Magufuli 'ataiua' nchi lakini CCM haitasalimika pia!

mpk

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
3,115
3,863
Katika mizania yoyote Kikwete anaijua siasa sana kuliko Magufuli na kumlinganisha Kikwete na Magufuli kwenye siasa ni sawa na kulinganisha dimbwi na bahari. Uamuzi wa Kikwete kumkatalia kumkabidhi chama Magufuli unaweza kuchukuliwa kama ubinafsi au kutaka kutumia chama kulinda maslahi yake lakini ana maono.

Magufuli kubomoa nyumba za watu kwa maelfu ni 'ubabe', kufukuza, sorry kutumbua watumishi kwa mamia ni 'ubabe', kuzuia kuonyesha bunge live ni 'ubabe', mteule wake kufungia wabunge adhabu ambazo hazijawahi kutokea ni 'ubabe', kumteua mkuu wa mkoa na kumfukuza ndani ya siku 30 bila kumsikiliza ni 'ubabe', kumfukuza mkurugenzi wa jiji tena hadharani ni 'ubabe', kuwatangazia watanzani kwamba nchi yao itaendeshwa kikwatakwata ni 'ubabe', kufukuza wanafunzi 7000 kwa wakati mmoja tena wasio na hatia ni 'ubabe'.

Kuwatangazia watu unaowaongoza kwamba unowaongoza kwamba unataka waishi kama mashetani ni 'ubabe'
Haya ni makosa mengi sana kufanywa na kiongozi kwa muda wa miezi sita tu. Na kwa kuwa tulianza kwa vigelegele, haya yote hayakuonekana kama makosa. Lakini wasiosalimika ktk hili ni CCM, hawa ndo wahanga namba moja wa makosa haya!
 
Usisahau la kuzuia waaajiriwa kuchukua mafao yao hadi wafikishe umri wa miaka 55.

Ni kama aina fulani ya utumwa unarudi.Biashara hazifai kufanya sasa hivi na ajira ndo hizoooo na wanafunzi ndo kama unavyoona.Inabidi wananchi tuanze kupasa sauti zetu kimya kimya utashangaa katiba inakuja kubadilishwa na tunatawaliwa kwa miaka 30 ijayo na mtu yule yule.

Tunapoelekea ni pabaya sana.
 
Katika hoja yako kuna mambo nayakubali mengine sikubaliani nayo. Naunga mkono suala la watumishi kuwajibishwa pale wanapoleta utendaji mbovu. Hakuna mwajiri hata siku moja anaweza kuvumilia mfanyakazi asiye na tija. Ilifikia mahali unaingia ofisi za umma kutaka huduma watumishi waliopo humo ambao tunawalipa kwa kodi zetu wanakuangalia kama vile huitajiki au wee siyo mtanzania. Kwa hili mh. Rais tena akaze uzi zaidi.

Suala la kutoonyesha bunge LIVE, viongozi waandamizi walioshinikiza hili suala wamechemka. Suala la uhuru kwenye vyombo vya habari ni muhimu sana.
Kwenye era tuliyopo kuzuia vyombo vya habari kufanya kazi kwa uhuru ni sawa na kuirudisha nchi kwenye ujima. Nashangaa kweli ulimwengu unakimbia mbele Tanzania inapiga mbio kurudi nyuma. Hii ni hatari sana kwa afya ya Taifa.

Kuna mambo kwa kweli viongozi wetu wanafanya vizuri ila mengine wanatakiwa kukaa chini na kufanya maamuzi kwa busara zaidi ili kuondoa madhara yanayoweza kujitokeza. Na waache kufanya kazi kwa sifa bali wafanye kazi kwa tija. Na wafuate sheria zilizowekwa na siyo kujiamulia tu.

Hakuna kero kubwa kama kufanyia kazi jasho lako then ajitokeze mtu kukupangia masharti namna ya kuitumia. Hela iliyopo kwenye nifuko ya jamii ni wanachama. Mwanachama akiamua kujitoa ni haki yake na hela ni mali yake. Kuna mantiki gani ya kumzuia kuchukua hela yake? Mshahara wake umeshakata kodi, hata mafao yake mwisho wa siku anayataka kweli umzuie?

