Magufuli; Hapa ndio tulipofika

bnhai

JF-Expert Member
Jul 12, 2009
2,824
2,381
Tunashukuru Rais wetu maana hoja sasa;

1.Nani ameomba kibali kwenda nje
2. Nani amefanya ziara ya kushtukiza
3. Nani amefunga geti la Wizara.
4. Nani amefukuzwa kazi.

ASANTE SAANA MHESHIMIWA KWA UTEKELEZAJI WA ILANI
 
Ilani ni ya Magufuli si ya ccm!
Inawezekana maana hatuelewii tunakoenda, kwahiyo hatujui tutashukia wapi. Siku dereva akisimamisha gari, telemkeni ndio hapa, hakuna swali maana hatujui tunapoelekea.
 
Hata maigizo ya baadhi ya wengine nayo yatasaidi kutuamsha, tulilala sana usingizi.
 
Inawezekana maana hatuelewii tunakoenda, kwahiyo hatujui tutashukia wapi. Siku dereva akisimamisha gari, telemkeni ndio hapa, hakuna swali maana hatujui tunapoelekea.
Muwe wavumilivu tu. Magufuli atatufikisha tu.
 
Haya ndio matokeo ya kuwa na kile kinachoitwa MABADILIKO YA KWELI. Haya ni mabadiliko yanayosimamiwa na CCM. yaani serikali ya chama kilichokuwa kinaunga mkono safari za nje na kuzitetea, leo serikali yake inalaani na kuzizuia. Chama kinapongeza. hakuna mahala wamewaomba radhi watanzania kwa kuboronga. wanageuka juu kwa juu. lakini gharama yake ndio hiyo. wao wenyewe hawajakubaliana wafanye nini. Matokeo yake Magufuli anafanya kile kitu anachoona watu watapenda kusikia au kuona. lakini hii ni nchi. ni taasisi kubwa yenye taasisi nyingi ndani yake. kama hakuna mfumo wa kitaasisi, haya yote yanayofanywa hayana mashiko. kuna mahala yataparaganyika. hata na yeye mwenyewe akiwa bado madarakani. na akija ondoka ndio kabisaa
 
Ndani ya huu mfumo hafiki popote
..hasa akiwa na watu wenye fikra kama zako ndio kabisaa, hatufiki popote.
..kama ulidhani yeye ndio hafiki popote kumbuka kuwa wewe, mimi na yule ndio hatufiki popote.
 
Haya ndio matokeo ya kuwa na kile kinachoitwa MABADILIKO YA KWELI. Haya ni mabadiliko yanayosimamiwa na CCM. yaani serikali ya chama kilichokuwa kinaunga mkono safari za nje na kuzitetea, leo serikali yake inalaani na kuzizuia. Chama kinapongeza. hakuna mahala wamewaomba radhi watanzania kwa kuboronga. wanageuka juu kwa juu. lakini gharama yake ndio hiyo. wao wenyewe hawajakubaliana wafanye nini. Matokeo yake Magufuli anafanya kile kitu anachoona watu watapenda kusikia au kuona. lakini hii ni nchi. ni taasisi kubwa yenye taasisi nyingi ndani yake. kama hakuna mfumo wa kitaasisi, haya yote yanayofanywa hayana mashiko. kuna mahala yataparaganyika. hata na yeye mwenyewe akiwa bado madarakani. na akija ondoka ndio kabisaa

Maneno yako ni ya kweli kamanda; bila kuwa na taasisi imara Magufuli atakuwa anatwanga maji kwenye kinu!!
 
Itabidi mshuke tu na kuanza kuzungusha mikono huko porini na kupiga mayowe mabadilikoooo....
Umenifanya nicheke. Tatizo hili gari huwa lina spidi saana lakini huchakaa haraka hasa safari ikikaribia mwishoni
 
Back
Top Bottom