Elections 2015 Magufuli: Hatujaahidi kwenda mwezini, ahadi zetu zinatekelezeka

the horse

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
652
441
Akiwa amekwishatembea mikoa 13, wilaya zake zote na majimbo yote akizungumza na watanzania kwanini wamchague yeye Dkt. Magufuli amekuwa akionekana mtu anayemaanisha kile anachokizungumza ameaahidi yafuatayo mpaka sasa:-

• Ninao uwezo, ujasiri na maarifa ya kubadilisha mfumo wa uongozi na utendaji ili uwatumikie zaidi wananchi na uwezeshe uwajibikaji wa viongozi ambao si waadilifu. Maagizo haya yapo kwenye ilani yetu ya 2015-2020 na nimejiandaa kuyasimamia kwa dhati kabisa. Najua wapo watu wanasema Magufuli mzuri ila mfumo ni mbaya naomba niwahakikishie ndugu zangu mfumo wowote duniani huwekwa na mtu/watu na mtu/watu wanaweza kuubadilisha. Hivyo msiwe na hofu mimi ndiyo MAGUFULI mnanitambua kwa uadilifu na uchapakazi sitabadilika!

• Nitajenga utamaduni mpya wa viongozi kuwajibika kwa matokeo ya kazi tunazowapa. Nawahakikishia sitachelewa wala kusita kuwaweka pembeni viongozi na watendaji watakaokuwa wanatuchelewesha katika kutimiza ahadi zetu kwa wananchi. Nitahakikisha tunakuwa na mpango kazi madhubuti wa kutekeleza ahadi zetu na tutakuwa tunawajulisha wananchi kila hatua ya utekelezaji.

• Natambua ajira ni tatizo la kidunia lakini serikali yangu lazima ikabiliane nalo tena kwa ufasaha sana. Awamu yangu itakuwa ya viwanda. Ambapo serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi Tutajenga viwanda kwa usindikaji wa samaki mwambao wa bahari ya Hindi,Ziwa Victoria na Tanganyika; Tutajenga viwanda vya saruji; nyuzi,nguo na magunia; Nyama na bidhaa za ngozi; pembejeo za kilimo; kufufua viwanda vilivyokufa au kudorora na kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji wa ndani na nje kuwekeza katika ujenzi wa viwanda. Kuna umuhimu pia wakutazama sheria, taratibu na kanuni zetu za ajira serikalini nitalifanya hili.

• Tumekuwa tukipambana sana kuona tunajitegemea kibajeti mfano mwaka 2005 bajeti yetu ilikuwa inategemea misaada kwa 34% na leo bajeti yetu 2015/2016 inategemea misaada kwa 8% tu. Awamu yangu tutahakikisha tunajitegemea kamili. Natambua ili tujitegemee lazima tukusanye kodi kwa ufanisi; leo tunakusanya bilioni 900 kwa mwezi toka bilioni 175 kwa mwezi 2005 awamu yangu itakusanya mara tatu zaidi. Tutapunguza misamaha ya kodi na kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ili fedha nyingi zaidi ziende kwenye miradi ya maendeleo. Tutazipitia upya tozo za kodi ili ziwe kwenye kiwango ambacho watu wengi zaidi watalipa kodi na kwa hiari. Ikiwa hivyo na serikali tukaisimamia vyema hakika Taifa hili litapaa kimaendeleo.

• Uhakika zaidi wa mapato ndiyo unaotufanya tuseme watoto wetu watasoma bure kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne bure pamoja na kuimarisha miundombinu ya kitaaluma kama madarasa, madawati, vitabu, vyoo, na nyumba za walim pamoja na kuwalipa vizuri ili wafundishe kwa ari zaidi. Pamoja na kuboresha huduma za afya nchini ili zipatikane kwa haraka, gharama nafuu, karibu zaidi kwa uhakika na kuhakikisha upatikanaji wa madawa na vifaa tiba. Pia tutazingatia umuhimu wa kuwaendeleza watumishi wa kada ya afya na kuboresha maslahi yao na mazingira yao ya kazi.

