Ngara, Kagera: Mkutano wa hadhara wa Rais Magufuli na Rais Nkurunziza wa Burundi

kunze

JF-Expert Member
Nov 22, 2016
398
469
Wadau,Umofia kwenu,

Hafla inafanyika viwanja vya Posta ya zamani kwenye wilaya Ngara inayopakana na Rwanda na Burundi.

Asanteni

======

NGARA: Rais Magufuli amewasili katika uwanja wa mpira wa Lemela Wilaya ya Ngara, Kagera ambapo atampokea Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza.

NGARA: Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza amewasili uwanja wa mpira wa Lemela, Ngara, Kagera na kupokewa na Rais Magufuli asubuhi hii.

Rais Magufuli amesema mazungumzo yake na Rais Nkurunziza yamehusu ushirikiano wa biashara na ujenzi wa reli kutoka Dar, Rwanda na Burundi.

Rais Dakta JOHN POMBE MAGUFULI amekutana na Rais PIERRE NKURUNZINZA wa Burundi katika uwanja wa mpira wa Lemela Wilayani Ngara Mkoani Kagera.

Baada ya kuwasili katika uwanja huo Rais NKURUNZINZA amepata mapokezi ya kijeshi ya mkuu wa nchi kwa kupigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride la heshima lililoandaliwa na Jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ na kisha kuangalia vikundi vya ngoma.

Akisalimia wananchi Rais NKURUNZINZA amesema ushirikiano mzuri kati ya nchi yake na Tanzania unaimarishwa kuhakikisha wananchi wanaendesha shughuli zao kwa amani bila hofu ya usalama wao.

Mchana huu Rais MAGUFULI atazungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara Kwenye Viwanja vya Posta ya Zamani Mjini Ngara.

======

Sasa ni Hotuba ya rais katika Viwanja vya Posta ya Zamani Mjini Ngara. Fuatilia hapa chini.

=> Niwaombe na nitoe wito kwa ndugu zangu wa Burundi 150,000, waanze kurudi kwao. Siwafukuzi ila warudi nyumbani.

=> Tunajenga reli; mazungumzo yanaendelea na kila kitu kikikamilika tutaanza ujenzi wa reli

=> Tumesema hizi ushuru ndogo ndogo kwa wakulima tumefuta. Ukisafirisha mzigo wako usiozidi tani moja hutalipa ushuru wowote.

=> Tumefuta kodi saba kwa wananchi wanyonge. Nazungumza hivi ili watendaji wasikie.

=> Tukikuta mtu ametozwa kodi kwa mzigo unaopungua tani moja huyo mkurugenzi na DC watakiona cha mtemakuni.

=> Tumeamua kutoa elimu bure na hii imeongeza hata kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi

=> Tumetenga shilingi bilioni 483 kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wanafunzi watakaofaulu kwenda kusoma elimu ya juu.
Tumeanza kuchukua hatua kwa mafisadi.

=> Waliokuwa wananufaika na mishahara hewa, vyeti feki hewa, kaya hewa na pembejeo hewa na wawekezaji hewa tunalala na nao mbele.

=> Tumetoa vifaa vya maabara kwa shule 1900 na tumevigawa Tanzania nzima

=> Tumeamua kuagiza madawa moja kwa moja nje ili kupunguza gharama ya dawa.

* Mmeniambia kuhusu maji, lakini najua mtu wa maji yuko hapa.

=> Mtu wa maji: Tulinunua pampu mpya na imeanza kufanyakazi tangu tarehe 15/08. Tuna mpango wa kujenga tenki la maji na mota ya maji.

=> Rais Magufuli: Maagizo kwa mkurugenzi wa H/Mashauri: Hizo milioni 200 anza kuziweka kwenye maji kwa ajili ya wananchi badala ya kuwapelekea wanajeshi.

=> Naomba hili mniachie, hili la maji nikifika Dar tutakaa na waziri wa maji tuangalie namna ya kufanya.

=> Na mimi nitaleta milioni 13 za kujenga hiyo moter na ole wao iungue na wao wataungua.

=> Tatizo la Ngara ni mgawanyo wa Bushubi na Bughufi. Niwaombe ndugu zangu wa Ngara na Mbunge; hakikisheni matatizo haya yanaisha, yanatucheleweshea Maendeleo

=> Tumetenga fedha kwa ajili kujenga barabara 92km kutoka Rulenge hadi Nyakahura.

