Magufuli atumia lugha ya Kiswahili kwenye hotuba ya kumkaribisha PM wa India

Rais wako akienda China, Germany je mwenyeji wake atatumia kingereza? Je atatumia Kiswahili? The answer is absolutely NO.China kichina. Germany kijerumani. Watz tuache kujidhalilisha kwa kutukuza lugha za kigeni na kuidharau lugha ya taifa letu. Kiswahili ndo lugha ya taifa. Hivyo Raisi wa taifa hili ana haki na wajibu wa kutumia LUGHA YA TAIFA YA TAIFA HILI KWENYE MATUKIO YOTE YA KITAIFA NA KIMATAIFA. i.e KISWAHILI ONLY.
Pole kwamba hujui kuwa kiingereza pia ni lugha ya Taifa letu.
 
..kama huna vocabularies za kutosha unapoongea kimombo ni bora ukaacha na kutumia kiswahili ulichokua nacho...na hii si aibu wala haikushushi bali ndio uhalisia....kuliko kuongea kimombo cha kuchapia na kujipa aibu bure....
 
Sasa mbona kuna mtu mwingine anaisoma hiyo hotuba Kiingereza tena ilikuwa na maana gani yeye kutumia kiswahili then huyo dada anaisoma kwa Kiingereza yote. Kwa ajili ya interpretation to English.It is wastage of time

Hapana sio kwa kuwa mkalimani yupo raisi asiongee.Wala suala la kupoteza muda halipo kwani muda na matukio yote atakayoyafanya mgeni yamepangiwa muda na ikulu sio na mgeni.Raisi atatoa hotuba kwa lugha atakayoipenda kama alivyokienzi kiswahili na mkalimani ataisoma yote kwa lugha anayoielewa mgeni (kiingereza) na kwa faida ya waalikwa wengine wasioielewa lugha ya raisi yaani kiswahili.Wala msijidanganye eti raisi wa awamu ya tano hafanyi safari za ulaya na kwingineko kwa sababu tu hatatoa hotuba kwa lugha ya kizungu.Anae mkalimani na anaweza kusafiri nae popote.Magufuli kwa wasiomjua ni jasiri sana wala hayo hayamtishi na wapo maraisi wengi wasiotoa hotuba kwa kiingereza.
 
Tuondoe basi kiingereza katika lugha zetu za serikali kibaki kiswahili tu nitaelewa. lkn huku tunasema kiingereza ni lugha yetu pia na tunaotumia kila siku. halafu anakuja mgeni unaanza kumuongelea kiswahili.
Hapana ndugu kiingereza si lugha yetu, lugha lugha yetu ni kiswahili ni mkangamyiko tu wa serikali katika kulisimamia hilo lakin huo ndio ukweli halisi
 
Ww kiswahili ni lugha kubwa sana urimwenguni kwa sasa sio ajabu kutumia lugha yetu mbona wachina wanatumia lugha yao popote wanapo kuwa na mambo kama haya nawanafanya vizur tu kiuchumi tuache kuwa watumwa wa lugha za watu
 
Kama ana vitamkwa tena vya kiswahili shida iko wapi mbona wengine wanakuja nchini hawajui kiingereza still mawasiliano yanawezekana, hebu rejea ziara ya rais wa china alipokuja
 
We mleta mada unapendekeza na kushinikiza rais atumie kiingereza kwa sababu zipi? kwa nini huyo mgeni asitafsiriwe kama ambavyo nchi zingine hufanya? Acha mambo ya kitoto na utumwa usokuwa na msingi....Magu huwa nampinga kwa mengi ila katika hili namuunga mkono 100% eti tulikemee kwa nguvu zote hovyo kabisa!!!
 
Wakuu nimesikitishwa sana na kitendo cha Rais wetu mh. Dr. Pombe kushindwa kutumia lugha iliyozoeleka ya english tunapowakaribisha viongozi wa dunia.

Hii inawanyima mabalozi mbalimbali waliohudhuria mkutano kushindwa kwenda sambamba na mzee wa mwendo kasi kuhusu anachozungumzia.

