"Magufuli kama Kweli ipo hivi ulivyoamua si Sawa hata Kidogo"

Ndikwega

R I P
Feb 1, 2012
5,979
5,527
Kuna mdau katoka kunipasha kuwa eti Mh.Rais amesema hataki kushauri kwa kipindi kama cha miaka mitatu hivi ili ajionee wapi atashindwa, baada ya hapo ndipo ataanza kuufanyia kazi ushauri atakaopewa.
Hofu yangu ni kuwa itakuwaje nchi iendeshwe na Mawazo ya mtu mmoja(Rais)?
Inamaana ndani ya muda huo asiyotaka kushauriwa hata tukiwa tunaangamia ili mradi yeye hajakubaliana na Mawazo yetu na tufe tu?
Kama ndivyo, Je, Rais kajiona yeye anauwezo kimawzo kuliko Raia yeyote hapa nchini?

Tafadhali Mh.Rais kama ndicho ulichoazimia badilisha hayo Mawazo, Yoote yatakushinda kabla ya saa 6 na Unabii utakuwa umetimia.
 
Katika lile kundi la wagombea wa CCM huyu hakuwa mgombea bora hata katika 7 bora hakuwemo, lakini Mkapa na Kikwete badala ya kuweka maslahi ya nchi mbele, wakaweka maslahi yao mbele. Ni nani katika hawa anaweza kuendelea kuwalinda kama Marais wastaafu kutokana na madhambi yao chungu nzima waliyoyafanya walipokuwa madarakani. Hawakuona mwingine yeyote zaidi ya Magufuli sasa nchi inayumba kwa kasi ya kutisha.
 
We nani mpaka uiamlie ccm mgombea wake, ?? Au na wewe ni kapi la ccm B.
Maana unajifanya kuyajua ya ccm kuliko ya ufipa!!!
 
Ushauri wote uko kwenye ilani ...wewe unataka kushauri nini zaidi ya umbeya?
 
Nani amekwambia mimi naiamulia CCM? Mimi nazungumza kama Mtanzania ambaye ana haki ya kufanya hivyo wakati wowote ule na mahali popote pale. Hakuna aliye na hati miliki ya Tanzania hivyo wote tuna haki ya kukosoa kile ambacho hatukubaliani nacho na kusifia kile ambacho tunaona ni kizuri kwa maslahi ya nchi. Acha kukurupuka mpumbavu wewe.

We nani mpaka uiamlie ccm mgombea wake, ?? Au na wewe ni kapi la ccm B.
Maana unajifanya kuyajua ya ccm kuliko ya ufipa!!!
 
Nani amekwambia mimi naiamulia CCM? Mimi nazungumza kama Mtanzania ambaye ana haki ya kufanya hivyo wakati wowote ule na mahali popote pale. Hakuna aliye na hati miliki ya Tanzania hivyo wote tuna haki ya kukosoa kile ambacho hatukubaliani nacho na kusifia kile ambacho tunaona ni kizuri kwa maslahi ya nchi. Acha kukurupuka ******** wewe.
Mara nyingi hawa Watawala wanaona nchi hii ni sehemu ya familia zao.
 
Hilo ni kosa kubwa sana Mkuu. Nimesoma mahali humu eti Magufuli hataki ushauri kutoka kwa yeyote yule mpaka amalize miaka mitatu. Ndani ya hii miezi minane tu nchi inayumba hivi uchumi unaanguka kwa kasi ya kutisha, vitisho vya polisi kwa wapinzani kila kona nchini sasa kama hii ni ukweli kwa miaka mingine mitatu nchi hii si itakuwa imeanguka vibaya sana kiuchumi na kisiasa hata ushauri utakaotolewa wakati huo utakuwa ni useless? Kujenga nchi ni kazi kubwa sana lakini kuibomoa ni kazi rahisi mnooo.

Mara nyingi hawa Watawala wanaona nchi hii ni sehemu ya familia zao.
 
Si ajabu kwangu, tangu azuie shughli za siasa ambazo zipo kwa mujibu wa sheria, anaweza akafanya lilote hata zaidi ya hilo.
Marehemu, Rupondija, Mabina na Nsena wangekuwa hai wangewaambia tabia ya huyu mtu. nini naogopa kusema nije kutolewa kucha na kutobolewa macho. Hawa niliowataja walikuwa wakubwa wake wa kazi pale NCU miaka ya 80 na 90. Jinsi alivyokuwa haambiliki. Wakati huo yeye akiwa Mkemia wa mbegu za pamba.
 
Duniani kote hamna democrasia ya kutukana wenzio.

Chadema wanamwaga matusi hadi wanaonyesha kidole cha kati bungeni kwa kisingizio cha democrasia. .

Huo ushauri mnaotaka kumpa Magufuli, si muende mkampe mwenyekiti wa chadema aliyebadili gia angani na kuuza chama
 
Alafu akija kufeli ndio aje akiri alikosea kama alivyofanya Mkapa huku Taifa limeshaingia hasara.Bila kuondoa kipengele cha Katiba kinachotoa kinga ya Raisi kutoshitakiwa,mambo ya aina hii kamwe hayataisha.
 
Kuna mdau katoka kunipasha kuwa eti Mh.Rais amesema hataki kushauri kwa kipindi kama cha miaka mitatu hivi ili ajionee wapi atashindwa, baada ya hapo ndipo ataanza kuufanyia kazi ushauri atakaopewa.
Hofu yangu ni kuwa itakuwaje nchi iendeshwe na Mawazo ya mtu mmoja(Rais)?
Inamaana ndani ya muda huo asiyotaka kushauriwa hata tukiwa tunaangamia ili mradi yeye hajakubaliana na Mawazo yetu na tufe tu?
Kama ndivyo, Je, Rais kajiona yeye anauwezo kimawzo kuliko Raia yeyote hapa nchini?

Tafadhali Mh.Rais kama ndicho ulichoazimia badilisha hayo Mawazo, Yoote yatakushinda kabla ya saa 6 na Unabii utakuwa umetimia.
Ni uchochezi, usihoji mambo/matamshi ya Ikulu
 
Back
Top Bottom