Magufuli awavaa JKT na Magereza, ampongeza Meya wa Jiji la Dar

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
RAIS John Magufuli amewataka wananchi na wadau wa maendeleo nchini kuendeleza hamasa, mwamko na nguvu walizozionesha kwenye oparesheni ya upatikanaji wa madawati katika ujenzi wa madarasa.

Aidha, Dk Magufuli amebainisha kuwa pamoja na kuwepo kwa changamoto za uhaba wa madawati, uhaba wa vyumba vya madarasa na vyoo, mfumo mpya wa elimu bure katika shule za msingi na sekondari umeonesha mafanikio hasa katika ongezeko la udahili wa wanafunzi wa darasa la kwanza.

Pamoja na hayo, ameonesha kutoridhishwa na kasi ya utengenezaji wa madawati inayofanywa na majeshi mawili ya Kujenga Taifa (JKT) na Magereza, baada ya vyombo hivyo vya dola kutumia siku 90 kutengeneza madawati 60,000 kati ya 120,000 waliyotakiwa kutengeneza kwa fedha za Bunge.

Rais Magufuli aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati wa hafla ya kukabidhi madawati yaliyotengenezwa kutokana na Sh bilioni sita zilizotolewa na Ofisi ya Bunge baada ya kufanikisha mpango wa kubana matumizi yake na kuamua zitumike kununulia madawati.

Alisema tangu atoe agizo la kila halmashauri kuhakikisha shule zake zina madawati ya kutosha, wananchi, wadau na mashirika mbalimbali ya umma na binafsi vikiwemo vyombo vya habari vimeitikia kwa hamasa oparesheni hiyo na kwa mwamko mkubwa.

Alibainisha kuwa baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kuanza kutekeleza ahadi yake ya kuanzisha mfumo wa elimu bure, idadi ya udahili iliongezeka maradufu ya awali kwa wanafunzi wanaojiunga na darasa la kwanza.

Alisema kuanzia Januari mwaka huu, jumla ya wanafunzi milioni 1.8 sawa na asilimia 84.5 walidahiliwa kujiunga darasa la kwanza tofauti na mwaka jana ambako wanafunzi 128,000 tu ndio waliodahiliwa.

“Hata hivyo, hakuna jambo zuri linalokosa changamoto, kutokana na ongezeko hili la idadi ya wanafunzi, tumekumbwa na tatizo kubwa la uhaba wa madawati, vyumba vya madarasa na vyoo,” alisema.

Alisema tangu mfumo huo uanze, Tanzania ilikabiliwa na upungufu wa madawati milioni 1.4 kati ya hayo shule za msingi pekee zilikuwa na upungufu wa madawati milioni 1.1.

Dk Magufuli alisema kutokana na changamoto hizo, wakati akiwaapisha wakuu wa mikoa Machi mwaka huu, aliwaagiza wakuu wa mikoa na watendaji wengine kuhakikisha wanaanzisha oparesheni katika maeneo ili kila mwanafunzi wa shule ya msingi na sekondari apate dawati.

Alisema kutokana na agizo hilo na uhamasishaji uliofanywa na viongozi mbalimbali wa serikali na vyombo vya habari nchini, wadau mbalimbali walijitokeza zikiwemo kampuni binafsi, mashirika ya umma, wasanii na watu binafsi kuchangia katika oparesheni hiyo.

Alieleza kuwa hadi sasa zaidi ya madawati milioni moja yamepatikana kati ya madawati hayo asilimia 88 ya madawati yanayohitajika yamepelekwa katika shule za msingi na asilimia 95.8 ya madawati yanayohitajika yamepelekwa katika shule za sekondari.

“Kwa maana hiyo kwa shule za msingi kwa sasa tumebakiza asilimia 11.2 tu ya madawati na sekondari asilimia 4.2 ili tufikie lengo la madawati yanayohitajika,” alisisitiza Rais Magufuli.

“Nimefarijika sana kuona Watanzania wote tumeungana kufanikisha oparesheni hii. Hii ndio Tanzania ninayoitaka, na kwa moyo huu tuliouonesha katika suala hili la madawati naomba tukimaliza hapa tuuhamishie kwenye madarasa,” alisisitiza Magufuli.

Aidha, alisema kwa mujibu wa taarifa alizopatiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene, takribani halmashauri 24 zimefikia malengo ya kupata madawati kwa asilimia 100 katika shule za msingi na halmashauri 46 katika shule za sekondari.

Halikadhalika, Dk Magufuli alisema taasisi za Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mfuko wa Pensheni wa PPF na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zilimuahidi na kutangaza hadharani kuwa nazo zitachangia fedha kwa ajili ya kutengenezea madawati, lakini hadi sasa hajakabidhiwa fedha hizo.

“Pamoja na taasisi hizi kutangaza hadharani hasa BoT iliyoahidi kutoa shilingi bilioni nne, hazijanipatia fedha zao ila nikizipata nitazielekeza kwenye madawati,” alisema.