Natamani wenye mifuko hii wangekuwa wanaelewa kumpatia mtu hela akiwa na miaka 55 au 60, ni kumtengenezea maisha ya stress na kumpotezea tu uhai. Maana katika miaka 55 au 60 ndo unakuta mzee anaanza kujitahidi kuwekeza anakutana na changamoto kibao hela inapotea, hana nyuma wala mbele, presha zinapanda na kupotea.

Lakini mafao haya haya angepewa mtu baada ya kila miaka 5, akiwa kazini watu wangewekeza hela, watu wangetengeneza ajira nyingi binafsi, watu wangelipa kodi, na pato la nchi pia lingepanda. Me sijui kama walioamua kuleta hii sheria kama kweli walilipambanua kwa kina. Huwezi kutegemea kupanua wigo wa ajira wakati wale unaotegemea wasaidie sekta binafsi huwawezeshi na hata basi kile kilicho tayari kuwaidia kuinua sekta bado hutaki kuwapatia.

Mara nyingine ninapofikiria mambo kama haya naona siasa ni usanii mtupu na hakuna aliye tayari kumuinua Mtanzania kutoka katika dimbwi la UMASKINI. It's real very SAD, why ONLY us!!!
 
Katika hoja yako kuna mambo nayakubali mengine sikubaliani nayo. Naunga mkono suala la watumishi kuwajibishwa pale wanapoleta utendaji mbovu. Hakuna mwajiri hata siku moja anaweza kuvumilia mfanyakazi asiye na tija. Ilifikia mahali unaingia ofisi za umma kutaka huduma watumishi waliopo humo ambao tunawalipa kwa kodi zetu wanakuangalia kama vile huitajiki au wee siyo mtanzania. Kwa hili mh. Rais tena akaze uzi zaidi.
Unayakubali yapi sasa?
 
PIGA picha. Vuta hisia na kumbukumbu. Unakumbuka nini katika wakati kama huu, miaka 10 iliyopita? Mimi nakumbuka machache, yaliyotangulia na yaliyofuata baadaye. Nyakati zinashindana na kupingana; lakini zinafanana, anaandika Ansbert Ngurumo. Nakumbuka nyakati za kushangilia “ari mpya, nguvu mpya, kasi mpya.” Ni shangilio la kaulimbiu. Naoanisha hilo na hili la sasa: “Hapa Kazi Tu!”

Nakumbuka enzi za Rais Jakaya Kikwete kuitwa “chaguo la Mungu?” Wengine walimwita “Tumaini lililorejea.” Wapo waliomuita, “Mkombozi mpya wa Tanzania.” Wakati wakimwita Kikwete mkombozi, mtangulizi wake, Rais Benjamin Mkapa, alipewa majina yote mabaya. Mbabe. Katili. Mwizi. Aliambiwa ameharibu nchi. Hakuwa mtu wa watu. Naona kama tumerudi nyuma miaka 10. Chaguo la Mungu sasa linapewa sifa za kijambazi, na huyu mpya, John Magufuli anaitwa “mpenzi wa Mungu.”

Kikwete aliyeshangiliwa na kusifiwa, sasa anazomewa na watu wale wale waliomsifu na kumtukuza. Wapo wanaodiriki kusema amekuwa mbaya kuliko Mkapa. Miaka 10 baada ya kuahidiwa “maisha bora kwa kila Mtanzania” yakashindikana, sasa watu wanazungumzia “Tanzania Mpya” ya Rais Magufuli. “Tanzania yenye neema inawezekana” ya Kikwete imetoweka ghafla. Hatujiulizi wanakotoa kaulimbiu tamu zinazoteka wananchi kwa muda, halafu zikawatesa baadaye.

Watu wale wale, mambo yale yale. Hatujifunzi. Hatukui. Hatuendelei kwa sababu hatutumii fikra bali hisia. Ndiyo maana tunadanganywa kirahisi.
Namkumbuka, Gado, mchora katuni mmoja katika magazeti ya Nation, Kenya. Alichora waandishi wa Tanzania wakiwa wanalamba viatu vya Rais Kikwete.
Tafsiri yake ilikuwa pana. Ilikera watawala na waandishi. Lakini ujumbe ulikuwa umefika, kwamba vyombo vyetu vya habari, badala ya kumhoji rais, vilimtukuza.

