Magufuli Awasaidie Waliodhulumiwa Kanisa lake na Sumaye Mloganzira Kibamba Tabata

domokaya

JF-Expert Member
Apr 22, 2010
3,475
2,000
Rais John Pombe Magufuli ana wajibu wa kuwasaidia wananchi waliodhulumiwa maeneo yao maeneo ya Mloganzira, Kisopwa na Tondoloni na aliyekuwa waziri Mkuu Frederick Sumaye kwa kivuli cha eneo la jeshi.

Eneo hilo liliporwa kupitia jeshi ili baadae limilikishwe kwa waziri mkuu huyo kwani alifahamu lingekuwa prime area ambapo ndipo chuo cha tiba MUHIMBILI kimehamishiwa.

Wakati huo huo Dr John Pombe Magufuli anawajibika kurudisha kiwanja cha shule ya Msingi Kisukuru kilichoporwa na Kanisa lake mwenyewe analoabudu.

Kiwanja hicho kilichopo katika shule ya msingi Kisukuru kilitolewa na serikali kwa wananchi ili wajenge shule na kukabidhiwa kwao na makamu Wa Rais Hayati Dr Omar Ali Juma.

Miti ilipandwa na mipaka ikawekwa. Kiwanja hicho kikawa kinatumika, milingoti ya magoli na kila kitu chenye kuhitajika katika uwanja Wa shule vilikuwepo.

Ujanja ukafanyika na matokeo take ujenzi Wa Manisa shuleni Kisukuru unaendelea.

Msemakweli Rais JPM sema kweli katika ishu hizi mbili. Ishu wa waliodhulumiwa Mloganzira, Tondoloni, Kisopwa na ishu ya kanisa lako unaloabudu kudhulumu kiwanja cha shule.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom