Magufuli atuma salamu kwa Kikwete na CCM

mkuu kwenye wekundu hapo ni kweli maneno yhayo yametamkwa na ndg. Idd azzan au unamuwekea maneno kinywani?
hii ameitengeneza yeye, labda angesema kuwa jk anadhalaulika na watumishi wa serikali!
 
Unajua akuna siasa mbaya kama za utapeli rais kikwete amekuwa akidanganya wananchi
sasa naona kunamengine anadanganya akijua yuko vijijini kumbe yuko mjini na watu wanamsubir
ahadi zake

kwa mnaokumbuka kuna upuuzi mmoja amechukua kiwanja cha jangwani nampaka leo hii ajabomoa
kama agizo la rais kikwete lakini mpaaka leo hii amekuwa kimya akipita juu angani kama anatafuta
sayari nyingine ..kwa upande wa magufuli pamoja na mapungufu yake jamani huyu bana akikomaa
sijui huko kwake mkewe anaisikiliziaje amri zake..akisema kesho siuitaji huu ukuta wanabomoa usiku
sasa nimeka nikajiuliza kuna haja ganai ya kuwa na rais hewa asiesikilizwa ama anashiriki kwenye
huo mgao wa jangwani anajifanya kutufanya wapumbavu watanzania

tanzania tuamke ni wakati wa kurudisha mali zetu zote walioiba huku mjini kumejaa watu wa nchi mbalimbali
wamekalia magorofa ambayo mimi na wewe tulipaswa kuyapangisha lakini kwa kuwa wana hela ya kuhonga
nhc leo hii mi na wewe tunaishi buza na bonyokwa

watanzania tuamke
 
hii ameitengeneza yeye, labda angesema kuwa jk anadhalaulika na watumishi wa serikali!
hata kama hajasema maneno hayo moja kwa moja lakini halii inavyojionyesha ni kuwa jamaa ni lege lege ..kwa nini kauli zake hazifanyiwi kazi?
 
Mkuu huyu Idd Azzan ni miongoni mwa watu waliokuwa wakilalamika kwamba kuna mtu amejinyakulia kiwanja jangwani kumbe ni kituo cha mradi wa mabasi yaendayo kasi. Idd Azzan ana maslahi na kiwanja hicho kwa kuwa team ya Villa Squad ambayo Idd ana maslahi ndani yake ilikuwa ikitumia sehemu hiyo kufanya mazoezi!
 
KAULI ya Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, kuwa kwa vyovyote iwavyo lazima abomoe mabango yote ya biashara barabarani akisema kuwa hakuna wa kumzuia kuyaondoa kwa kuwa anatekeleza sheria za nchi, imetuma ujumbe mzito kwa wakubwa wake wa kazi.

Miongoni mwa viongozi walioguswa na kauli hiyo ya Magufuli ni Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambao kwa wakati tofauti walimkemea waziri huyo, wakimzuia kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria, kwa masilahi ya kisiasa.

Alipomtembelea wizarani kwake wiki chache zilizopita, Rais Kikwete alimwambia Magufuli, “acha ubabe.” Kabla ya hapo, Pinda alimfokeza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Jimbo la Chato, linalowakilishwa na Magufuli, akimtaka asitishe bomoabomoa mara moja.

Hata juzi wakati akifungua semina elekezi mjini Dodoma, Rais Kikwete alikemea tabia ya ubabe wa mawaziri na kauli za kupingana wenyewe kwa wenyewe kupitia kwenye vyombo vya habari.

Lakini katika wiki hii pekee, Magufuli ametoa kauli zinazoonyesha hayuko tayari kusitisha ubabe wake wala bomoabomoa, kazi ambayo amekuwa akiifanya kwa kuzingatia sheria zilizopo.

Source: Tanzania Daima

Hawa hawanijui ngoja..........anafikiri nji hii ni yake peke yake............

KATUNI(441).jpg

Hivi keshaacha UBABE ama waliamua kumwachia JUMBA BOVU.....
 
Mheshimiwa Magufuli, wenzako wanazingatia maslahi binafsi katika utendaji wao, ambapo wewe unaangalia maslahi ya taifa na vizazi vijavyo, na hivyo usishangae unapopingwa hadharani. Ukweli wako na uwazi wako unaogopwa nao kwa ndio maana hawakuiti ofisini mkaongea yaishe walivyozoea, we kaza kamba, hadi kieleweke. Umeona mwenzako Tibaigana alivyoburuzwa kutetea haki, na sasa naona kishafyata mkia maana sioni tena cheche zile. We usikubali, kaza kamba hadi kieleweke.

Tunaujua utendaji wako na moyo wako wa kujenga taifa, usisite milango iko wazi kupokewa na wapinzako kwa vile unaakisi kila wetu tunaotea. Miaka miwili ijayo tutakuwa na hadithi zaidi za kusimuliana.

Huyu jamaa namkubali sana.
Ndo waziri pekee aliyekwisha onyesha msimamo wa waziwazi dhidi ya rais na waziri mkuu katika kusimamia sheria na yale anayoyaamini.
Wengine wametusainisha mikataba mibovu kwa hofu ya simu za "mamlaka ya juu".

