Magufuli hajaleta nidhamu makazini, bali ameleta woga kwa watumishi.

Bonde la Baraka

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
4,580
7,934
Naweka BIG NO kwenye hili suala wanalosema watu kuwa Magufuli ameleta nidhamu makazini.
Watumishi wa umma(baadhi) wamekuwa na woga kuhofia kuwajibishwa, hasa kwenye Halmashauri maana huko kila mtu hujigeuza Mungu mtu. Sheria wakati mwingine hazifuatwi bali harsh tu.
Hakuna nidhamu kwa mtu asiyepandishwa daraja, asiyeongezwa mshahara, asiyebadilishiwa cheo au kitengo baada ya kujisomesha kwa gharama zake n.k . Kinachofanyika ni kuigiza tu kuwa yu mwema na mchapakazi kwa kitambo kidogo.
Mwenye ushahidi kuwa sasa amekuwa na nidhamu zaidi katika kipindi hiki cha Magufuli zaidi ya kipindi cha Kikwete aje atueleze.
 
Na kwanini uwe na woga kama unafanya kazi zako ipasavyo na unafuata sheria???
 
Mimi sina woga hata keep kidogo, kuja tu hapa kuandika Magufuli kaleta woga kwa watumishi inaonyesha kuwa najitambua. Wewe huwezi
Na kwanini uwe na woga kama unafanya kazi zako ipasavyo na unafuata sheria???
 
Yani ni majanga Kwa sasa hivi Takukuru wameweka kambi ofisi za halmashauri kazi haifanyiki tena.
 
Wengi ni woga kwa sababu hawakuzoe kufanya kazi zao ipasavyo. Na walivyo wapuuzi huwatishia na watu wengine.
 
Mratibu wetu wa elimu ikifika saa moja na nusu siku hizi anaondoka na daftari la mahudhurio anarudisha usiku
 
Nilikuwa wizara fulani juzi wakati nasubiria huduma walikuja wahusika kama 9 hivi kwa nyakati tofauti kuniuliza na kuhakikisha kama nimeshasikilizwa.
Hili ni jambo jema.
 
Mtu anayejua kufanya kazi hawezi kuwa muoga. Anajivunia na skills zake na hata kujiongeza mwenyeweeee

Uoga utakuwa kwamba hawajui kufanya kazi walizopangiwa. Ni wengi sana.. JPM anahitaji vichwa vyenye exposure kumsaidia.
 
Kwanini pawepo na makamusi ya kitabibu, kiuchumi, lugha, utumishi n.k?
Neno moja linatofautiana kulingana na aina ya mimbari.
Kiutumishi neno woga halina tija na ni baya, hata kibiblia Waoga hawataurithi ufalme wa mbinguni.
Ehee ufipa kwa porojo

Hivi ukisema nina hofu ya mungu inamaana wewe humtii mungu
 
Na kwanini uwe na woga kama unafanya kazi zako ipasavyo na unafuata sheria???
Hata Mimi nawashangaaa magu bana kiboko Alisema atanunua korosho zote ameshanunua wanajeshi wanasomba halafu wanaenda bangua kwa mdomo uzuri wa kiongozi ni mfano kama alivoonesha halafu hata zikikaaa miaka 5 tutauza tuuu na zikikaaaa sana huwa zinakuwa dhahabu kama si makinikia .cccm oyeeeeeeeeee
 
Nakubaliana na wewe mwingine anaogopa kabisa kufanya maamuz ya msingi kama ku-sign document flan kwasababu huenda akawajibishwa bila kuangalia taaluma yake inasema nini kuhusu juu ya jambo hilo...
 
Naweka BIG NO kwenye hili suala wanalosema watu kuwa Magufuli ameleta nidhamu makazini.
Watumishi wa umma(baadhi) wamekuwa na woga kuhofia kuwajibishwa, hasa kwenye Halmashauri maana huko kila mtu hujigeuza Mungu mtu. Sheria wakati mwingine hazifuatwi bali harsh tu.
Hakuna nidhamu kwa mtu asiyepandishwa daraja, asiyeongezwa mshahara, asiyebadilishiwa cheo au kitengo baada ya kujisomesha kwa gharama zake n.k . Kinachofanyika ni kuigiza tu kuwa yu mwema na mchapakazi kwa kitambo kidogo.
Mwenye ushahidi kuwa sasa amekuwa na nidhamu zaidi katika kipindi hiki cha Magufuli zaidi ya kipindi cha Kikwete aje atueleze.

Kwani katika Kipindi cha Kikwete hiyo Nidhamu kwa Watumishi wa Umma ilikuwepo? Hoja yako imekaa zaidi katika ' Kumnanga ' tu Rais Dkt. Magufuli pamoja na Serikali yake ya sasa ila siyo ya kuelezea uhalisia wa mambo. Na unaoneka umeandika Kimahaba ya Kisiasa zaidi na siyo Kimtizamo.

Ni kweli siyo kwamba Rais Dkt. Magufuli amefanikiwa kwa 100% ila angalau ameweza Kuthubutu na kidogo sasa kuna ' some seriousness ' huko Serikalini. Halafu usisahau kwamba nidhamu ya Watumishi wa Serikalini hailetwi tu na Rais wa nchi bali huanzia Kwanza katika Maadili ya Mtu mmoja mmoja kisha Rais yeye ' anaikazia ' tu.

Yangu ni hayo tu.
 
So kuna baadhi ya watu wanaishi kama digidigi?
Nakubaliana na wewe mwingine anaogopa kabisa kufanya maamuz ya msingi kama ku-sign document flan kwasababu huenda akawajibishwa bila kuangalia taaluma yake inasema nini kuhusu juu ya jambo hilo...
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom