MAGUFULI BABA UZIDI KUBARIKIWA WATANZANIA TUNAKUELEWA KWA KULIREJESHA TAIFA MIKONONI MWA MUNGU .

katichi

JF-Expert Member
Nov 26, 2016
2,033
2,000
"Wametuletea mambo kubakana,Wanaume kwa wanaume,Wanawake kwa wanawake, wakati hata ng'ombe au mbuzi hazijawahi kufanya huo mtindo,ni ujinga ,ni upumbavu,ifike mahali watanzania tujitambue na tumuogope Mungu, haya mambo ya kukopi kopi tutakopi vitu vya ajabu".(JPM)


Ifike hatua watu tusimamie na kunena ukweli , watu wa nchi kufanya uchafu huu hakika laana hii italitafuna taifa hatutaona mema ambayo Mungu amekusudia hata tukikazana kujenga viwanda kila mtaa kama taifa limekataliwa na Mungu kwa ajili ya laana hizi tutabaki kulialia milele mana pasipo Mungu hauwezi lolote.

Neno la Mungu linasema utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na hayo mengine yote tutazidishiwa iwe ni ajira,afya, baraka, elimu( Astashahada,Stashahada na Shahada).

Tukumbuke pia njia iendayo upotevuni ni pana na waendao huko ni wengi si ajabu kuona wengi wakipinga ukweli huu zikiwepo NGO's kwa kigezo cha haki za binadamu.

Hakika MAGUFuLI Mungu azidi kukutunza mana unatukumbusha kuenenda katika njia nyembamba iletayo neema, Yafaa nini ukatujengea viwanda vingi vitakavyo shibisha miili yetu alafu ukatutumbukiza taifa kwenye shimo la jehanamu ya moto?

" Basi ndugu zangu, nawasihi kwa huruma zake Mungu , itoeni miili yenu iwe shabihu iliyo hai, takatifu ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana, wala msifuatishe namna ya dunia hii,bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenumpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza na ukamilifu. ( Rum. 12:1-2 )

BARIKiWA RAIS WANGU!
 

ELI-91

JF-Expert Member
Aug 24, 2014
3,591
2,000
Mungu hana time na mambo ya kijinga. Yuko bize kumdhibiti shetani
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom