Bumpkin Billionare
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 1,332
- 621
Mheshimiwa Mnyika!Kupanda au kushuka kwa bei ya bidhaa yoyote inategemea na "simple theory of demand and supply". Masuala ya kupanga bei yaachiwe soko kwani usafiri uko huria na dynamics hizo zitumike.
Hapo tutahitaji nguvu za ziada. Nauli za vivuko vyote viko juu Kigamboni I am told ndiyo ya chini zaidi! Tuangalie na kushupalia bei ya umeme ambayo inagusa kila mtu nchi nzima aliye hai na hata !
Sasa wewe pia unaleta 'Simple Theory of Kata Schools Standards' kwenye bidhaa muhimu ktk maisha. Mh. Mnyika hakusema kuwa soko litakwama, yeye amechelea kuwa huduma zitakuwa ghali. Tuwe tunazingatia application ya theories tunazofundishwa darasani na impact yake ktk maisha ya watu. Hebu niambie namna ambayo demand inaweza ikashusha price ya bidhaa chini zaidi ya accumulated cost of production kiasi niamini tuache tu gharama za usafiri zipande na bei itashuka yenyewe.
Kama unaona alilolisema Mh.Mnyika halina maana kwa wakazi wa Kigamboni juu ya kupanda bei za bidhaa za vyakula, ilitoka wapi haja ya Mkuu wa Nchi kukemea kupanda kwa bei ya sukari? Kwa nini asingeacha demand iishushe?
Kuwa juu kwa gharama za vivuko mahali pengine hakutoi uhalali wa kupandisha Kigamboni. Kama lengo ni kuweka sawa viwango kwa nini wasishushe huko gharama zilipo juu? Kumbuka ile ni huduma na sio biashara na ukileta mambo ya kulinganisha nitakuomba utulinganishe na Kenya ambako kivuko cha Mombasa (Likoni) ni bure.
Mwalimu wako alipaswa kukuelewesha kuwa elasticity of demand inakuwa determined na price kama other costs zitabakia kuwa constant. Gharama za usafiri zikipanda mwenye Guta hazimuumizi, anazihamishia kwa mwenye Genge ambaye naye anazipost kwa mlaji. Hakuna namna ya kuwapa nafuu wenzetu wa Kigamboni ktk hili zaidi ya kushusha gharama zisizo za lazima.
Ni kawaida ya CCM kukosa ubunifu na ndio maana bajeti ikicheza kidogo tunapandishiwa kodi kwenye sigara na bia. Na hili ni zao la wachumi wa namna yako ya kufikiri.
Na kwa yeyote mwenye FIKRA KUWA MAGUFULI NA TEMESA ni watu smart asome hapa: Kati ya mwaka 2008 au 2009(sina hakika na muda) hiki kivuko kipya kikubwa kilivyoletwa nchini, wataalam wa kukiunganisha waliestimate assembly time kuwa miezi 5 lkn badala yake ikawa 8.(hoja yangu haiko hapa)
Kwa muda woooote huo wa miezi hiyo ya kuunga ferry mpya, TEMESA hawakuwahi kufikiri ni wapi kitakuwa kikitia nanga. Ni baada ya kivuko kukamilika ndio zikaanza pilika pilika za kutengeneza GATI ya kupaki kivuko kipya kwani ni kikubwa kuliko vile vilivyokuwa vikitumika. Matokeo yake ikawa usumbufu mkubwa wa kuvuka kwani ferry moja ilitumika kuvusha watu na magari na nyingine ilikuwa bize kubeba mawe kwa ajili ya ujenzi wa gati upande wa magogoni. Ikumbukwe wakati huo huo daraja la Mto Kizinga (karibu na Mtongani kama unaenda Mbagala) nalo lilikuwa under construction (KAJIMA) kwa hiyo barabara ilifungwa. Hii ni kudhihirisha uzembe kwani gati zingeweza kujengwa taratibu kwa ferries kubeba mawe usiku taratibu kwa miezi ile ambayo assembling ilikuwa inafanyika. Hili linajirudia tena kwenye vigezo gani vimezingatiwa ktk kupandisha bei ya GUTA na MKOKOTENI. Mimi siamini kama TEMESA na MAGUFULI ndio watu sahihi wa kulifanyia kazi suala hili. Wachumi na Wataalam wa Sayansi ya Jamii ndio walitakiwa walifanyie kazi hili, tuone tofauti ya ukandarasi wa majengo na usimamizi wa huduma za jamii. Si kila sehemu siasa inafaa kutumika