Leo tukitazama nyuma, tunajivuna kwa kazi tuliyofanya kumdekeza na kumfikisha Kikwete hapo alipo leo? Yupo wapi Kikwete “rafiki wa vyombo vya habari” aliyehitimisha miaka 10 ya utawala wake bila kuruhusu zitungwe sheria za kulinda taaluma ya habari, waandishi, wamiliki wa vyombo vya habari na watoa habari? Kwa sababu ya “urafiki huo” wakosoaji kadhaa wa serikali – waandishi na wanaharakati wengine, waliumizwa, waliteswa, na wengine waliuawa. Tuligawanyika ilipofika zamu yetu kujadili mateso na dhuluma hizi. Tulilewa madaraka yasiyo yetu.

Hayo ndiyo malipo ya mapokezi ya shangwe tuliyompa. Miaka mitano ya kwanza ya “ari mpya, nguvu mpya na kazi mpya” ilizaa miaka mitano mingine ya “ari zaidi, nguvu zaidi, na kasi zaidi.” Tuliona lakini hatukutafakari. Hatukushtuka! Rais Kikwete huyu tunayemzomea leo, tulimharibu wenyewe. Na sasa tunamzomea wenyewe. Ni malipo ya “urafiki wa mashaka.”
Alipoanza ziara za kushtukiza katika ofisi na idara za serikali, tuliona ni mapinduzi makubwa sana. Alipopeleka wateule wake katika semina elekezi, halafu akawahutubia mwanzo hadi mwisho, tulisifu ubunifu mpya wa utendaji.

Hatukuhoji Kikwete amepata wapi maarifa ya ghafla anayojaribu kupandikiza kwa wasaidizi wake. Hatukuhoji alipata wapi uadilifu wa ghafla uliotufanya tumuone tofauti na mfumo wake. Tulidanganywa na tabasamu lake. Tulimezwa na nguvu yake ya kuteka na kutumia vyombo vya habari kuimba sifa zake. Hata vichwa vya habari vilibadilika. “Kikwete, we acha tu! Haijawahi kutokea.” Tulivyo wasahaulifu, Rais Magufuli naye alipoanza ziara za kushtukiza, tukarejea kule kule.

Rais Magufuli alipofuta semina elekezi, tukamuona shujaa, wakati sisi ndio tulishangilia semina hizo zilipoasisiwa na Kikwete miaka 10 iliyopita. Kama vile Rais Kikwete alivyojaribu kujijenga kwa kumbomoa Mkapa, huyu naye anajijenga kwa kumbomoa Kikwete. Ndiyo “majipu” haya yanayotumbuliwa. Ni “majipu” ya Kikwete. Ni “majipu” tuliyosababisha wenyewe kwa kushangilia matendo, kauli na vituko vya Kikwete. Ni “majipu” ya makofi na vifijo vyetu. “Majipu” haya yanayotumbulia ni salamu kutoka juu. Ni dhihaka isiyo kifani kwamba chaguo la Mungu linatumbuliwa majipu!

Tunaponzwa na ukasuku wa “kuimbaimba” kaulimbiu za watawala.
Rais Magufuli wa leo hatofautiani na Rais Kikwete wa Machi 2006. Wote wanajua jinsi ya kucheza na hisia za wananchi. Huyu anazungumza lugha ya wananchi waliokata tamaa. Anatoa matumaini mapya kwa wananchi maskini wanaokerwa na utajiri wa wengine, na walioaminishwa kwamba utajiri huo, kama usingekuwa mikononi mwa hao wachache, ungekuwa kwa maskini hao.

Wananchi wanashangilia jinsi anavyotumbua majipu kwa sababu aliyetanguliwa aliyalea. Lakini naye anasahau kwamba anajenga msingi wa yeye kutumbuliwa baadaye. Kikwete tuliyemlea, aliyelewa sifa zetu, akafanya atakavyo, ameacha shida zinasotesa wananchi. Wanasema amewaachia shida. Wanalia. Rais Magufuli anatumbua majipu yake, yeye “anatumbua raha” alizojiandalia kwa miaka 10 mfululizo. Na wakati wananchi wanashangilia utumbuaji wa majipu unaofanywa na rais, hawana muda wa kutafakari, ni akina nani wanateuliwa kuziba nafasi za wanaotumbuliwa.