Dk Magufuli pia alipongeza hatua ya wabunge kushirikiana bila kujali itikadi na vyama vyao na kuwa mstari wa mbele katika kufanikisha suala la upatikanaji wa madawati na kusisitiza kuwa ni wakati sasa kwa Watanzania kuweka mbele uzalendo na maslahi ya taifa badala ya vyama vyao.

''Leo unapomuona hapa Dkt. Tulia na Msigwa wamekaa pamoja inatia moyo kweli'' Rais alisema.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na baadhi ya wabunge wa CCM, CHADEMA, CUF na pia Mameya wote wa Dar es Salaam.

“Kwa mwelekeo wa leo (jana) nadiriki kusema Tanzania tumeweka historia mpya. Ndugu zangu Tanzania ni yetu sote na ndio maana hata katika kampeni zangu nilisema tuweke maslahi ya watanzania mbele, tushirikiane bila kujali vyama vyetu kutatua shida za Watanzania,” alisisitiza.

Rais Magufuli alimpongeza Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita (Chadema), kwa kauli zake zenye mlengo wa maendeleo alizokuwa akizitoa katika maeneo mbalimbali. “Kauli zako na dhamira zako ni za kuleta maendeleo kwa watanzania bila kubagua vyama vyao, ila wasije wakakufukuza kwa kuwa nimekusifia. Sina uhakika labda wanaweza kukufukuza kwa sababu nimekusifia. Hata wakikufukuza bado nina nafasi nitakupa kwa sababu unapenda maendeleo,” alieleza.

Alishukuru na kulipongeza Bunge kwa kuamua kwa makusudi kubana matumizi na kukubali fedha walizomkabidhi Rais ziende kwenye madawati.

“Mfano mzuri ni leo hii watoto wetu sasa wanakaa kwenye madawati, ukiwaona huwezi kujua nani baba yake ni Chadema, ACT-Wazalendo wala CCM. Utakachokina wote ni watoto wa Watanzania,” alifafanua.

Akizungumzia kazi ya kutengeneza madawati hayo iliyofanywa na JKT na Magereza, pamoja na kupongeza ubora wa madawati hayo, alibainisha wazi kusikitishwa na kasi ya utengenezwaji wake ambayo haiendani na uharaka wa upatikanaji wa madawati hayo.

Alisema majeshi hayo yalikabidhiwa fedha hizo Sh bilioni sita na Bunge tangu Aprili 11, mwaka huu hadi jana tayari zilishapita siku 90, lakini yameweza kukabidhi madawati 60,000 tu kati ya madawati 120,000 waliyotakiwa kutengeneza.

“JKT ina kambi zaidi ya 10 nchi nzima, na kila kambi kuna kuruta na wale wanaopewa adhabu, inawezekana vipi jeshi hili litengeneze madawati 30,000 kwa siku 90, yaani ina maana lilikuwa linatengeneza madawati 30 kwa siku?” alihoji.

Kuhusu Magereza, alisema pia jeshi hilo limemuangusha kwa kuwa pamoja na kuwepo kwa magereza ya wafungwa katika kila mkoa na wilaya isipokuwa wilaya mpya, pia jeshi hilo limetengeneza madawati 30,000 kwa miezi mitatu kwa maana ya madawati 30 kwa siku.

“Wafungwa wako wengi na wengine hata leo wamefungwa, kila mkoa kuna magereza ukiacha wilayani, na Serikali imekuwa ikitenga fedha za kutosha kwa ajili ya chakula cha wafungwa hawa, kwanini haingii akilini eti wametengeneza madawati 30 tu kwa siku,” alisisitiza.

Aliyataka majeshi hayo kujipanga na kuja na mikakati itakayoyaweza kutengeneza kwa kasi madawati pindi wanapopatiwa zabuni, ili wanapojitokeza wafadhili wengine, majeshi hayo yaendelee kutengeneza madawati hayo.
Chanzo: Habarileo
 
Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita ni kati ya viongozi wachache wa vyama vya upinzani ambao wamekomaa kisiasa na wanafahamu vizuri kuishi katika mazingira ya siasa za Tanzania.

Ni kati ya viongozi wa upinzani wenye hekima na busara ambao wanafahamu vizuri umuhimu wa kushirikiana na serikali katika mazingira ya siasa za Tanzania.

Ni kiongozi ambaye yuko tayari kujishusha ili atimize malengo yake kwa sababu anafahamu katika mazingira ya siasa za Tanzania, bila Meya kushirikiana na serikali hawezi kutimiza ahadi zake kwa ufanisi.
 
Tatizo ni Makonda sasa. Kama rais amemsifia huyo meya tutegemee Bifu kali kutoka kwa makonda!! Mkuu kwani makonda hakusifiwa?
Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita ni kati ya viongozi wachache wa vyama vya upinzani ambao wamekomaa kisiasa na wanafahamu vizuri kuishi katika mazingira ya siasa za Tanzania.

Ni kati ya viongozi wa upinzani wenye hekima na busara ambao wanaofahamu vizuri umuhimu wa kushirikiana na serikali katika mazingira ya siasa za Tanzania.

Ni kiongozi ambaye yuko tayari kujishusha ili atimize malengo yake kwa sababu anafahamu katika mazingira ya siasa za Tanzania, bila Meya kushirikiana na serikali hawezi kutimiza ahadi zake kwa ufanisi.
 
Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita ni kati ya viongozi wachache wa vyama vya upinzani ambao wamekomaa kisiasa na wanafahamu vizuri kuishi katika mazingira ya siasa za Tanzania.

Ni kati ya viongozi wa upinzani wenye hekima na busara ambao wanaofahamu vizuri umuhimu wa kushirikiana na serikali katika mazingira ya siasa za Tanzania.

Ni kiongozi ambaye yuko tayari kujishusha ili atimize malengo yake kwa sababu anafahamu katika mazingira ya siasa za Tanzania, bila Meya kushirikiana na serikali hawezi kutimiza ahadi zake kwa ufanisi.
Basi Magufuli aige mfano wa Meya Jiji la Dar Es Salaam, Isaya Mwita (UKAWA), kwa ukomavu wa Siasa. Aache uoga wa kutumia Polisi kuzima shughuli za vyama vya Upinzani.
 
Jambo Jema..
Kwa maendeleo ya Taifa..
Kiongozi anabudi kushirikiana na watu wote/vyama vyote..Hekma na sio Ubabe..

Hongera Mtukufu Rais na Wadau wote wa maendeleo
 
Wengine watakuja na kuanza ku-discourage hiyo nia ya prezdaa. CC:mmawia.
 
Basi Magufuli aige mfano wa Meya Jiji la Dar Es Salaam, Isaya Mwita (UKAWA), kwa ukomavu wa Siasa. Aache uoga wa kutumia Polisi kuzima shughuli za vyama vya Upinzani.
Kwani wewe una define vipi shughuri za vyama vya siasa?
 
Tatizo ni Makonda sasa. Kama rais amemsifia huyo meya tutegemee Bifu kali kutoka kwa makonda!! Mkuu kwani makonda hakusifiwa?

mtanzania halisi! mzee wa kudhania na kutunga.....najua unadhania pia makonda anaweza

kulala na mama yako?

makonda alimsifia meya pia...

acheni hizo mnadharaulika mno na chuki zenu
 
...
.....
Alieleza kuwa hadi sasa zaidi ya madawati milioni moja yamepatikana kati ya madawati hayo asilimia 88 yamepelekwa katika shule za msingi na asilimia 95.8 shule za sekondari.

.....
Chanzo: Habarileo
uhandishi gani huu? hajawahi kujifunza hesabu ya asilimia kweli?
 
Kwani wewe una define vipi shughuri za vyama vya siasa?
Uhuru wa kidemokrasia wakuikosoa serikali, ambapo JPM kamtumia mteule wake Naibu Spika kuzima hoja za Wapinzani Bungeni. Unajua kilichotokea.

Uhuru na haki ya kikatiba ya kukutana na kufanya Mikutano ya hadhara, ambapo, JPM kutumia Policcm kazuia, eti intelijensia imegundua figisufigisu, wakati Chama Cha Majipu (CCM) kinakutana July 23, PoliCCM waliokataza sasa wapo Dodoma wanafanya gwaride kwa fedha za walipakodi, kulinda Mkutano wa Chama Cha Majipu (CCM)..
Hakika huu ni Ukaburu.... In Nyerere's voice.
 
Tatizo ni Makonda sasa. Kama rais amemsifia huyo meya tutegemee Bifu kali kutoka kwa makonda!! Mkuu kwani makonda hakusifiwa?
Ahadi ya rais kwa meya ni kumpa kazi nyingine aliyonayo,dogo akileta bifu anatolewa yeye,anapewa meya,SASA AACHE KUMBAGUA NA KUWABAGUA MAMEYA,awape viti kwenye mikutano yote ya serikali jijini Dar.
Atambue mkulu anamuona na anatambua uwezo wake na ndiyo maana kila kwenye hafla Anko Magu lazima amuulizie meya,hiyo ni TAADHARI.
 
mtanzania halisi! mzee wa kudhania na kutunga.....najua unadhania pia makonda anaweza

kulala na mama yako?

makonda alimsifia meya pia...

acheni hizo mnadharaulika mno na chuki zenu
Wewe ndiyo unaedharaulika viba sana,mwanamke wa umri wako hawezi kukosa uvumilivu kwa kauli ndogo kiasi hicho hadi wewe umjibu matusi"mama yake anaingiaje hapa",
 
Hata Makonda amemsifia Meya wa Jiji.

Tatizo ni sisi wananchi ambao tunajaribu kutengeneza bifu ambalo halipo. Mihemko ya kisiasa inatupofusha mpaka tunashindwa hata kupanuka kifikra.

Mkuu uko sahihi, sisi wananchi ndio tunazielewa siasa tofauti na kuishia kuwafitinisha wabunge wetu

Laiti kama sisi tutabadilika na kuona positivities katika wanasiasa wetu basi Tanzania itakuwa ya amani na yenye maendeleo
 
Magu anauma na kupuliza. Hana lolote wakati keshajiwekea safu yake ya uchakachuaji. Kwani alishindwa nini kumsifia meya bila kuingilia vyama? Eti akifukuzwa kwa kusifiwa na rais
 
Back
Top Bottom