Magufuli, baada ya kuona hali ya wafungwa na mahabusu; je, unahitaji kuona na salary slip za watumishi ndio uboreshe masilahi yao ikiwemo mishahara?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,371
Hotobua za mawaziri vivuli wa Mambo ya Ndani na yule wa Sheria pamoja na michango ya wabunge wa upinzani na baadhi ya wabunge wa CCM, kila mara imekuwa ikieleza hali mbaya katika magereza yetu ila serikali yako na hata zilizopita sidhani kama zimewahi kufanyia kazi maoni na mawazo ya wabunge hawa na ulichokiona huko Butimba ni matokeo tu ya serikali hizi za CCM kutofanyia kazi ipasavyo ushauri unaotolewa na wabunge Bungeni kwahiyo ulichokiona huko ndio matokeo ya kutofanyia kazi maoni yanayotolewa na wabunge.

Swali nalojiuliza ni kuwa,kama mpaka wewe mwenyewe utembelee magereza ndio hatua zichukuliwe,je utaweza fanya hivyo kwa kila jambo na kwa kila eneo linalolalamikiwa katika nchi hii?

Swali lingine nalojiuliza ni je,labda watumishi wa umma nao wakuonyeshe salary slip zao ndio ujue wana mishahara duni yenye utitiri wa makato labda ndio utachukua hatua za kurekebisha hali hiyo?

Napata shida sana kuelewa haya mambo, au sijui ndio uchaguzi umekaribia, kwakweli sielewi!
 
Back
Top Bottom