Magufuli Bus Terminal haijakidhi viwango vya kuitwa stendi ya Kimataifa

Hahahaa hata mie sijui kwa nini huwa wanafanya hivyo
halafu chumvi inabaki exposed nje ya yai siku nzima...
kuna nzi, Covid 19 virus, mikono ya wanaume wanaokojoa mitaani bila kunawa halafu wanakuja kuchagua yai wanaona dogo wanalirudisha...

mayai ya mtaani yapigwe marufuku
 
Kule juu kuna lounge kubwa tu.
Bado haijaisha kwa kiwango chote.
Wapiga debe ni changamoto bado.
Mmoja nilimwambia sijisikii kuongea na wewe. Akaniamba hajawahi kujibiwa na binadamu vile.
 
Kule juu kuna lounge kubwa tu.
Bado haijaisha kwa kiwango chote.
Wapiga debe ni changamoto bado.
Mmoja nilimwambia sijisikii kuongea na wewe. Akaniamba hajawahi kujibiwa na binadamu vile.
Pole sana mkuu, siku nyingine akikusumbua majibu kwa kichina atasepa kimya kimya
 
Ebu tuambie Stand gani zilizopo maeneo mengine au kwenye mikoa mingine tunaweza kulinganisha na ile.
Leta taarifa kuwa kuna mabasi yanakosa nafasi kuingia na kupaki ndani
 
Ebu tuambie Stand gani zilizopo maeneo mengine au kwenye mikoa mingine tunaweza kulinganisha na ile.
Leta taarifa kuwa kuna mabasi yanakosa nafasi kuingia na kupaki ndani
Umewahi kuingia Msamvu bus terminal?
Magufuli Bus Terminal ni ya kijinga mno aheri Msamvu bus terminal ama pale Dodoma pako poa kidogo
JamiiForums137962104.jpg
JamiiForums1616884762.jpg
 
Pole sana mkuu, siku nyingine akikusumbua majibu kwa kichina atasepa kimya kimya
Hahahahah .
Asante . Unajua jamaa alinishangaa, vile inakuwa una mambo mengi. Unataka kukamilisha upo eneo la tukio Afu anakufuata mtu na kukuuliza maswali lukukii yani mm nakereka sana mkuu.
 
Najua sio wote wanaoweza kuelewa kwa sababu tunatofautiana kiakili Ila nimeona wapo watu wengi hawakubali hii stendi kuitwa ya kimataifa kwa kuwa ipo kishamba mno hasa humo ndani.

Mie sio mhandisi bali ni raia wa kawaida ambaye nina macho ya kuona na masikio ya kusikia hivyo niliyoyaona ndani ya hiyo Bus terminal hainishawishi nitoe pendekezo la kiufundi kufanya marekebisho bali nasema tuache kudanganyana tuseme tu ukweli mkandarasi hakuwa na uwezo wa kujenga hiyo bus terminal Ila alipewa hiyo kazi.

Kuhusu ubora wa flyover siwezi kuzisifu hizo flyover kuwa zipo vyema, kwa taarifa tu bado bado kuna foleni pale ubungo na Tazara hivyo bado shida ni kubwa na wanaoleta hiyo shida ni wasimamizi wasio na uwezo wa kufanya kazi
Ni sahii tuna tofautiana kiakili, lakini naomba hata hivyo uelewe kuwa tunaweza tukawa na akili sawa, bado tukatofautiana kimaarifa na exposure.

Wewe unadai kuwa hiyo stendi imekaa kishamba mno ndiyo maana haina hadhi ya kuitwa stendi ya kimataifa, sawa nakubaliana na hilo, ila tu narudia tena kusema kuwa, kama unaona imekaa kishamba mno basi ilitakiwa utuambie jinsi gani stendi yenye hadhi ya kimataifa ilitakiwa ionekane. Kusema tu kuwa imekaa kishamba mno bila wewe mwenyewe kutoa mapendekezo, hiyo peke yake naona haitoshi ndugu yangu, kwani mambo hayaendi kirahisi hivyo kama unavyo fikiri.

Eleza exactly ni kitu gani hiyo stendi ilitakiwa iwe nacho ili iwe na hiyo hadhi inayo takiwa. Kama unatoa critic kwa wajenzi na wapanga miji unatakiwa useme wewe ulikuwa unapendelea nini ili wao nao wakuelewe.

Katika kupendekeza kitu haina haja wala umuhimu wa mtu kuwa mhandisi, kwani kwa kukupa siri tu, sio wahandisi wote walio soma wanajua kila kitu. Yako mambo ambayo wao nao hawayaelewi na wahandisi walio maliza masomo yao nchini ndiyo kabisaa!

Wewe kama mmoja wapo wa mtumiaji wa hiyo stendi kuna mambo unaweza ukawa umeyapenda na ambayo pengine wakati wa ku-plan na kujenga hiyo stendi hao wahusika hawakuyajua au waliyajua, lakini waliamua kuyapuuzia, ni haki yako kuyasema bayana ili na wenzio nao wakafaidika nayo. Hiyo ndiyo maana ya TEAM WORK!.

Wenzetu wa majuu waki-plan kufanya ujenzi mkubwa kama huu, mara nyingi wananchi wanaombwa kutoa maoni yao juu ya vitu ambavyo vinatakiwa viwe considered kwenye hilo jengo. Kwenye nchi kama hizi zetu wajenzi na watu wanao plan hiyo miradi sijui kama wanafanya hivyo. Kama hawafanyi hivyo basi nafikiri itakuwa tu ni kwa ajili ya ukosefu wa akili ya kuthaminiana.

Mimi sikubaliani hata mara moja na wewe kuwa, kwa mtazamo wako, mkandarasi hakuwa na uwezo wa kujenga hiyo bus terminal, Ila alipewa tu hiyo kazi. Naomba nikuambie kitu ndugu yangu, tatizo hapa sio mkandarasi, tatizo hapa ni sisi wenyewe na wasimamizi tuliowapa mamlaka ya kusimamia miradi kama hiyo. Sisi na wasimamizi wetu tunakasumba ya kuwaza utajiri tu wa hela za dezo. Miradi kama hii ndiyo utajiri wa watu wenye mamlaka kujitajirisha na sio kingine.

Mimi ningekuomba tu tushukuru kuwa mradi kama huo kwa namna fulani umemalizika na kutoa huduma. Tumwombee Jemedari wetu Hayati Rais Magufuli huko aliko peponi Mungu amweke mahali pema. Yeye ndiye aliye yawezesha hayo yote yaka kamilika. Japo kuwa sio kwa kurizisha ki hivyo.

Na hivyo hivyo kuhusu ubora wa flyovers zetu, kama ulivyonsema, huwezi kuzisifu hizo flyovers kuwa zipo vyema na kwa taarifa yako bado kuna foleni pale Ubungo na Tazara ambazo bado ni shida kubwa na wanaoleta hizo shida ni wasimamizi wasio na uwezo wa kufanya hizo kazi, huo ni ukweli usiopingika. Na ndiyo maana mimi napinga kama wewe kuwa yale madaraja mawili hayawezi kuwa na hadhi ya kuitwa Flyover. Yale ni madaraja tu. Period!

Kwenye hii nchi ndgu yangu kulikuwa na dhana ya baadhi ya Marais na viongozi, miradi kama hii huko nyuma haikumalizika na hela zilikwisha potea na viongozi wa juu hata hawakuwa na ubavu wa kuhoji kulikoni?
 
Mwendazake na Mfugale wLitupiga hapo
Wapendwa jana nilikwenda kupokea mgeni kutoka mkoani ambaye aliniomba nikampokee pale Mbezi Luis kwenye stand mpya ya Magufuli, binafsi nilikuwa sijawahi kuingia ndani ya hiyo stand tangu izinduliwe Ila mara nyingi nimesikia na kusoma ktk vyombo vya habari hapa Tanzania wakiisifia kuwa ni stand ya kimataifa

Hata hivyo kila nilipopita Morogoro rd hapo Mbezi Luis niliona kwa nje jengo hilo limavutia kwa macho hivyo nikawa naamini kuwa kweli ni stand ya kimataifa.

Jana basi ndio nikaingia humo ndani kwa mara ya kwanza ili nipokee mgeni kutoka mkoani, kwa kweli stand hiyo ni ya kimtaa na sio kimataifa kwa sababu

1. Hakuna alama ama maelekezo yoyote kwa mgeni isipokuwa kuna utitiri wa machinga, wapiga debe, wabeba mizigo wenye kuleta usumbufu kwa abiria.

2. Hakuna taarifa yoyote kuhusu kuwasili kwa basi husika

3. Hakuna viti vya kukaa kwa wale wanaosubiria wageni wao.
(mfano, stand za mwendo kasi kuna mabenchi ya kukaa kwa abiria waosubiria usafiri) lakini kwa hii stand unakalia kingo ya parking

4. Mrundikano wa wauza mikate walioweka meza zao za mikate pasipo mpangilio wowote, wauza Jojo, wauza fegi, wauza dawa za kienyeji na mambo mengi yanayo fanana na hayo

Sijajua hasa mataifa gani yanaitumiaga hii stand hadi iitwe stand ya kimataifa Ila najua chinga, wasukuma mikokoteni na maasai wauza mitishamba ndio watumiaji wakuu kibiashara ktk hii stand na wote ni watanzania tu

Anayejua ukimataifa wa hii stand ulipo anijuze tafadhari.
View attachment 1837197View attachment 1837198View attachment 1837201
 
Back
Top Bottom