Je, tunawajua na kuwaamini wanaoingizwa kuzina nafasi za waliotumbuliwa majipu? Mbona wengi wao ni watu waliokuwa karibu sana na Magufuli huko alikotoka? Mbona na huko kuna majipu mengi waliyosababisha kabla ya kuondolewa? Yawezekana utumbuaji huu wa majipu ni fursa ya Magufuli kuchomoa watu wa Rais Kikwete na kuchomeka watu wake kwenye serikali?
Rais Magufuli si “rafiki wa vyombo vya habari” lakini ana uhusiano mzuri na baadhi yetu, na ameanza kujifunza jinsi ya kuishi na vyombo vya habari na waandishi ili wasimtumbue jipu.

Anajaribu kujenga kundi la watetezi wake. Ameshapata genge la washangiliaji. Anajaribu kugawa makundi ya wakosoaji. Nia yake ni moja. Aachwe apumue. Afanye atakalo. Tutajadiliana baada ya miaka mitano. Na kwa wengine, Rais Magufuli hachekicheki kama Kikwete. Anafura. Anachukia. Anaamuru.
Mtu mmoja amesema, “kama mliumizwa na rais anayetabasamu, kwa huyu mtauawa wengi. Punguzeni makali. Huyu ni mkali.”

Sikiliza kauli na ahadi zake mbele ya majaji na mahakimu. Rejea hotuba yake bungeni kuhusu mustakabali wa katiba mpya. Jikumbushe hotuba yake ya Singida kuhusu vyama vya siasa.
Hakika, hii siyo Tanzania tunayotaka kujenga. Nchi ya waoga. Nchi ya wanafiki. Nchi ya kujipendekeza. Nchi ya kukubali bila kuhoji. Nchi itakayoangamia kwa ukimya wetu.

Imeandikwa na Ansbert Ngurumo
 
CCM hawajalipana mishahara kwa miezi zaidi ya mitatu,mishahara yao inapatikana kwa dili ndani ya serikali,kwa kutengeneza uhaba wa sukari,mchele,halafu ikishaagizwa pesa inaenda CCM,hizi dili magufuli atazikubali? Je magufuli atakubali kuwafukuza wapiga dili walioishia darasa la saba wanaoshinda Lumumba na ofisi za CCM nchi nzima?magufuli atakubali kuzikagua Mali za chama ambazo sasa zimemilikishwa au kutumika kwa watu wachache? Magufuli atakubali? Atakubali kuwa mwanasiasa sio MTENDAJI na sio mwanasiasa?
 
Katika mizania yoyote Kikwete anaijua siasa sana kuliko Magufuli na kumlinganisha Kikwete na Magufuli kwenye siasa ni sawa na kulinganisha dimbwi na bahari. Uamzi wa Kikwete kumkatalia kumkabidhi chama Magufuli unaweza kuchukuliwa kama ubinafsi au kutaka kutumia chama kulinda maslahi yake lakini ana maono.

Magufuli kubomoa nyumba za watu kwa maelfu ni 'ubabe', kufukuza, sorry kutumbua watumishi kwa mamia ni 'ubabe', kuzuia kuonyesha bunge live ni 'ubabe', mteule wake kufungia wabunge adhabu ambazo hazijawahi kutokea ni 'ubabe', kumteua mkuu wa mkoa na kumfukuza ndani ya siku 30 bila kumsikiliza ni 'ubabe', kumfukuza mkurugenzi wa jiji tena hadharani ni 'ubabe', kuwatangazia watanzani kwamba nchi yao itaendeshwa kikwatakwata ni 'ubabe', kufukuza wanafunzi 7000 kwa wakati mmoja tena wasio na hatia ni 'ubabe'.

Haya ni makosa mengi sana kufanywa na kiongozi kwa muda wa miezi sita tu. Na kwa kuwa tulianza kwa vigelegele, haya yote hayakuonekana kama makosa. Lakini wasiosalimika ktk hili ni CCM, hawa ndo wahanga namba moja wa makosa haya!

Hapna wahanga sio CCM, NI WANANCHI MASKINI
 
Usisahau la kuzuia waaajiriwa kuchukua mafao yao hadi wafikishe umri wa miaka 55.

