Magufuli hana uwezo wa kuwakamata na kuwashtaki mafisadi

Kasema ukweli kuwa kuna mambo hawezi kupambana nayo akiwa ndani ya ccm, bahati mbaya hao hao waliotibua ndani ya ccm wamehamia vyama mbadala mbaya zaidi nako wameshika hatamu za uongozi, bora tuache akomae nao humo humo.

Hivi kweli leo Tundu Lissu ni wa kukaa meza moja na Lowasa? Hapana tubaki tu na Magufuli atindue atakapoweza basi.
 
Hao ambao tunadhani wangeweza kuchimbua makaburi marefu ndio hao wana kesi za wizi wa majengo ya ummma, wanakesi za kupokonya mashamba ya watu, wanamiliki apartment kwenye vitega uchumi vya ccm, wamekopa hadi kufilisi benk zetu, sibora tubaki na magufuli tu, angalau anaonyesha ka sura ka utu.
 
Sababu kubwa ya yeye kusema makaburi mengine akiyafukua atashindwa kuyafukia ni kwamba yamo makaburi ambayo na yeye amezikwa.
Hivyo basi, kutokana na roho ya unafiki inayoonekana kumtawala atakimbizana na yale ambayo yeye hajazikwa ndani yake, jambo ambalo linathibitisha kuwa pamoja na kujigamba kote bado hawezi kupambana na ufisadi.
Unapopambana na malaria huchagui mbu gani wa kuua bali unaua kila mbu anayekatiza mbele yako.
Michezo ile ile ya kila siku kwenye akili za Watanzania inaendelea.
 
Kasema ukweli kuwa kuna mambo hawezi kupambana nayo akiwa ndani ya ccm, bahati mbaya hao hao waliotibua ndani ya ccm wamehamia vyama mbadala mbaya zaidi nako wameshika hatamu za uongozi, bora tuache akomae nao humo humo.

Hivi kweli leo Tundu Lissu ni wa kukaa meza moja na Lowasa? Hapana tubaki tu na Magufuli atindue atakapoweza basi.

Sasa Lowasa kahamia upinzani si ndo rahisi kumshughulikia? Maana mlimwogopa akiwa mccm mwenzenu.......lasivyo hamna ushahidi wowote fungeni mabakuli yenu
 
Kasema ukweli kuwa kuna mambo hawezi kupambana nayo akiwa ndani ya ccm, bahati mbaya hao hao waliotibua ndani ya ccm wamehamia vyama mbadala mbaya zaidi nako wameshika hatamu za uongozi, bora tuache akomae nao humo humo.

Hivi kweli leo Tundu Lissu ni wa kukaa meza moja na Lowasa? Hapana tubaki tu na Magufuli atindue atakapoweza basi.
Si msome muelewe mada? Je kama wamehama si ndio ingekuwa rahisi kuwaanika hadharani na kuwashughulikia? Usijidanganye au kujitekenya na kucheka mwenyewe, ndani ya CCM kuna makaburi hata mimi ningenshauri President aachane nayo cha msingi ni kuziba njia zote labda waruke ukuta( impossible mission).
 
Kuna mambo ukiyakumbuka utagundua kwanini, ninasema sio kila Kaburi linafaa kufukuliwa!!!

1.Rais alisema "Kuna MTU alikamatwa anaiba milioni 7 kwa kila dakika, yuko mikono salama". Cha kushangaza kesi yake haisomwi kila Mara kama ile ya Lema!!!

TBC TV Wangeirusha live hii kesi japo tujue inaendaje na imeishaje!!! Lakini wanarusha Chereko chereko badala waende mahakamani siku ikiwa inasikilizwa!!! Any way

2.Kuna MTU amejimilikisha ufukwe wa Koko beach, akawahonga baadhi ya viongozi wa mkoa na Manispaa ili anunue eneo hilo". Cha ajabu hakuna mrejesho WA watu waliotumbuliwa kwa kosa hilo,pia je nani mmilki wa huo ufukwe kwa Sasa?

3.Mkuu wa Wilaya, ambae Wilaya yake itapata NJAA, ajue amejifukuzisha kazi!!!.Sasa karibia 3/4 ya Wilaya zote nchini zina NJAA japo wengine hawasemi kuogopa kutumbuliwa!!!.Je wakisema atawatumbua wote? Au wanategeana nani aanze kusema kisha wengine wapate mrejesho?

