Magufuli hii si haki!

Kimla

JF-Expert Member
Jun 8, 2008
3,741
6,430
Mh Rais kwanza hongera kwa kazi nzuri sana. Mie ninaona unachofanya licha ya kuwa na nia nzuri lakini wengine umteukwaza hasa wanaCCM na wafanya biashara.Wewe unaangalia watu masikini tu, nitatoa mfano juu ya hili.

1. Mh Wakati Sukari imeadimika sisi Wana CCM na wafanya biashara tulizoea kupata msamaha wa kuleta sukari bila ushuru na tulipiga pesa kweli lakini mwakajana ukakataa hilo na badala yake unahamasisha makampuni yazalishe sukari nchini. Kufanya hivyo kukatukosesha watendaji wa serikalini na wafanyabiahsara mavuno bila Jasho. Hii sirikubali
2.Umezuia safari yningi za nje zilizokuwa zinatupa pesa na badala yake kwa savings hizo ukaleta ndege 2..Hii ni jambo zuri kwa wengi lakini kwa sisi wanaccm na wafanyabishara pamoja na wafanyakazi umafanya hali na status zetu kwenye jamii zishuke. Hii silikubali
3.Kipindi hiki amacho mahindi yamepungua tulitarajia uturuhusu tuingize mahindi na machele wa Tailandi ili tupige pesa ya kufa lakini wewe unataka tulipe kodi ili wale walio na mzigo nchini bei zao zisipungue.Sasa sisi percent zetu tulizozoea kuzipata wakati kama huu tutazipata je. Huu ndo wakati wa sisi kunufaika lakini hukati hilo.Hapa kama wafanyabiashara ndani ya CCM na Vyama vingine umetukwaza
4.Umezuia mikutano kwenye mahotel-Wakati hapa ndo orgnizers tulipata riziki ..mfano ukiaandaa semina ya sh million 4 kwa siku basi tuanongeza anagalia million 4 zingine za ziada ..hizi ziada zilirudi kwa wananchi kupitia ujenzi, sherehe zakifanilia nk..sasa umekata kabisa.
5.Umedhibiti bodi ya Korosho na mfumo wa bei zake kiasi kwamba wakulima wakapat mamillion mengi kwenye mauzo mpaka wanatuona wafanyakazi kama viazi fulani. Lakini zamani sisi wafanyakazi kuanzia wizarani haki bodi na vyama tulikuwa tunapercent yetu..Sasa mwaka huu zote wamechukua wakulima.Hii Si haki.
6.Kuna mengi tu unatukwanza sana --sisi tulijua utakuwaunaongea ila unatekeleza kinyume ili tuendelee kunufaika lakini wewe umekomalia wote tuwe sawa...Tuachie kidogo tugawane gawane hata kidogo ,overall hawa wananchi wakawaida waliisha
 
Keleleeee, na bado, hama nchi kama unaona Mh. Rais humtaki..!! Alafu si Magufuri, ni Magufuli

Mh. Rais anafanya vema kwa kiasi kikubwa kabisa.. full stop
 
Back
Top Bottom