Msimamo wake dhidi ya jengo la Tanesco dhidi ya bomoa bomoa ya kimara pia ni ya kupigiwa mfano. Hakumung'unya maneno wala nini.

CCM huko waliko wanamwogopa huyu bwana kuliko wanavyoigopa Ukawa.

Kama kuna mtu mwenye uthubutu wa kuipindua system na wale mabilionea wanaoishikilia ni huyu jamaa.

Uthubutu wake na msimamo ni wa hatari. Alimshikia bango Bakhresa wakati ule dah...
Hakuna cha boss, tajiri, mwana ccm, ukawa...akikunyooshea rula kanyoosha.

Kwa hilo nampa pongezi.
Lowassa hana rekodi ya ujasiri, uthubutu na maamuzi magumu kama huyu bwana. Kumpinga rais na waziri mkuu hadharani inataka ubavu wa hatari.
 
daaah..!!mungu amsaidie ashike hii nchi
 
namsikitikia sana kwa kuwa nia anayo lakini uwezo wa kiutekelezaji hataupata maana hataweza kuufumua mfumo wa kulindana ambao umeota mizizi ndani ya ccm.amuulize kikwete kwa nini alishindwa kutimiza kwa vitendo kauli yake ya "urais wangu hauna ubia na mtu".na mwenyekiti wa chama chake si atakuwa huyu huyu? masikini john pombe magufuli! pooole!
 
Eti jamaa anasema jamaa anamsimamo sasa angetoa mabango barabaran leo picha zake za kugombea kaziweka wapi??
 
KAULI ya Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, kuwa kwa vyovyote iwavyo lazima abomoe mabango yote ya biashara barabarani akisema kuwa hakuna wa kumzuia kuyaondoa kwa kuwa anatekeleza sheria za nchi, imetuma ujumbe mzito kwa wakubwa wake wa kazi.

Miongoni mwa viongozi walioguswa na kauli hiyo ya Magufuli ni Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambao kwa wakati tofauti walimkemea waziri huyo, wakimzuia kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria, kwa masilahi ya kisiasa.

Alipomtembelea wizarani kwake wiki chache zilizopita, Rais Kikwete alimwambia Magufuli, “acha ubabe.” Kabla ya hapo, Pinda alimfokeza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Jimbo la Chato, linalowakilishwa na Magufuli, akimtaka asitishe bomoabomoa mara moja.

Hata juzi wakati akifungua semina elekezi mjini Dodoma, Rais Kikwete alikemea tabia ya ubabe wa mawaziri na kauli za kupingana wenyewe kwa wenyewe kupitia kwenye vyombo vya habari.

Lakini katika wiki hii pekee, Magufuli ametoa kauli zinazoonyesha hayuko tayari kusitisha ubabe wake wala bomoabomoa, kazi ambayo amekuwa akiifanya kwa kuzingatia sheria zilizopo.

Source: Tanzania Daima

Kwa huyu jamaa lazima wataisoma number.
 
yani anauza nyumba za serikali alaf nyumba2 anampa girfriend wake? Leo hii tumpe ikulu c atatumaliza huyu'
 
Hizo nyumba Lowasa na Sumaye wamejigawia nyingi, waambie waongelee hoja hiyo ya kurudisha nyumba majukwaani uone watakwambia nini! by the way Jambo hilo liliridhiwa na baraza la mawaziri na Hao mafisadi walikuwamo na mmoja alikuwa waziri mkuu! acha kuropoka usichojua utawaaibisha akina Lowasa na Sumaye.
 
KAULI ya Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, kuwa kwa vyovyote iwavyo lazima abomoe mabango yote ya biashara barabarani akisema kuwa hakuna wa kumzuia kuyaondoa kwa kuwa anatekeleza sheria za nchi, imetuma ujumbe mzito kwa wakubwa wake wa kazi.

Miongoni mwa viongozi walioguswa na kauli hiyo ya Magufuli ni Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambao kwa wakati tofauti walimkemea waziri huyo, wakimzuia kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria, kwa masilahi ya kisiasa.

Alipomtembelea wizarani kwake wiki chache zilizopita, Rais Kikwete alimwambia Magufuli, “acha ubabe.” Kabla ya hapo, Pinda alimfokeza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Jimbo la Chato, linalowakilishwa na Magufuli, akimtaka asitishe bomoabomoa mara moja.

Hata juzi wakati akifungua semina elekezi mjini Dodoma, Rais Kikwete alikemea tabia ya ubabe wa mawaziri na kauli za kupingana wenyewe kwa wenyewe kupitia kwenye vyombo vya habari.

Lakini katika wiki hii pekee, Magufuli ametoa kauli zinazoonyesha hayuko tayari kusitisha ubabe wake wala bomoabomoa, kazi ambayo amekuwa akiifanya kwa kuzingatia sheria zilizopo.

Source: Tanzania Daima

Na huyu ndie Rais wetu
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom