Magufuli hajawaona wataalamu wa IT kutoka CIVE-UDOM?

Labda nikuulize,umesoma IT? Ili nijue wapi pa kuanzia kukuelekeza.
Pia Kijana,kutengeneza program si kazi ya mchezo hasa kwenye security na hapo kwenye sercurity ndo mahali pa kucheza na algorithm za hatari ambazo wanafunzi wengi tu katika algorithm tunakimbia.

Kwanini makampuni makubwa kama bank hazitoi kazi kwa Watanzania ili wawatengenezee program zao za kibank.

Ndio.
Labda tuanzie hapo kwenye security, threads hazina haja ya security.
Suala la security litaanzia kwenye sub-programs hapo ndipo kazi inaanza, na hiyo inafanywa na consultant sio hao vijana wa vyuoni. Na hii inafanyika mara nyingi sana.
Vijana wa kihindi/ Africa hufanya uploads za threads huko Ulaya na Marekani.

N.B. algorithm ya security huanzia kwenye sub-programs na kwenye program yenyewe na huyu consultant wa mwisho ndio mwenye kudhibiti security algorithms zote.
 
kiukweli hawa vijana huwa wako vizuri kwa upande Wa IT na wanaweza kufanya mambo makubwa ila kwa vile wanadharauliwa ndani ya nchi yao basis!
 
Tusiwe hivyo wadau, kwani samata kwenda kucheza soka ubelgiji ina maana hakuna wabelgiji wakupewa hiyo nafasi mpaka muafrika kutoka Tanzania?

Hivi leo kagame akisema anaomba wataalamu wa gas waende rwanda mnataka magufuli akatae.

International relationship z all about win win. Mnataka kula tu wazee bila kuliwa!!!

Acheni hizo, kweli nyinyi ni ma-IT the best in Town wa ku-crack software za wazungu na kuuza kwa bei juu kama yako vile, hebu tupeane wana afrika mashariki. Pamoja daima.
 
Nadhani watu wanamlaumu Magu bure tuu, yeye kasema anachukua kule kwa sababu kwanza imeshafanyiwa utekelezaji na imeonekana kufanya kazi vizuri na pili wale watakaokuja ni watu ambao wameshabobea kwwnye huo mfumo sasa kama humu kuna mtu ambae mfumo wake umeshawahi kutumika na ukawa successfull basi aseme na sio kulalamika tuu kwamba tuna wataalam wakati wataalam wenyewe wa vyeti na labda research projects tuu lakini hawana project yoyote ambayo imeshawahi kutekelezeka.
Badala ya kulalamika pelekeni project proposal zenu serikalini na kwenye media watu wazione wajue mpo maana watu wengi hatujui kama wataalam mpo kweli.
 
Sasa huko ni kugundua au kutoa photocopy?
Hebu tutolee na ww tuone kama unaweza,,kusema unafanana na facebook,angekuambia kitaalamu zaid kuwa amegundua social network kwa jina la 2daysky ucngeelewa,,kakurahisishia maana alijua watu kama nyie hamkosekanagi,so mnahitaj mifano zaid kueleweshwa napo mnakuwa wagumu kuelewa,,
Sasa huko ni kugundua au kutoa photocopy?
 
hicho kiujinga cha 2daysky ndo utalaamu? hamna kitu apo... kama hatuma watalaamu wacha tufanye outsourcing
 
IT haipo kiivyo sana kwamba ukimaliza tu chuo basi unaweza fanya vitu vya ajabu hadi kuitwa mtaalamu.

Inaweza kuchukua miaka zaidi ya 10 kujiweza katika Coding japo wakati unamaliza chuo unajiona unaweza fanya vitu vingi.

IT inachangamoto nyingi kiasi kwamba uzembe kidogo tu,unaleta hasara kubwa kwa kampuni au nchi hasa masuala ya security.

Hivyo huwezi sema UDOM kuna watu wamemaliza na kuwaita wameiva kisawasawa kukabili changamoto za IT.Najua unazungumzia vikazi vidogo vidogo vya kutengeneza application lakini mtu huyo huyo kutengeneza utilitues s/w inakuwa ni kazi sasa hapo atawezaje kufanya security ya kazi zake n.k
Kwa hiyo hata hao malecture nao hakuna kitu c ndo hivyo????jamaa katolea mfano wa chuo cha udom,,but wapo wengi watz ambao ni wataalam wa it,wengine wamesomea nje ya nchi,,angewaita alafu tuone kama wangeshindwa anachokihitaj..
 
Mkuu,sijazungumzia lolote kuhusu hao wataalam wa Rwanda na inawezekana hao wataalamu wa Rwanda wanaozungumziwa sio hawa waliomaliza shule juzi tu na kuitwa wataalamu.Nime-challenge tu kwa mtoa mada kuwa kumaliza chuo tu sio kwamba ndo mtu anakuwa expert wa kumtegemea katika IT.

Nikuulize inajua ni kwanini unatoka na bachelor yako chuoni ila unapoenda kwenye makampuni mengine makubwa wanataka angalau mtu mwenye certificate za mfano CCNA,certificate za Oracle n.k Ukijibu hapo ndo uje uniulize maswali sasa
Hujui chochote cha IT Acha kudanganya "certificate za Oracle"?
 
Naomba mtulie, tutawaleta wataalamu wa IT, toka Rwanda, Bunge na hicho chuo chenu cha udom vitahamishiwa Rwanda pia.
 
Ndugu wanabodi salaam.

Awali ya yote nimesikitishwa na kauli ya Rais Magufuli kutangaza kuwa anakwenda kuajili wataalamu wa IT kutoka nchini Rwanda kuja kudhibiti upotevu wa mapato ya kodi nchini Tanzania.

Cha kusikitisha zaidi wakati Mh Rais ana mpango huo tuna Chuo Kikuu Cha Dodoma college of informatics (CIVE) kinatoa wataalamu wazuri sana wa maswala ya IT.

Ni college iliyojengwa kwa kodi za wananchi na ufadhili wa Bill Gate. Vijana hawa wapo vizuri sana kwani ni juzi tu hapa kijana wa hapo UDOM amegundua mtandao unaoelekeana na Facebook unaoitwa 2daysky leo hii ni dharau iliyoje Mh. Rais kudharau uwezo wa vijana wetu hawa.

Ku wapi kubana matumizi?

Hiki chuo kilijengwa cha nini kama hatuamini products zake?
Kwani wale wataalamu wa It wa chadema wapo wapi?
 
Umesema sawa!

Kiukweli hatuwezi kuwategemea UDOM hawa ni wachanga ktk field!

Ila kuna thousands of Tanzanians duniani wanatoa huduma ktk mataifa mengine, pay them, warudishe nyumbani ndugu zetu! Shida unapofikiri kubana matumizi unapodeal na Watanzania Ila unawish kuspend kwa wageni! Mfano kama mnyarwanda atataka kulipwa 1,000/- na Mtanzania 100,000/- bado ni gharama nafuu kumlipa mtanzania pesa itakayozunguka nchini, kuliko kulipa buku ambayo ndio hairudi tena ktk mzunguko wetu!

Hili la kukodi wanyarwanda likifanyika, awamu ya 5 itaingia ktk mgogoro mkubwa sana na Watanzania na wengi tutaongea ktk ballot box 2020! Ile dhamira njema serikali ya yetu itatoweka! Lakini for centuries tutalipia gharama za urafiki huu wa mashaka!
 
IT inachangamoto nyingi kiasi kwamba uzembe kidogo tu,unaleta hasara kubwa kwa kampuni au nchi hasa masuala ya security.

Hivyo huwezi sema UDOM kuna watu wamemaliza na kuwaita wameiva kisawasawa kukabili changamoto za IT.Najua unazungumzia vikazi vidogo vidogo vya kutengeneza application lakini mtu huyo huyo kutengeneza utilitues s/w inakuwa ni kazi sasa hapo atawezaje kufanya security ya kazi zake n.k

Katika issues za security, bado kwa mtu wa UDOM Utakuwa uzembe, Ila kuna guarantee ya hujuma toka kwa mnyarwanda!

Kama tunafahamu vema mtaalam wako wa IT huwa na codes ambazo anaweza kuaccess system, anaweza ku hack mfumo mzima wa mawasiliano, anaweza kuuza codes na kila kitu anachotaka kufanya akiwa mbali!

Tunawezaje kuwa control wanyarwanda au ndio tutaomba msaada wa Kagame kuwakamata kama watatuhujumu!
 
NDUGU....
Tatizo sio usomi na wasomi...
Tatizo upigaji, hatuna uadilifu wala uzalendo
Mwanao akishindwa kuuza duka, BORA UAJIRI MTUMISHI...
It's just as simple...
Kama nchi nzima hatuna mwadilifu, tunajuaje hata hiyo approach ya kuleta wataalam toka Rwanda si harakati za upigaji?
 
Umesema sawa!
Kiukweli hatuwezi kuwategemea UDOM hawa ni wachanga ktk field!
Ila kuna a thousands of Tanzanians duniani wanatoa huduma ktk mataifa mengine, pay them, warudishe nyumbani ndugu zetu! Shida unapofikiri kubana matumizi unapodeal na Watanzania Ila unawish kuspend kwa wageni! Mfano kama mnyarwanda atataka kulipwa 1,000/- na Mtanzania 100,000/- bado ni gharama nafuu kumlipa mtanzania pesa itakayozunguka nchini, kuliko kulipa buku ambayo ndio hairudi tena ktk mzunguko wetu!
Hili la kukodi wanyarwanda likifanyika, awamu ya 5 itaingia ktk mgogoro mkubwa sana na Watanzania na wengi tutaongea ktk ballot box 2020! Ile dhamira njema serikali ya yetu itatoweka! Lakini for centuries tutalipia gharama za urafiki huu wa mashaka!
Mshaurini kama atasikia. Niliambiwa yeye anajua yote, wala hahitaji msaada wa maoni ya mtu.
 
Kama mnaweza mbna hamjawahi kutoa mapendekezo yenu serikalin kuwa mapato yanapotea na sasa tufanye 123.IT ni kitu kinachobadirika kila wakati yawezeka kinacholetwa sisi hatuna na hapo udom bado hakijafundishwa, au semeni nyie mlitaka mpewe nafasi ya kwenda Rwanda kujifunza hicho kitu.
 
Hujui chochote cha IT Acha kudanganya "certificate za Oracle"?

We ndo hujui IT.Nikufahamishe IT zina certificate nyingi katika kukufanya kuwa mjuzi wa kitu kimoja mathalani Database.

Pitia hizi link na uache uvivu wa kujishughulisha kidogo kabla ya ku-comment.
Oracle Certification Program - Wikipedia, the free encyclopedia
All Certifications | Certifications | Oracle
Ni kwamba hizi kampuni ambazo zina product zao huwa wanatoa certificate za ngazi tofauti tofauti kama ilivyo kwa cisco wanavyotoa Cisco certifications - Wikipedia, the free encyclopedia soma table hiyo uone hizo level zilivyo nyingi,basi ujue sasa Oracle,java,product zote za microsoft zinazohusu Database na programing language huwa wanatoa certificate za ngazi tofauti tofauti ili kukupa u-profession wa ngazi uliyofikia usije ukaharibu kazi za watu.

Kama wewe ni IT then hujui haya sasa tutegemee nini kwako,Magufuli akuite umfanyie troubleshouting katika office yake kwenye Database,Idiot.

Kajipangeee!!
 
Ndio.
Labda tuanzie hapo kwenye security, threads hazina haja ya security.
Suala la security litaanzia kwenye sub-programs hapo ndipo kazi inaanza, na hiyo inafanywa na consultant sio hao vijana wa vyuoni. Na hii inafanyika mara nyingi sana.
Vijana wa kihindi/ Africa hufanya uploads za threads huko Ulaya na Marekani.

N.B. algorithm ya security huanzia kwenye sub-programs na kwenye program yenyewe na huyu consultant wa mwisho ndio mwenye kudhibiti security algorithms zote.

Mr.unafikiri nakuelewa unachozungumza hapa? Ndo maana nikauliza una ujuzi wa IT? Then suala la programing sio suala la kujua tu umefanya hiki basi linaleta jibu hili na suala gumu sana ni kwenye loop ila kuna namna ya kuweka code zako ili iwe faster katika excution n.k. Na loop inahitaji uandike algorithm sio 'procedure' kama kweli unafanya kazi kitaalamu.

Kazi ya Consultant ni kuandika security ya program? Dah! Sina uhakika kwa hilo maana sijawahi fanya kazi za hivyo.
 
Back
Top Bottom