=> Leo najua hamlizungumzii la umeme, ninafahamu umeme haujafika baadhi ya maeneo.Ila REA awamu ya tatu utafika karibu kila sehemu. Ninyi tunachowaomba ni kufanya kazi.

=> Leo nimekuja na mgeni wangu Nkuruzinza na kikubwa ni kuwashukuru. Napenda kuwahakikishia mimi na serikali yangu tushikamane.
Dunia ya leo ni biashara,

=> Kwa haya machache naomba niwashukuru, sijawahi kuona makaribisho mazuri namna hii.

+> Rais anauliza hadhara: Hayo mabango ni ya nini? Bango limeandikwa; "Sisi hapa Ngara tuna upungufu wa ardhi, tunaomba mchango wako vijana tupate ardhi tufanyekazi kama ilivyo kaulimbiu yako ya hapa kazi tuu. Tunaomba tupewe maeneo Kasulu".

=> Majibu(Rais Magufuli): Mh mkuu wa mkoa chukua namba yake na atawakilisha wote wanaohitaji ardhi. Hakikisha wanapata ardhi.

Nawashukuru wananchi, waandishi wa Habari na wanakwaya
Asanteni sana ndugu zangu wa Ngara, Mungu awabariki sana.




Rais Magufuli amhakikishia Rais wa Burundi ushirikiano wa kutosha na amemuahidi kuendelea kushirikiana na Burundi katika kuimarisha maisha ya wananchi wa nchi zote mbili na kuimarisha biashara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo kuna Ziara ya Kikazi ya Rais Pierre Nkurunzinza Nchini Tanzania.

Nkurunziza atakutana na rais Magufuli ambaye yupo ziarani Mkoa wa Kagera.

Baada ya Mazungumzo ya Marais hao, baadae Rais Magufuli atafanya mkutano wa hadhara katika Viwanja vya Posta ya Zamani Mjini Ngara Kagara
 
Habari zenu wanachadema, wanaccm na wengine kama mimi .
Leo ni zamu ya wilaya ya Ngara kupokea ugeni wa marais wawili mmoja kutoka Burundi na mwingine ni mwenyeji.Tafadhali mulioko huko leteni habari!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo kuna Ziara ya Kikazi ya Rais Pierre Nkurunzinza Nchini Tanzania.

Nkurunziza atakutana na rais Magufuli ambaye yupo ziarani Mkoa wa Kagera.

Baada ya Mazungumzo ya Marais hao, baadae Rais Magufuli atafanya mkutano wa hadhara katika Viwanja vya Posta ya Zamani Mjini Ngara Kagara
Mtu na rafiki yake. Like dissolves like!, tabia ya Nkurunzinza ikoje mnao ijua. From there tutajua or we can predict with certainty within 95% confidence interval tabia ya Rafiki.
 
UJIRANI MWEMA;
ILA MSIMAMO, AONDOE NG'OMBE KWENYE MAPOLI YA TANZANIA.
KATUMWA NA WAFUGAJI ??????????????????
 
Leo kuna Ziara ya Kikazi ya Rais Pierre Nkurunzinza Nchini Tanzania.

Nkurunziza atakutana na rais Magufuli ambaye yupo ziarani Mkoa wa Kagera.

Baada ya Mazungumzo ya Marais hao, baadae Rais Magufuli atafanya mkutano wa hadhara katika Viwanja vya Posta ya Zamani Mjini Ngara Kagara
Huyu Nkurunzinza imefikia hatuwa anafanya ziara mithili ya panya na shimo lake?

Yani anategeshea kukutana na Magufuli mpakani ili incase aweze kukimbilia kwao hata kwa bajaj?
 
Nkurunziza anaogopa kukutana na rais dar, hata akipinduliwa iwe raisi kwake kuibukia hapo nchini kwake
 
Mtu na rafiki yake. Like dissolves like!, tabia ya Nkurunzinza ikoje mnao ijua. From there tutajua or we can predict with certainty within 95% confidence interval tabia ya Rafiki.
Hata siku akikutana na Trump mtasema hivyo hivyo...
 
Back
Top Bottom