Kambi ya Fisi
JF-Expert Member
- Feb 3, 2018
- 13,463
- 21,945
Wapendwa jana nilikwenda kupokea mgeni kutoka mkoani ambaye aliniomba nikampokee pale Mbezi Luis kwenye stand mpya ya Magufuli, binafsi nilikuwa sijawahi kuingia ndani ya hiyo stand tangu izinduliwe Ila mara nyingi nimesikia na kusoma ktk vyombo vya habari hapa Tanzania wakiisifia kuwa ni stand ya kimataifa
Hata hivyo kila nilipopita Morogoro rd hapo Mbezi Luis niliona kwa nje jengo hilo limavutia kwa macho hivyo nikawa naamini kuwa kweli ni stand ya kimataifa.
Jana basi ndio nikaingia humo ndani kwa mara ya kwanza ili nipokee mgeni kutoka mkoani, kwa kweli stand hiyo ni ya kimtaa na sio kimataifa kwa sababu
1. Hakuna alama ama maelekezo yoyote kwa mgeni isipokuwa kuna utitiri wa machinga, wapiga debe, wabeba mizigo wenye kuleta usumbufu kwa abiria.
2. Hakuna taarifa yoyote kuhusu kuwasili kwa basi husika
3. Hakuna viti vya kukaa kwa wale wanaosubiria wageni wao.
(mfano, stand za mwendo kasi kuna mabenchi ya kukaa kwa abiria waosubiria usafiri) lakini kwa hii stand unakalia kingo ya parking
4. Mrundikano wa wauza mikate walioweka meza zao za mikate pasipo mpangilio wowote, wauza Jojo, wauza fegi, wauza dawa za kienyeji na mambo mengi yanayo fanana na hayo
Sijajua hasa mataifa gani yanaitumiaga hii stand hadi iitwe stand ya kimataifa Ila najua chinga, wasukuma mikokoteni na maasai wauza mitishamba ndio watumiaji wakuu kibiashara ktk hii stand na wote ni watanzania tu
Anayejua ukimataifa wa hii stand ulipo anijuze tafadhari.