Magufuli hajawaona wataalamu wa IT kutoka CIVE-UDOM?

Zawadi B Lupelo

JF-Expert Member
Jul 19, 2015
2,549
3,722
Ndugu wanabodi salaam.

Awali ya yote nimesikitishwa na kauli ya Rais Magufuli kutangaza kuwa anakwenda kuajili wataalamu wa IT kutoka nchini Rwanda kuja kudhibiti upotevu wa mapato ya kodi nchini Tanzania.

Cha kusikitisha zaidi wakati Mh Rais ana mpango huo tuna Chuo Kikuu Cha Dodoma college of informatics (CIVE) kinatoa wataalamu wazuri sana wa maswala ya IT.

Ni college iliyojengwa kwa kodi za wananchi na ufadhili wa Bill Gate. Vijana hawa wapo vizuri sana kwani ni juzi tu hapa kijana wa hapo UDOM amegundua mtandao unaoelekeana na Facebook unaoitwa 2daysky leo hii ni dharau iliyoje Mh. Rais kudharau uwezo wa vijana wetu hawa.

Ku wapi kubana matumizi?

Hiki chuo kilijengwa cha nini kama hatuamini products zake?
 
NDUGU....
Tatizo sio usomi na wasomi...
Tatizo upigaji, hatuna uadilifu wala uzalendo
Mwanao akishindwa kuuza duka, BORA UAJIRI MTUMISHI...
It's just as simple...
 
Sasa huko ni kugundua au kutoa photocopy?
Huo ni ugunduzi kwani ninaposema unaelekeana simaanishi kuwa unafanana kwa kila kitu isipokuwa functions tu nimejiunga na 2daysky kiukweli amejitahidi sana mpaka sasa amepata ufadhili wa Bill Gate kufuatia ugunduzi wake. Naitumia hii kama mfano tu kuonesha watanzania tunaweza
 
IT haipo kiivyo sana kwamba ukimaliza tu chuo basi unaweza fanya vitu vya ajabu hadi kuitwa mtaalamu.

Inaweza kuchukua miaka zaidi ya 10 kujiweza katika Coding japo wakati unamaliza chuo unajiona unaweza fanya vitu vingi.

IT inachangamoto nyingi kiasi kwamba uzembe kidogo tu,unaleta hasara kubwa kwa kampuni au nchi hasa masuala ya security.

Hivyo huwezi sema UDOM kuna watu wamemaliza na kuwaita wameiva kisawasawa kukabili changamoto za IT.Najua unazungumzia vikazi vidogo vidogo vya kutengeneza application lakini mtu huyo huyo kutengeneza utilitues s/w inakuwa ni kazi sasa hapo atawezaje kufanya security ya kazi zake n.k
 
K

Kwahiyo wanyaruanda ndio wanaexperience kutuzidi ss tz kweli? hakika ukiwa ccm unakuwa na akili za kifisadi tuu
 
Mkuu The hammer
Hapa naomba ufafanue zaidi ķwani katika uelewa wangu S/W program ina sub-programs nyingi na hizo sub-programs kuna threads ambazo zina support hizo sub-programs. Kwa uzoefu imethibitishwa kwamba vijana wa vyuoni wana uwezo mkubwa wa kutengeneza hizo threads tena kwa gharama nafuu sana, labda una ufafanuzi mwingine. Nipo tayari kusahihishwa.
 
Mkuu,sijazungumzia lolote kuhusu hao wataalam wa Rwanda na inawezekana hao wataalamu wa Rwanda wanaozungumziwa sio hawa waliomaliza shule juzi tu na kuitwa wataalamu.Nime-challenge tu kwa mtoa mada kuwa kumaliza chuo tu sio kwamba ndo mtu anakuwa expert wa kumtegemea katika IT.

Nikuulize inajua ni kwanini unatoka na bachelor yako chuoni ila unapoenda kwenye makampuni mengine makubwa wanataka angalau mtu mwenye certificate za mfano CCNA,certificate za Oracle n.k Ukijibu hapo ndo uje uniulize maswali sasa
 
Huo ni ugunduzi kwani ninaposema unaelekeana simaanishi kuwa unafanana kwa kila kitu isipokuwa functions tu nimejiunga na 2daysky kiukweli amejitahidi sana mpaka sasa amepata ufadhili wa Bill Gate kufuatia ugunduzi wake. Naitumia hii kama mfano tu kuonesha watanzania tunaweza

Nadhani lugha nzuri zaidi ungesema ametengeneza mtandao unaofanana na facebook. Huwezi kugundua kitu ambacho tayari kipo hiyo ni ku-copy
 
Mkuu The hammer
Hapa naomba ufafanue zaidi ķwani katika uelewa wangu S/W program ina sub-programs nyingi na hizo sub-programs kuna threads ambazo zina support hizo sub-programs. Kwa uzoefu imethibitishwa kwamba vijana wa vyuoni wana uwezo mkubwa wa kutengeneza hizo threads tena kwa gharama nafuu sana, labda una ufafanuzi mwingine. Nipo tayari kusahihishwa.

Labda nikuulize,umesoma IT? Ili nijue wapi pa kuanzia kukuelekeza.
Pia Kijana,kutengeneza program si kazi ya mchezo hasa kwenye security na hapo kwenye sercurity ndo mahali pa kucheza na algorithm za hatari ambazo wanafunzi wengi tu katika algorithm tunakimbia.

Kwanini makampuni makubwa kama bank hazitoi kazi kwa Watanzania ili wawatengenezee program zao za kibank.
 
Back
Top Bottom