko hivi tulivyo.
Asante..