Ikumbukwe Kikwete alipiga kizungu alipomkaribisha Obama, Mkapa alipiga kizungu akipomkaribisha Clinton na Bush.

Sasa huu utaratibu wa Dr. Pombe kutumia kiswahili kwenye hotuba za kimataifa umeanza lini?

Watanzania tulikemee hili kwa nguvu zote
a03b88d0ed233831bfccd326ba3f93a1.jpg


Ikulu yetu ilinde misingi yake
Nadhani tukukemee wewe ambaye unaendeleza utumwa kwenye nchi iliyo pata uhuru wake toka mwaka 1961,Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania atatumia kiswahili,kama inakuuma hama nchi.
 
Nimeguswa sana na Mheshimiwa Rais kutumia kiswahili maana nilikuwa napata shida sana kuona tunang'ang'ania kuongea lugha isiyokuwa yetu na kuiacha lugha yetu adhimu ya Kiswahili.
 
Kama kubadilika na kukataa utumwa tuanzie kwenye elimu yetu kibaki tu kiswahili na hata tunapotaka kazi basi tuhojiwe kiswahili. kabla ya hapo Rais anatakiwa atumie kiingereza kama mgeni anayekuja hajui kiswahili.
Hivi unafikiri marais wote duniani wanajua kiingereza!
Sio lazima kabisa. Rais anaweza kutumia kiswahili vizuiri kabisa kama Rais wa urusi anavyotumia kirusi akihutubia UN n.k au kukaribisha mgeni. Marasi wanakuwa na wakalimani wao wanaotembea nao.
Kwahiyo ndugu, usije ukafikiri kiingereza ni big deal. Ni lugha kama kisukuma tu. Ila umuhimu wake ni kwasababu inazungumzwa sehemu kubwa duniani.
 
Atumie lugha yetu tu wala sio ishu,shida kunawatu wanajikomba sana kwenye uzungu.kama mnakipenda sana kiinglish kamsikilizeni Kameruni na Obama nahoja zao za kutetea uliwaji maboga.
Tutasoma kutumia kingreza lakini tutatumia lugha yetu kadri inavyowezekana na hatutakionea haya kiswahili kwa maneno ya mabeberwa
 
..kama huna vocabularies za kutosha unapoongea kimombo ni bora ukaacha na kutumia kiswahili ulichokua nacho...na hii si aibu wala haikushushi bali ndio uhaliusia....kuliko kuongea kimombo cha kuchapia na kujipa aibu bure....

Mkuu:
Lakini Kiongozi wetu ana shahada ya uzamivu (PhD) na aliipata kwa lugha ya kingereza. Sasa alijielezaje wakati wa kutetea tasnifu (Dissertations) zake. Je ni kweli yeye ni mufilis wa vocabularies?
Vinginevyo hata kwenye hilo jopo (panel) alilowasilisha tasnifu zake kuna tatizo.
 
Hakuna kosa alilofanya. Amesema wazi kuwa ametumia kiswahili kukienzi ila hotuba yake itasomwa kwa kiingereza na inasomwa sasa. Jamani tusipinge kila kitu
Hawakujipanga. Kutumia kiswahili ni vizuri sana (tena sana), lakini walipaswa kujipanga kwa kuandaa mkalimani ili wasikilizaji walioohudhuria waende sambamba nae...pa kucheka, wacheke! Sasa hii ya kusomewa hotuba baada ya mzungumzaji (Mh Rais) kumaliza, mimi binafsi limenipa tabu kidogo na kwa kweli linapoteza muda na ladha ya hotuba yake (ambayo ilikuwa nzuri tu!).

Matukio kama haya yanatutia aibu kimataifa.....tukichanganya na haya ya kukosea teuzi za za ma DC etc. , kwa kweli inabidi wajitizame upya na kujipanga vizuri zaidi kwa sababu ni mambo ya aibu kufanywa na watu waliostarabika kama sisi watanzania.
 
Back
Top Bottom