herzegovina
JF-Expert Member
- Oct 28, 2015
- 3,129
- 4,712
Naweza kusema pamoja na rais Magufuli kuonekana sio mwanasiasa mzuri lakini karata zake amezichanga vizuri sana.
Tangu aingie madarakani alionekana dhahiri kuwa ni rais asiye na simile kwa upinzani. Amekuwa akiwashughulikia kweli kweli.
Muda wote nguvu kubwa imekuwa ikitumika "kuwazima" hawa wapinzani sema tu ugumu ulikuwa sehemu moja tu....MIOYO YA WANANCHI.
Wananchi wengi wanaamini wapinzani ni watetezi wao na ndio maana huwa wapo tayari hata kufa kwa ajili ya kuwalinda wapinzani.
UCHAGUZI wa 2020 ukafanyika na nguvu kubwa ikiambatana na wizi, ghiliba na dhulma ikatumika ili kumrudisha JPM pamoja na CCM yake madarakani huku asilimia kubwa ya wananchi ikibaki na majonzi makuu kutokana na kuporwa haki yao ya kuchagua na kuongozwa na watu wanaowataka.
"Mabeberu" nao hawakuwa nyuma...wakaanza kupiga spana. Ikabidi sasa iwe isiwe lazima wapinzani warudi. Amini usiamini, "Nguvu kubwa" pia imetumika kuwarudisha hao wapinzani. Ukimuangalia Mdee anavyoapa unaona kabisa kuwa "huyu sio Mdee". Speech aliyoitoa inaonekana kabisa ni "script" iliyoandikwa. Pia inasemekana kuwa wote walioapa wana ulinzi wa watu fulani. Kiuhalisia wale sio walinzi bali ni waangalizi wao. Hapa ndipo "UJINIAZ" unapokuja.
Ushindi wa JPM ni upi? Baada ya hiki kutokea ambacho kitafuatiwa na ACT kule zenji, wananchi watastaafu siasa. Hawatataka tena kufuatilia mambo ya siasa. Wataona wanasiasa wote wapo kwa ajili ya matumbo yao tu. Hawatajali tena ni nani anawaongoza. Sasa hapa ndipo kale kahoja ka KUONGEZA MUHULA katakapokuja na wananchi hawatojali tena.
Kumi tena.