Ni kama aina fulani ya utumwa unarudi.Biashara hazifai kufanya sasa hivi na ajira ndo hizoooo na wanafunzi ndo kama unavyoona.Inabidi wananchi tuanze kupasa sauti zetu kimya kimya utashangaa katiba inakuja kubadilishwa na tunatawaliwa kwa miaka 30 ijayo na mtu yule yule.

Tunapoelekea ni pabaya sana.
Nyie mnaopinga mipango ya serkari ni wanafiki na serikali haina sababu ya kuwasikiliza. Hapa sasa hivi kunakelee za wazee walipwe pensheni. Wanalipwa kutoka kwenye mfuko gani PSPF,NSSF LAPF? Serikali inapanga kuangalia namna bora ya kuwahudumia wazee wetu kwakuwa tulitoka katika enzi ya jahiliya.
Hii mifuko haifi wewe utaondoka utaicha ikihudumia watu. Ulichokichangia humo lengo lake ilikuwa ni kukusaidia pale nguvu zako zitakapopungua. Hivyo ukiacha kazi eneo hili utaendelea kuchangia kama mtu binafsi mpaka utakapopata kazi sehemu nyingine na kuendelea kuchangia wewe na mwajiri mpya. Hata watu ambao hawana ajira wanashauriwa kujiunga kwenye uchangiaji huu wa mifuko ya hifadhi.
Sidhani wewe uliyetoa mchango huu si unayetoa povu kuhusu wazee kulipwa pensheni. Kama unajua kuwa wazee wanahitaji kuwezeshwa basi changia kujiandaa na uzee wako.
 
Wanafunzi kufukuzwa ni sawa kabisa kwa mujibu wa taratibu za uendeshaji na usimamizi wa vyuo vikuu. Kutumbua wazembe na wabadhirifu wa mali za umma ni sawa kabisa. Tena maomba aongeze kasi ya kuwatumbua hadharani. Watanzania tumezi mno kwa tabia ya uzembe na wizi.

Kupiga marufuku kuchukua mafao mpk utakapofikisha miaka 55 ni sawa kabisa. Uzoefu unaonyesha wengi mnaishia kuzifuja tu hizo pesa halafu mnageuka kuwa wazee mzigo. Acha hela yako huko ili uzee wako usigeuke kero kwa taifa. Kumteua Mkuu wa MKOA na kumtumbua ndani ya siku 30, hii ni zaidi ya sawa. Hata ndani ya siku saba ingekuwa poa. Mkuu gani asiyeweza kufuatilia na kujiridhisha juu ya taarifa anazopewa na watendaji walio chini yake? Watanzania tuache maisha ya kulindana. Halafu pia tujenge tabia ya kukataa baadhi ya teuzi kama hatuziwezi.

Kubomoa nyumba za mabondeni kwa hili naomba aingie na mikoani. Ninyi ndiyo wa kwanza kulalamikia serikali mnapopatwa na mafuriko. Haikubaliki! Haikubaliki! Serikali naomba iongeze kasi ya kuzibomoa. Ili tupange miji yetu vema lazima pia waliojenga holela wabomolewe nyuma zao. Ukitaka uzuri sharti uzurike.

Watanzania tuache kelele. Binafsi naona rais yuko sahihi kwa mambo yote isipokuwa hili la kuonyesha bunge recorded.
 
Makufuli alisema ana uchungu na wanyonge..
leo kawatimua watoto wao kama mbwa bila hata nauli wakati ni serikali hiyohiyo iliyowaomba wasiende form five ili wakasomee diploma wawe walimu wa dharura wa sayansi..
Ivi ni kweli mwanafunzi mwenye grade A na B matokeo ya form IV,tena masomo ya sayansi hana sifa za kusomea Diploma ?
eti hata waliowadahili na kuwapa mikopo nao ni majipu wakati hela walizotoa hazikua za Pombe zilikua makusanyo chini ya JK..
akh mi mgeni..
nilidhani anatumbua majipu kumbe anatumbua aliyoyafanya JK liwe zuri au baya..
 
Baba anayempenda mtoto wake ni yule anayechuma fimbo na kumcharaza mara kwa mara. Pia upo umuhimu wa kukubaliana na ukweli kwamba huwezi kuitarajia kesho yenye mabadiliko kwa kuitegemea fikra zile zile za jana, ambazo uzoefu unaonyesha kuwa hazijaweza kukusaidia.
 
Back
Top Bottom