Japo ELIMU YETU NI DUNI LAKINI INAWEZA JAPO KUFIKIRIA KIDOGO. NAOMBA KUJIBIWA HOJA HIZO TATU, TUWEKE SIASA KANDO HASA KWA SWALI LA TATU, MAANA NJAA HAINA CHAMA
 
kuna kusema kwa namna nyingi, mbona wamesha sema kuwa njaa ipo, ulitaka watumie ulimi sio? juzi hapa hujaona takwimu zinatolewa za kiasi cha chakula kilichopo au wewe hujasikia?
 
Ukisikiliza kwa maneno wanasema wanachukia ufisadi na wana wanawashughlikia. Jiulize kina nani hao wanao shughlikiwa?

Mafisadi wa awamu hii ni wale wanao Fanya ufisadi wa wazi wakijua ukithubuti kuwasema utaishia jela.

Kashfa za ufisadi wakati huu zinazimwa kimabavu, Kama upo kushoto unamalizwa na kama upo nao unalindwa kwa gharama yoyote.

Wote tumeshuhudia lugumi, sakata la UDA, sakata la matumizi mabaya ya fedha za umma katika miradi ambayo ipo nje ya bajeti, sakata la MV Dodoma, etc.

Ukiambiwa watu wanapiga pesa huwezi kuamini kwa sababu hao hao wanao piga pesa ndio wanatumika kuwanyanyasa wale walio kinyume nao kwa kuwapakazia jambo lolote lililo baya na kuwatangaza kama mafisadi. Joseph msukuma kaa vizuri.

Tutakutana na viongozi wenye kiburi na dharau ambao hawajawahi kutokea toka tupate Uhuru.

Kazi yao ni kuwa aminisha wananchi kuwa wanafanya kazi na hawana msalia mtume kwa kujitumbua wao wenyewe kama sehemu ya propaganda.

Sioni dhamira yoyote ya kupambana na ufisadi kama kuna ufisadi usio weza kuguswa kutokana na nani kafanya.

Kama huamini jiulize Lipumba analindwa kwa sh. ngapi kwa siku, ndio utajua kweli tumerogwa.
 
Saiv upigaji ni mkubwa sana.trafiki tu wanakamua pesa sio mchezo mabarabarani huku
 
Hata mawaziri hawaruhusiwi kusema juu ya ufisadi wowote unao fanywa. Mahakama na bunge nao wanatafutiwa dawa.
 
Ni kweli kabisa. Ma traffic huku Musoma wanashika abiria wasio na elements na wanavaa kienyeji. La kushangaa abiria anashikwa hajavaa elements na anapandishwa kwenye pikipiki ya maaskari isiyo na elements.. Hii nchi ya maajabu sana
 
Wrong data,
 
Nafikiri neno ulilodhamiria kutumia ukimanisha kofia ngumu za kuvaa wakati wa kuebdesha pikipiki ni "helmets" na siyo "elements". Kwa makosa tunajifunza.
 
Saiv upigaji ni mkubwa sana.trafiki tu wanakamua pesa sio mchezo mabarabarani huku
Serikali imedhibiti ufisadi mkubwa ulikuwa unafanyika kwenye mikataba.

Vita ya ufisadi sio ya mtu mmoja au serikali peke yake. Ni vita kila mtu anabidi ashiriki hasa ufisadi mdogo mdogo kama unaofanywa na matrafiki!

Kama wewe umeona trafiki anaomba rushwa halafu ukakaa kimywa unategemea vipi ufisadi upungue?!
 
Subiri mahakama ya Mafisadi itakapoanzishwa July...hapo ndo utajua kama vita hii ni against mafisadi au ufisadi au both (mafisadi na ufisadi)
Mkuu, nasikia ati mahakama yetu pendwa imekosa kesi za Kusikiliza..

Nafikiri mafisadi yameisha!
 
Yeye mwenyewe msafi? Angekuwa msafi asingewazuia opposition parties kufanya mikutano ya hadhara. Kuna kitu kinacho m haunt yeye mwenyewe na chama snachokiongoza
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom