Magufuli: Damu, roho vya Magdalena Sakaya ni CCM. Jamani si aende tu kwanini anavuruga CUF

Mzee pambana na hali yako... na kwanza hata hawajakuomba vyeo, na kwa chuki hizi usituambie tena tukuombee kwa MUNGU!
 
Kwa ile nyomi ya Uwanja wa Tanganyika jana, wapinzani wajipange sana. Kigoma ni moja ya mikoa ya kwanza kupokea upinzani. Sijui wataenda nao mbele kwa umbali gani, maana siasa za sasa ni za kuwashika mkono walio wengi na wakiamua watakusambaratisha...wapiga kura halali
 
Ata Prof. Kitila kule Kigoma aliambiwa mbele ya umma kuwa sura yake ni ACT Wazalendo, lakini moyoni ni CCM.

Aisee, sijui alijisikiaje jamaa. Na Mkulu anapenda wapinzani wa dizaini hii, wanaohujumu vyama vyao kwa maslahi mapana ya CCM. Ndiyo maana Zitto aliitwa mpinzani mzalendo na yule wa Kakonko "kambunge ka CHADEMA"
 
Kwa maelezo aliyoyatoa Jana Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi JPM kwa mbunge wa kaliua -CUF Magdalena Sakaya, Je ni Sahihi Chama cha wananchi CUF kuendelea na mbunge huyo? Je sakaya ni mpinzani wa kweli? Kubaki na mwanachama wa aina hiyo ni athari gani chama kinaweza kupata?

Tukumbuke sakaya ktk bunge lililopita amepigia kura ya ndio bajeti ya serikali kinyume na msimamo wa Vyama vya upinzani.

Sakaya katika jimbo lake hakuna diwani wa CUF hata mmoja.
5e1adedd8ec0ed8f78eb3a6c415d63b1.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wapinzani hawana tofauti na mtoto....mtoto akioneshwa kipepeo basi kila kinachopaa huendelea kukiita kipepeo...yaani akiona inzi atamuita kipepeo,akiona mwewe atamuita kipepeo mkubwa,akiona nyuki atamuita kipepeo anayeuma akiona aircraft atasema ni kipepeo kinachobeba qatu.
 
Kwenye siasa hakuna rafiki wala adui wa kudumu. Ni mwendo wa kuangalia fursa tu.
 
Hivi nyie upinzani mnauelewaje? Mbona ni mazuzu kiasi hicho? Sasa mlitaka jpm awaambie ccm wasishirikiane na sakaya na hapo hapo aseme analeta maendeleo kweli! Aise upinzani hapa bongo ni uadui kila kitu wao ni kupiga na kuponda tu. Kwa misingi hii bora vyama vya upinzani vifutwe mana havina nia nzuri bali kukwamisha lolote lisifanikiwe
 
Back
Top Bottom