Magufuli, Jiuzulu kwa hiari yako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magufuli, Jiuzulu kwa hiari yako

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Haki, Jan 5, 2012.

 1. H

  Haki JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2012
  Joined: Jan 14, 2009
  Messages: 356
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maisha yanazidi kuwa magumu. Gharama za maisha zinapanda kila siku. Maghufuli kaamua kuongezea gharama za maisha kwa WTZ. Serikali inatakiwa ikate matumizi ili kuwa na kuwa na balance budget nzuri kwa nchi.

  Leo ktk TZ tunaona vinyume kabisa. Serikali inaonngeza matumizi yao, posho zao. Matokeo yake, Wananchi ndiyo wanatakiwa walipe hizo gharama za matumizi ya kijinga ya serikali. Tunapandishiwa Kodi, Nauli, ili maisha ya Vigogo yaendelee.

  Hii siyo society nzuri. Tunaomba Waziri Maghufli awajibike kwa kujiuzulu kwa sababu ya kuendeleza mpango huu wa serikali bila ya manufaa ya Wananchi.

  Kwanini WTZ walipishwe gharama kubwa za nauli kufidia matumizi ya kijinga(posho) ya Serikali? Kwa nini tuwalipie ili tubalance budget ya serikali? Kwa nini WTZ? Kwa nini tusikate matumizi?

  Nakubali kwamba Maghufuli unatekeleza mpango huu ili uwafurahishe Vigogo wa nchi,ndiyo maana hata Dewji kaamua hadharani kukusuport. Tunakuoma Ujiuzulu; hii ni Kashfa kwa nchi yetu.
   
 2. M

  Mbilikendaa New Member

  #2
  Jan 5, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hoja ya kumtaka Magufuli haina mshiko kitaifa kwanza binafsi nampongeza kwa kupandisha gharama ya Kivuko, yapo Mambo mengi ambayo yanawagusa watz na yanaongeza ugumu wa maisha si 100 kupanda kwa gharama za umeme na matatizo kibao yanayolikabili taifa letu nilitegemea wananchi wangepinga Hilo na ongezeko la shilingi 100 ambayo imedumu kwa ZAIDI ya miaka kumi na moja gharama za uendeshaji ni kubwa acha aongeze na kikubwa ni kuweka udhibiti mzuri wa kinachokusanywa. Magufuli chapa kazi
   
 3. H

  Haki JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2012
  Joined: Jan 14, 2009
  Messages: 356
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Hela zikusanywe ili ziende kulipa Posho za Wabunge na vigogo vya serikali au siyo!!

  Tuamkeni jamani. WTZ wake UP.
   
 4. L

  LAT JF-Expert Member

  #4
  Jan 5, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mtoa mada, hata jina la waziri wa ujenzi haujui linaandikwaje

  very low

  shame !
   
 5. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #5
  Jan 5, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  I would wish nauli ya KIVUKO ingepandishwa na kufikia 500/-

  Hivi ni Kigamboni pekee yenye wananchi wa kipato cha chini?

  Vipi Bunju, Kimara, Gongo la Mboto, Kitunda, e.t.c? Wao wanalipa kiasi gani kufika CBD?
   
 6. H

  Haki JF-Expert Member

  #6
  Jan 5, 2012
  Joined: Jan 14, 2009
  Messages: 356
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Angalia point inayoiweka. Usijaribu kuangalia mji gani unalipa bei gani. Focus na point ninayoiweka.
   
 7. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #7
  Jan 5, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Utamaduni wa kujiuzuru Tanzania haupo!! hata ukishikwa umehamishia hazina yote chini ya uvungu, wala toa kidogo tulia. Au ibua lingine zito zaidi kuwahamisha watu akili wanasahau haraka.
   
 8. Tz-guy

  Tz-guy JF-Expert Member

  #8
  Jan 5, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 439
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ajiuzulu kwa ajili ya kupandisha Sh. 100? Hapo si sawa, ila kutokana na kauli yake inabidi aombe msamaha kwa wananchi maana yeye si malaika mpaka asijikwae. Halafu kuhusiana na matumizi ya serikali msiangalie tu posho za wabunge (Japo nami silikubali), pia kuna mambo mengi sana kama vile: ongezeko la wanafunzi vyuoni ambao wanahitaji mikopo, kuwepo kwa shule za kata ambapo inabidi wapewe ruzuku, mwezi huu walimu wanaanza kulipwa madai yao ya muda mrefu, kuna baadhi ya miradi ya barabara serikali imeingia gharama baada ya wafadhili kujitoa, n.k. Sometimes tuwe na huruma kwa serikali yetu, sio kila wakati kuiponda.
   
 9. Prisoner 46664

  Prisoner 46664 JF-Expert Member

  #9
  Jan 5, 2012
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 1,955
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  Mkuu naona tunasahau kuwa mjenga nchi ni mwananchi mwenyewe.hakuna pa kutoa pesa za kuendesha shughuli za serikali zaidi ya kwa wananchi wenyewe..suala la maisha magumu muulizeni JK.Kwanini hatutumii ipasavyo rasilimali zetu nyingi tulizonazo kuongeza uzalishaji na hatimaye tuweze kuuza nje vya kutosha na kupunguza ugumu wetu wa maisha!??hii ardhi tuliyonayo ingepewa serikali ya dubai Tanzania ingekuwa taifa tajiri kuliko yote afrika mara..kwanini hatujifunzi??
   
 10. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #10
  Jan 5, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Sishangilii kuongezwa kwa nauli lakini pia siungi mkono hoja kwamba Maghufuli kujiuzulu eti kwa sababu kaongeza bei za kivuko. Bei ngapi zimeongezeka na hakuna waziri aliyeambiwa ajiuzulu. Bei za mafuta zinaonmgezeka kila siku hakuna waziri aliyeambiwa ajiuzulu, bei za vyakula na sukari zinaongezeka kila siku lakini hatujasema waziri ajiuzulu. Hivi kati ya kupanda kwa bei ya vyakula/sukari na kupanda kwa bei ya kivuko ni bei ipi inawaumiza wa Watanzania?

  Naanza kuona muandamo wa Maghufuli wenye vimelea vya kisiasa!!
   
 11. Thomas Odera

  Thomas Odera Verified User

  #11
  Jan 5, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 644
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hivi Magufuli ajiuzulu kwa ongezeko la mia na je Ngeleja na Omar wajiuzulu watakapopandisha gharama ya umeme na nauli ya treni? Je na spika naye na wabunge wake kwa kupandisha posho wajiuzulu ? Magufuli komaa wala usiombe radhi
   
 12. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #12
  Jan 5, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Unapoteza muda bure wa kulalamika maghufuli ajiuzuru wakati mkuu wa nchi anafurahia kupanda kwa nauli ili apate pesa za kufanyia matanuzi. Mbona Pinda hajasema chochote. Mbona mkuu wa nchi amekaa kimya. Mwacheni maghufuri yeye ametumwa kutekeleza.
   
 13. i

  ikindo Member

  #13
  Jan 5, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 87
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 25
  du! hivi ni kweli jamaa alisema shilingi mia tu mnalalamika wakati hainunui hata kondom ama masikio yangu yamesikia vibaya.

  halafu watu mnaangalia tu shilingi mia mbona hamuongelea kupanda kwa nauli za Maguta, mikokoteni na magari ambayo kwa kiasi kikubwa ndo yatakayoleta maisha magumu kwa sababu kila bidhaa inayoingizwa kigamboni kutoka kariakoo inabebwa na vyombo hivyo.
   
 14. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #14
  Jan 5, 2012
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  message sent.
   
 15. sblandes

  sblandes JF-Expert Member

  #15
  Jan 5, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,468
  Likes Received: 790
  Trophy Points: 280
  Kivuko kina gharama za uendeshaji n.k nani abebe mzigo wa kukigharamia kama si mtumiaji ?
   
 16. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #16
  Jan 5, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,797
  Likes Received: 1,339
  Trophy Points: 280

  Uko Sahihi Chief, Habari za Singapore.
   
 17. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #17
  Jan 5, 2012
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Kama nchi kma Kenya ambayo haina madini na raslimali kama Tanzania inaweza kuweka vivuko vya bure huko Mombasa na kwingineko ni kwanini Dr Magufuli apandishe bei ya hata hicho kidogo kinacholipwa na watanzania ambao nchi yao imejaaliwa madini kibao na raslimali lukuki?
   
 18. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #18
  Jan 5, 2012
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Hii inaonyesha ni jinsi gani haufahamua hata jiografia ya jiji hili achi mbali ya nchi yako. Nani kakuambi kuwa wakazi wote wa Kigamboni hutumia usafiri wa kivuko kufika makwao? webgi baada ya kuvuko kwa pantoni hutumia mabasi ya daladala, pikipiki na teksi kufika katika vitongji vyo mbali mbali.

  Je hao wakazi wa maeneo uliyoyataja hulip kiasi gani kuvua madaraja yaliyojengwa katika abarabara za huko? Kama hawalipi kitu chochote basi na wakazi wa Kigamboni hawastahili kulipa chochote katika vivuko kama ilivyo Kenya. nchi amabyo haiana madini na raslimali kama Tanzania.
   
 19. d

  davidie JF-Expert Member

  #19
  Jan 5, 2012
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 329
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi hawa wabunge wanaopinga ongezeko la nauli ya kivuko kwa kudai eti wana huruma na wapiga kura wao mbona wanapokea ongezeko la posho pasipo kuwa na huruma kwa wananchi wao na pesa hizo wanazopokea ndio zingeweza kufanya shughuli nyingine za maendeleo. Wanatakiwa watoe boriti machoni mwao kabla ya kutoa kibanzi machoni kwa wengine
   
 20. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #20
  Jan 5, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135

  Hana sababu yoyote ya maana ya kujiuzulu. wa kujiuzulu wenye serikali yatu huwaoni? Nadhani kwa mawazo yako ulipoanzisha thread hii, ungefurahi zaidi KUSIKIA WALE WALIOACHA WATU WAKAJENGA MABONDENI WAMEPANDISHWA VYEO. MBONA hujasema wale wanaoacha bei za mafuta kupanda kila siku, na wanaoshindwa kudihibiti uchumi wa nchi wajiuzuru?

  Amefanya kazi yake inavyotakiwa. hana sababu yoyote ya kujiuzulu.
   
Loading...