Magufuli atuma salamu kwa Kikwete na CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magufuli atuma salamu kwa Kikwete na CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, May 12, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  May 12, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  KAULI ya Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, kuwa kwa vyovyote iwavyo lazima abomoe mabango yote ya biashara barabarani akisema kuwa hakuna wa kumzuia kuyaondoa kwa kuwa anatekeleza sheria za nchi, imetuma ujumbe mzito kwa wakubwa wake wa kazi.

  Miongoni mwa viongozi walioguswa na kauli hiyo ya Magufuli ni Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambao kwa wakati tofauti walimkemea waziri huyo, wakimzuia kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria, kwa masilahi ya kisiasa.

  Alipomtembelea wizarani kwake wiki chache zilizopita, Rais Kikwete alimwambia Magufuli, "acha ubabe." Kabla ya hapo, Pinda alimfokeza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Jimbo la Chato, linalowakilishwa na Magufuli, akimtaka asitishe bomoabomoa mara moja.

  Hata juzi wakati akifungua semina elekezi mjini Dodoma, Rais Kikwete alikemea tabia ya ubabe wa mawaziri na kauli za kupingana wenyewe kwa wenyewe kupitia kwenye vyombo vya habari.

  Lakini katika wiki hii pekee, Magufuli ametoa kauli zinazoonyesha hayuko tayari kusitisha ubabe wake wala bomoabomoa, kazi ambayo amekuwa akiifanya kwa kuzingatia sheria zilizopo.

  Source: Tanzania Daima
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  May 12, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mheshimiwa Magufuli, wenzako wanazingatia maslahi binafsi katika utendaji wao, ambapo wewe unaangalia maslahi ya taifa na vizazi vijavyo, na hivyo usishangae unapopingwa hadharani. Ukweli wako na uwazi wako unaogopwa nao kwa ndio maana hawakuiti ofisini mkaongea yaishe walivyozoea, we kaza kamba, hadi kieleweke. Umeona mwenzako Tibaigana alivyoburuzwa kutetea haki, na sasa naona kishafyata mkia maana sioni tena cheche zile. We usikubali, kaza kamba hadi kieleweke.

  Tunaujua utendaji wako na moyo wako wa kujenga taifa, usisite milango iko wazi kupokewa na wapinzako kwa vile unaakisi kila wetu tunaotea. Miaka miwili ijayo tutakuwa na hadithi zaidi za kusimuliana.
   
 3. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #3
  May 12, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Mti ulio na matunda ndio hupigwa mawe, hii habari imekaa kiuchonganishi na wabahatishaji wa uraisi 2012 wanadhani Magufuli ni tishio. Hizi mbinu za kuwachafua potential candidates ilitumika sana mwaka 2005 na matokeo yake tumeyaona.

  Mwacheni MAgufuli afanye kazi!
   
 4. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #4
  May 12, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,058
  Likes Received: 3,085
  Trophy Points: 280
  J.k hawezi kumvumilia mtu anayeonekana kumchalenji,tusubiri tuone atafanyaje...ila huyu Magufuri nahisi ataadhibiwa,tusubiri tuone aina ya adhabu na impact yake kwa chama na jamii ya Tanzania
   
 5. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #5
  May 12, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,934
  Likes Received: 12,196
  Trophy Points: 280
  Hawa hawanijui ngoja..........anafikiri nji hii ni yake peke yake............

  [​IMG]
   
 6. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #6
  May 12, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Hahaha, hii imetulia.
  Unajua mabango yale ni ya mafisadi, na wanaompiga vita kila kukicha
   
 7. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #7
  May 12, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Kwanini wabomoe? kwani wakati yanajengwa walikuwa hawaoni? si serikali hiyo hiyo inawatoza hao wenye mabango kutegemeana na ukubwa?

  kubomoa ni uonevu
   
 8. E. J. Magarinza

  E. J. Magarinza Member

  #8
  May 12, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kuadadadekiiiiiiii........................................
   
 9. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #9
  May 12, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,375
  Likes Received: 3,138
  Trophy Points: 280
  Hii nio ccm ya sisi wamangimeza tuliochoak kufikiri na kwetu sisi ccm sheria baadaye na maslahi yetu kwanza ndiyo maana kuna watu wengi hapa tz wapo juu ya sheria na hatuna uwezo wa kuwafanya chochote....watu km rostam,lowasa,chenge,hosea wapo juu ya sheria na sisi ccm tunamchukia sana anayekuwa tofauti nasi
   
 10. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #10
  May 12, 2011
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Kuna kitu ambacho sikielewi kwenye hili zoezi zima la kubomoa mabango. Tatizo la haya mabango nini? Kwamba yamejengwa kwenye hifadhi ya barabara? Kama barabara inapanuliwa, inabidi yang'olewe lakini kama barabara haipanuliwi kwa wakati huu kwanini yaondolewe? Mbona mabango yako kila nchi? Au yeye anataka yawekwe wapi? Natafuta kujua tu!!!!

  Tiba
   
 11. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #11
  May 12, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,934
  Likes Received: 12,196
  Trophy Points: 280
  It is just a common sense barabara itapanuliwaje kama hayatabomolewa.
   
 12. T

  The Priest JF-Expert Member

  #12
  May 12, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 1,026
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  mkuu hapo inshu ni sheria inasemaje,na si mabango yanaaffect nini!kwan wao wakati wanatunga hiyo sheria walifikiria nini,sasa wanajikontradikt wao kwa wao,Magufuli bomoa kabisa.
   
 13. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #13
  May 12, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,396
  Likes Received: 423
  Trophy Points: 180
  Samahani Mkuu naomba kuuliza, hivi 2012 kutakuwa na mabadiliko ya Rais? Mimi nafikiri ungejibu hoja iliyoletwa badala ya kubashiri kile ambacho mleta habari hata hajakisema.

  Hoja: Je, Magufuli yuko sahihi kufanya kazi kwa kuzingatia sheria ambazo kwazo aliapa? Au alipaswa kufanya kazi kwa kuzingatia utu wakati sheria hazizingatii utu! Na kama suala ni utu, kwanini basi msizibadili/msizirekebishe sheria husika ili kuingiza elements za utu badala ya kumzodoa mtu anayefanya kazi? Hivi sisi Watanzania tumerogwa au tuna tatizo gani la kuzaliwa (natural problem)?
   
 14. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #14
  May 12, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Kinacho nishangaza ni pale ambapo mtu anaye fanya kazi kwa bidii huwa hatakiwi ktk siasa za tanzania kama Sokoine na sasa magufuri mda si mrefu chochote cha weza tokea tusubiri tuone.

  Kwa upande wangu namkubali jamaa na naomba upambane hadi dakika za mwisho kama hawakutaki wakutoe ni bora ijulikane umetoka kwa kuteleza sheria kuliko kutoka kwa ufisadi
   
 15. mkokoteni

  mkokoteni Member

  #15
  May 12, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 48
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 15
  Magufuli kosa lake ni kuwa muelekeo wake ni tofauti na walio wengi ndani ya hii serikali ya magamba.
  tusuburi, muda si muda ataundiwa zengwe!
   
 16. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #16
  May 12, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Harafu wadau hebu iangalieni hiii imekaaji ni haki kweli kulipiza kisasi kwa mtindo huuuuu?

  " Wananchi wa Kijiji cha Lusaka walilalamika mbele ya wabunge hao kwamba Serikali imekuwa ikiwanyanyasa na kibaya zaidi imefunga Shule ya Sekondari ya Kijiji hicho baada ya wananchi wa eneo hilo kumchagua Diwani wa Chadema."
   
 17. Nico1

  Nico1 JF-Expert Member

  #17
  May 12, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 60
  kiongozi anafanya kazi chini ya sheria ,kama sheria inamruhusu kufanya hivyo kwani kuna
  tatizo gani?unafiki tu hakuna lolote Tz mvunja sheria ndio shujaa,alafu sasa maguli ana azina kwa watz
   
 18. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #18
  May 12, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Wewe magufuli ni Dr wa ukweli. Huyo dk wa matamasha asikuzingue. Fanya kazi tuone kama atakuzingua
   
 19. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #19
  May 12, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Magufuli ni mtu ambae hawezi kufanya kazi na kundi la Kikwete kwani wao ni wasanii na populists; sasa mwenzao Magufuli is driven by results na ndio maana aliweza kusimamia ujenzi wa barabara nyingi enzi za Mkapa. Pinda is no match to Magufuli kwa vigezo vyote kwahiyo anaona kama anamfunika; hivyo watafanya kila hila to frustrate him na mwishowe atawaachia uwaziri wao wabakie na wakina Kawambwa!! .Kikwete should be thankful to Magufuli kwani ni mmoja kati ya mawaziri wachache wanaowajibika vilivyo. Kama hamtaki sheria zifuatwe kwanini mnazitunga? Juzi Kikwete aliwaambia wafuate sheria wanapotimiza wajibu wao ,halafu Magufuli anapotimiza wajibu wake kwa kufuata sheria , Kikwete huyo huyo anamwita mbabe ; what a contradiction!
   
 20. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #20
  May 12, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mabango mengi yamewekwa barabarani kinyume cha utaratibu na yanazuia vison ya madereva. Suala upanuaji wa barabara tu ila pia kuzuia vision ya incoming and outgoing traffic. Kuna distance inayotakiwa kuweka mango barabarani, si kila mmoja anajiwekea anavyoona bila kuangalia athari kwa taraffic.
   
Loading...