• Utawala wa Rais Kikwete umejenga vyuo vikuu vikubwa viwili UDOM na Nelson Mandela Arusha. Awamu yangu ilani inaelekeza serikali kujenga viwili pia mbavyo ni Chuo Kikuu Cha Kilimo na Sayansi Shirikishi cha Mwalimu J.K.Nyerere Butiama mkoani Mara na Chuo Kikuu Cha Sayansi za Madini mkoani Shinyanga. Pamoja na kukamilisha ujenzi wa chuo kikuu cha Afyana Sayansi tumizi cha Muhimbili eneo la Mloganzila nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Tutakamilisha kwani elimu ya juu ina umuhimu mkubwa sana katika maendeleo ya taifa letu. Serikali yangu pia itaendelea kuongeza bajeti ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu na kujenga hosteli za kutosha kwa wanafaunzi waliopo katika vyuo vya umma ili wasome kwa utulivu.

• Natambua nchi yetu ya Tanzania ina utajiri mkubwa wa rasilimali. Lakini nchi kuwa tajiri kwa rasilimali sio sifa. Sifa ni kwa wananchi kuwa matajiri kutokana na rasilimali hizo kupitia mazingira mazuri yaliyowekwa na serikali ili jitihada zao za kujiendeleza ziwanufaishe zaidi. Ninawahakikishia nitaangalia upya utaratibu wa uvunaji rasilimali zetu ikibidi kupitia upya sharia zetu ili wananchi wanufaike zaidi. Pia nitahakikisha watanzania wanashiriki katika uvunaji na sio kuwa vibarua bali kama wamiliki na wawekezaji na kuona mikataba inalinufaisha taifa. Kwa kutambua rasilimali asili hizi huisha na bei zake hubadilika kila wakati tutazitumia vizuri kwa maendeleo ya wananchi hususani kujenga rasilimali watu imara katika sekta muhimu kwa ajili ya kukuza uchumi wa taifa letu kama Afya,Sayansi na Teknolojia, Gesi, mafuta, madini na Uchumi pamoja na Masuala ya ulinzi.

• Nimetumika serikalini kwa miaka 20 bila kupewa onyo, kusimamishwa wala kufukuzwa nawahakikishia sitakuwa na mzaha wa uvumilivu na watendaji wazembe ,wabadhirifu na wanaoendekeza urasimu. Nawahakikishia nitajenga utamaduni mpya wa uwajibikaji. Kutakuwa hakuna kubebana wala kujuana. Nitaimarisha mfumo mzima wa utumishi wa umma ili kuiwezesha serikali kuwatumikia vizuri zaidi wananchi.

• Nawaahidi utumishi uliotukuka, uadilifu na uchapakazi. Mtarajie serikali itakayokuwa inafanya maamuzi sahihi, kwa wakati sahihi na utekelezaji sahihi lakini kwa haraka. Mtarajie uongozi wa kidemokrasia lakini uwepo wa nidhamu serikalini na jamii nzima. Nitasimamia utawala wa sharia hakuna mtu atakayekuwa juu ya sharia na hakutakuwa na mzaha wala majadilano katika kufuata na kutii sharia za nchi. Nitapenda kuona serikali inachapa kazi na wananchi wanachapa kazitu basi! Nitalinda umoja, amani na usalama wan chi yetu kwa nguvu zote.

• Nitatumia maarifa yangu, uwezo wangu na vipaji vyangu vyote na kumtanguliza Mungu wakati wote kutetea maslahi ya Tanzania katika dunia ya leo kwa kuyaenzi mema yaliyofanywa na watangulizi wangu. Nitahakikisha seikali yangu wakati wote inasimamia uadilifu ili kuendelea kuijengea heshima nchi yetu kimataifa. Nitaimarisha uhusiano na nchi zingine lakini nitatumia muda wangu mwingi ndani ya nchi ili kuharakisha maendeleo ya watanzania.

MAGUFULI: MCHAPAKAZI, MUADILIFU NA MFUATILIAJI
HapaKaziTu!!!!!
 
Kutokana na ukosefu wa elimu kilimo chetu kimekosa tija kwa maana ya kupata mavuno kidogo kwa ekari (quantity),kupata mavuno yasiyoendana na mahitaji ya soko kwa maana ya ubora (Quality) na hivyo kufanya mazao yetu kuuzwa kwa bei ya juu kuliko imported,Wasomi wetu wamekuwa wanatoka shuleni na vyuoni wakiwa na vyeti badala ya maarifa na ujuzi.hapo kwenye bold mtafanyaje?Huoni hiyo ni porojo?
 
Hatuhitaji Uongozi wa serikali ile ile, Magufuli kaa pembeni ili uone uongozi Wa Lowassa na Serikali ya UKAWA iwaineshe namna ya kuongoza, wananchi wanataabika, hospitali hakuna dawa, wanafunzi wanakaa chini, barabara mbovu ni dalili tosha kuwa hamna fikra mpya na pembuzi, ccm haiwezi kuleta mabadiliko, acheni porojo,.

Hujui Rais wa Libya alikuwa nani halafu porojo kibaoooo, hatutaki usanii wa serikali ile ile ya ccm,
#MabadilikoNiLazima2105
 
Sioni upinzani hapa zaidi ya porojo tu za ukawa.
Ni kazi kwenda mbele kama wee mvivu na mtu wa kulalamika tuu kaa pembeni, PISHA TINGATINGA.
 
Sisi tumeshaanza kujifunza kutamka Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Edward Lowassa
 
Kutokana na ukosefu wa elimu kilimo chetu kimekosa tija kwa maana ya kupata mavuno kidogo kwa ekari (quantity),kupata mavuno yasiyoendana na mahitaji ya soko kwa maana ya ubora (Quality) na hivyo kufanya mazao yetu kuuzwa kwa bei ya juu kuliko imported,Wasomi wetu wamekuwa wanatoka shuleni na vyuoni wakiwa na vyeti badala ya maarifa na ujuzi.hapo kwenye bold mtafanyaje?Huoni hiyo ni porojo?
Swali lako lina sehemu kuu tatu..\
1. Kuhusu Bei ya juu ya Bidhaa za ndani zinazotokana na Kilimo, sababu za kufanya bei kuwa juu ni tatu, gharama ya uzalishaji (pembejeo, viwandani) usafiri (miundombinu) na tatu ni Kodi..Serikali ya Magufuli imeahidi kuendelea kuimarisha miundombinu na ni ukweli ulio bayana kuwa barabara zetu leo ni bora kuliko miaka kumi nyuma, bado sehemu chache ambazo Dr ameahidi kuzishughulikia. Na vivyo hivyo UMEME, viwanda vimekuwa vikitumia gharama kubwa katika uzalishaji kutokana na gharama za nishati ambayo tayari imetangazwa kushuka hivi punde kutokana na gesi na kuhusu kodi, Dr magufuli alishasema kuwa atafuta kodi zote na tozo za kero ambazo hazina msingi kwa wananchi wa hali ya chini na atashughulika na matajiri wakubwa na wafanyabiashara wanaokwepa kodi.

2. Wasomi kutoka shuleni kuna sababu KUU MOJA, maslahi, kama wataboreshewa maslahi yao watabaki mashuleni na jambo hilo Dr Magufuli ameshalisema mara kadhaa kwenye kampeni zake, kuwa atakuwa rafiki wa walimu na wasomi wa ndani katika kuboresha mazingira yao ya kazi.

3. Kuhusu ajira suluhu yake VIWANDA, ambavyo DR Magufuli amesema kuwa TANZANIA yake itakuwa TANZANIA ya VIWANDA.
 
Mbona ameshindwa kuwa na maarifa ya slogan yake, na wakat alipata taarifa kuwa upo uwezekano wa kuteuliwa kupeperusha bendera ya ccm toka mwaka Jana mwezi wa 8
 
12003420_911949362175502_3902610971291937486_n.jpg

Wewe ndio chaguo letu tunaimani na wewe haujawahi kutuangusha na sasa tunahakika utalifikisha taifa lako mahala ambapo watanzania tunataka
kura yangu ni kwa magufuli
12033061_511061212381657_782874547506958936_n.jpg
 
Ujio wako MAGUFULI umetokea wakati watanzania wengi tunataka maendeleo sasa tunaomba usituangushe, kura zetu zote umepata na nakuhakikishia oct 25 utatangazwa kua rais mpya wa awamu ya tano TANZANIA

20150919014336.jpg

12002902_984358588273752_8938539151233777885_n.jpg
 
Kazi tu wakati ajira hamna?

sijui wewe ni kijana ma mzee ila cha msingi ninachotaka kukusihi achana na mkumbo fanya kazi tatizo la ajira halipo tanzania tu ni duniani kote isitoshe nchi yetu inawasomi wengi sana kwa kipindi hiki, na lingine tambua tanzania ni nchi ambayo nusu yake ya eneo ni kama nchi zote za afrika mashariki kwahiyo usitake kila kitu serikali ikufanyie kwa wakati ambao wewe unataka na kama una elimu nzuri tafutakazi hata kwenye makampuni binafsi IQ nzuri inajiuza tu
ni hayo tu ila magufuli atayatatua yote haya tumpe nafasi tuone yapi atatutendea
 
Back
Top Bottom