Uchaguzi 2020 Magufuli ataweza himili joto hili hapo Oktoba?

Miaka 5 yote ya kupiga kampeni mwenyewe bado hajiamini na mwoga mno.

Joto la mwaka huu tofauti na ilivyotarajiwa litakuwa kali sana huku hoja nzito nzito kutoka upinzani zikitamalaki huku JPM asijue cha kufanya!!
Aisee . . . yaani uchaguzi wa mwaka huu kuna uwezekano watu wakatafutana maana hizo hoja za SGR, STIGLERS, makinikia, ATCL na nyinginezo hazitakuwa za mchezo
 
Nguvu ya Dola nayo huwa ina mwisho wake. Ni nchi kibao zilikuwa na watawala maharamia wanaotawala kwa mkono wa chuma lakini siku ilipofika Vyombo Vya Dola vilisalimu amri. Nguvu ya umma usicheze nayo. Hata mimi siombei itokee hapa kwetu kwani madhara yake ni makubwa na nchi kuja kurudi tena kwenye mstari inachukuwa muda sana. Kuna wengi (hata mimi) huwa tunaona kama watanzania ni waoga wana na hawawezi kufanya fujo lakini historia inaonyesha watu wa aina hiyo ni wabaya sana na wanalipulika kama moto wa petrol mpaka kila mtu anashangaa.
Nikweli nguvu ya umma siyo mchezo hata hao polisi ni binadamu km siye inawezekana wanaathirika zaidi kuliko wengine muda utakapofika itawezekana tu 'it is never too late in life'
 
Atapata upinzani ndani ya CCM na kutoka kwa wapinzani.

Kachero katangulizwa tu lakini kuna kundi la watu wa maana wanagugumia chinichini kwa maumivu na sehem pekee ya kupunguzia machungu ni October 2020. Kundi hilo lipo nyuma ya Kachero wakiwemo watu wa mikakati ya ushindi kuanzia wa halali hadi wa goli la mkono.

Hivi Nape yuko wapi
 
Ndg utashangaa jinsi uchaguzi utakavyokuwa mwepei kama karatasi nimesoma hapo juu polisi wanataka majina ya wagombea wote wa cdm unafikiri ni kwa sababu gani? Kuna uwezekano wagombea wengi wakashindwa kugombea kwa ajili ya kesi au sheria ikawa kwenye jukwaa ukizungumzia miradi una kesi
Katika chaguzi zenye joto kali na la namna yake ni huu wa 2020!!

Kitakachopandisha joto zaidi ni aina ya mgombea anaetetea kiti chake kupitia CCM yaani John Pombe Magufuli.

Sipati picha combination ya Membe, Lissu, Mbowe, Nyalandu and the like mbele ya JPM.

Tunaomjua JPM ni mtu asiyeziweza hoja wala upinzani. JPM ni mtu mwoga na DHAIFU sana asiye na subira wala utulivu.

Miaka 5 yote ya kupiga kampeni mwenyewe bado hajiamini na mwoga mno.

Joto la mwaka huu tofauti na ilivyotarajiwa litakuwa kali sana huku hoja nzito nzito kutoka upinzani zikitamalaki huku JPM asijue cha kufanya!!

Hoja ya makinikia, wizi wa trillion 1.5, manunuzi ya kifisadi ya ndege, kivuko kibovu, nyumba za serikali kwa mahawara... Stigla na SGR vitatawala majukwaani huku akina Zitto wakijaribu kuwaelewesha watu ni kwa namna gani JPM kupitia ATCL amewalisha watanzania mzigo mzito wa hasara isiyobebeka!

Mbele ya hoja nzito Magufuli ni mwepesi kama karatasi!
 
Aisee . . . yaani uchaguzi wa mwaka huu kuna uwezekano watu wakatafutana maana hizo hoja za SGR, STIGLERS, makinikia, ATCL na nyinginezo hazitakuwa za mchezo
Kila mgombea atatupia hizp hizo. Yaani Mbunge wa Kilolo huko iringa ubamuuliza Mh umefanya nini kwenye jimbo lako, anajibu Mh magufuli amejnga Flyover😆😆😆😆
 
Asante sana kwa ukweli huu ambao watanzania wanapaswa kuujua. Tutashuhudia Lissu akinyimwa kugombea na akiwekwa ndani, na hili litazua makubwa nchi hii.

Kwa vyovyote uchaguzi utakuwa mgumu kwa JPM kuliko watu wanavyofikiria. Najua haki haitatendeka na chochote kinaweza kutokea. Tuunge mkono juhudi za kuleta demokrasia na maendeleo ya watu sio vitu.
Upinzani wa Tanzania ni kupinga ukweli na siyo kupinga yasiyofaa.

Kwa hali ya siasa ilivyo Tanzania hata vyama vyoooote vya upinzani vikiungana havitamshinda JPM.

Chukulia mfano huu rahisi kabisa. Kwa uchaguzi mkuu wa mwaka2015 ilikuwa ni aibu sana kumuona kinana akiishabikia CCM lakini sasa vijana wengi ni wapenzi wakubwa wa CCM.

Si hivyo tu lakini pia kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ilikuwa ni aibu sana kupita mtaani ukiwa umevaa vazi la CCM lakini kwa sasa vazi la CCM ni dili hata ukipita madukani ndiyo linalouzwa sana zaidi ya mavazi mengine ya vyama vingine.

Kwa hiyo uchaguzi wa mwaka huu ni laini sana kwa JPM zaidi ya uchaguzi wa mwaka 2015
 
IMG_20200716_173621.jpg
 
Tatizo ni lazima waibe kura, ata iweje CCM atapita,, niliamini kwa asilimia kubwa sana CCM itaondoka madarakani 2015 wakat wa Rowassa lakin haikuwa ivyo. i m disappointed kwakwel
 
Asante sana kwa ukweli huu ambao watanzania wanapaswa kuujua. Tutashuhudia Lissu akinyimwa kugombea na akiwekwa ndani, na hili litazua makubwa nchi hii.

Kwa vyovyote uchaguzi utakuwa mgumu kwa JPM kuliko watu wanavyofikiria. Najua haki haitatendeka na chochote kinaweza kutokea. Tuunge mkono juhudi za kuleta demokrasia na maendeleo ya watu sio vitu.
Si angeamua kupumzika tu.Yanini kutafuta maradhi majukwaani kama yaliyompata Kikwete. Nahisi mheshimiwa raisi kwa sasa amechoka sana japo ni miaka 5 tu.Angewaachia wajanja wengine wakatifuana na yeye akaondoka na ushindi wa vita dhidi ya corona na ujenzi wa vituo vya afya.
 
Wanasiasa na wajanja wa dunia wote lao moja tu... vuta fikra kwa Lowasa ilikuwaje halafu endeleeni kumshangilia Membe
 
Back
Top Bottom