Elections 2010 Magufuli atoa rushwa kuisaidia CCM Igunga

Mulangila Mukuru

JF-Expert Member
Feb 24, 2010
1,945
724
Leo taarifa ya habari ya ITV imemuonyesha waziri Magufuli akitoa ahadi kibao za ujenzi wa madaraja na makalvati huko igunga akiwa pamoja na naibu waziri wa maji ambaye naye katoa ahadi zake ,
Hivi jamani hawa watu wameenda kama makada wa magamba au mawaziri wa serikali? na kama wameenda kama makda wa CCM je hii si rushwa ya Mchana kweupe?
 
wamezidiwa wameona njia pekee ni kutumia viongozi wa kiserikali ili watoe ahadi wakipata wanachotaka kwaheri mpaka 2015
 
ndo walivyo hao,wakiulizwa watasema wanatimiza ahadi za ilani ya chama
 
Hiyo ni rushwa laivu lakini kwa kuwa Tume ya uchaguzi ni ya magamba,Takukuru ni ya magamba,polisi nayo ni ya magamba basi tutkomaa nao hivyo hivyo na ndo maana tunasema People's Power.bila nguvu ya umma hatuwezi kujikomboa kamwe.
Walikuwa wapi kuyasema hayo kabla ya uchaguzi mdogo,Wasira anaesema atawapa maji kutoka ziwa victoria,Magufuli ameapa kwa jina la mungu kujenga daraja,kisha waseme CCM-Magmba imewajengea daraja wakati hilo lilikuwa tatizo la muda mrefu iweje waje waseme wanalitatua leo.Jimbo la Kishapu kuna barabara inayoanzia kishapu penyewe ilianza kujengwa tangu miaka ya 1981 hivi ni umbali wa maili kumi na saba hadi ishirini haijaisha hadi leo sijui inaendelea kujengwa au ndo ilishasahaulika,lakini leo Mh Nchambi mwenye asili ya kiarabu akijivua gamba na kuitishwa uchaguzi watakwenda na kusema barabara itajengwa,hawa ni waongo,sanaa tupu mpaka wabanwe mbavu ndo waanze kuapa mbele ya wananchi kuwajengea madaraja na kuwapa maji.wanapumlia mashine huko Igunga pamoja na ahadi zao zote.
Hiyo kiukweli ni rushwa laivu hakuna cha kutekeleza sera wala ilani.
 
ndo walivyo hao,wakiulizwa watasema wanatimiza ahadi za ilani ya chama
Hiyo ni rushwa ya wazi wazi kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi, maana IIlani ya uchaguzi iliandikwa mwaka jana na kimsingi si lazima waseme mawaziri wa ujenzi kuhusu ujenzi wa barabara ama Maji kuhusu kuwapa maji wananchi.
 
huo ni uvunjaji wa sheria ya maadili ya uchaguzi.
sio tishio sana lakini, hawa tumewazoea. Naamini kwa mtanzania yeyote aliyeamka baada ya kazi nguu ya CDM, wanaharakati wa haki za binadamu na demokrasia, pamoja au mtanzania aliyeamka baada ya kupugika sawasawa kwa kipindi chote cha utawala wa CCM, hawezi kuichagua tena,

anayeichagua ccm ni yule asiyejua alipo.........yupo yupo tu!! tia maji tia maji.
 
rafu za ccm igunga zinaeneza chuki dhidi yake nchi nzima. wanapika kikiiva ccm wanapakuliwa wote.
 
Yuko wapi ritz aka mwita25 aka rejao, kishongo aka philanderer atetee matumbo?
 
Hivi si huyu jamaa alimfanyia makaratee kimada wake akanunua nyumba ya serikali kwa bei ya bure pale Ubungo darajani?
 
WaTanzania bado tunasafari ndefusana kupata democrasia ya kweli dawa ya Ccm ni kuwapiga chini 2 no more
 
hivi huko ni kuwachezea watanzania na wanaigunga leo bajeti gani utaitoa wakati miradi mingi imekwama kwa kukosa pesa udanganyifu kweupe na kuapa haki ya mungu wewe magufuli mungu gani huyo wakati ofisi hazina pesa ukapate za daraja la miaka hamsini,hatwapi kula ccm na apa labda muibe
bado mmekuwa na tabia karibu na taarfa za habari jioni mnazima umeme hadi muda ukiisha mnarudisha tutajua tu kilichotokea simu zipo zimeni na mitandao na sasa shirika la tanesco linaenda kulipa mafisadi mmmmmmh
 
Leo taarifa ya habari ya ITV imemuonyesha waziri Magufuli akitoa ahadi kibao za ujenzi wa madaraja na makalvati huko igunga akiwa pamoja na naibu waziri wa maji ambaye naye katoa ahadi zake ,
Hivi jamani hawa watu wameenda kama makada wa magamba au mawaziri wa serikali? na kama wameenda kama makda wa CCM je hii si rushwa ya Mchana kweupe?

Chadema na CUF wasiokuwa na serikali hawataweza kukifanya walichofanya CCM kupitia mawaziri wa serikali

hii sio haki kwa mchakato wa kampeni unaotakiwa kuwa na uwanja sawa wa ushindani kati ya chama kilichopo madarakani na vile vya upinzani
 
hivi huko ni kuwachezea watanzania na wanaigunga leo bajeti gani utaitoa wakati miradi mingi imekwama kwa kukosa pesa udanganyifu kweupe na kuapa haki ya mungu wewe magufuli mungu gani huyo wakati ofisi hazina pesa ukapate za daraja la miaka hamsini,hatwapi kula ccm na apa labda muibe
bado mmekuwa na tabia karibu na taarfa za habari jioni mnazima umeme hadi muda ukiisha mnarudisha tutajua tu kilichotokea simu zipo zimeni na mitandao na sasa shirika la tanesco linaenda kulipa mafisadi mmmmmmh
Ni kweli mkuu, wanaigunga wakawaulize watu wa jimbo la Busanda, magufuli huyohuyo aliwadanganya wakimchagua Bukwimba vibarabara vyao vyote vitawekwa Lami, hadi leo vumbi kama kawa
 
mi nafikiri anaigunga wangemwuliza huyo waziri wa magamba alikuwa wapi miaka yote?kwanini hakujenga hilo daraja?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom