Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 20,353
- 38,574
Kama kuna tamaduni ambayo CCM wanatakiwa waikwepe kwa gharama yoyote ile ni ya kuwa na Mwenyekti ambaye pia ni Rais wa nchi. Mantiki ya kuwa hivyo ilianza wakati ule wa chama kushika hatamu ambapo kulikuwa hakuna vyama vingine vya siasa zaidi ya CCM. Lakini kwa sasa ambapo watu wameshaanza kuona kuna tofauti kati ya chama cha siasa na serikali ni vyema CCM ikatafakari kama wanahitaji kuendelea na tamaduni hiyo.
Siku hizi watu wanaotamka "viongozi wa chama na serikali" wamebakia wachache sana wakiongozwa na Nape. Magufuli mimi namkubali sana kwa uwezo wa kukariri namba lakini sidhani kama ana ladha ya uanasiasa.Hata wakati wa Kampeni waliovutiwa na Magufuli ni wale waliokuwa na kiu ya kuwakomoa wengine lakini siyo kwamba yeye mwenyewe ana mvuto wa kisiasa.
Chama cha siasa kinahitaji kuongozwa na mtu mwenye Karisma na Maono vitu viwili ambavyo Mwana CCM huyu Magufuli hana. Kikwete alikuwa na Karisma lakini kina Lowassa na kundi lake wakamsaidia kuweka maono. Kwa kutumia Karisma yake akawatumia wana mkakati Nape na Kinana kupambana na Lowassa lakini alipotaka chama kiwe na Maono alimtafuta Mangula toka kwenye mashamba yake ya Viazi kuja kuwa Makamu mwenyekiti wake.
Hakuna jambo mahsusi ambalo Magufuli amewahi kulifanya kwa miaka zaidi 20 aliyokuwa kwenye siasa linaloweza kumfanya kuwa na sifa ya kuongoza taasisi kubwa ya kisiasa kama CCM. Mtu asiye kuwa na Karisma wala maono kwenye taasisi ya kisiasa ni msiba mkubwa. Mkapa alikuwa na Maono lakini alimtumia Malecela aliyekuwa na Karisma kuendesha CCM wakati yeye akiendesha Serikali.