Magufuli ataheshimika zaidi akiomba msamaha

mzamifu

JF-Expert Member
Mar 10, 2010
6,368
3,814
Kati ya mawaziri wote ktika serikali ya dr kikwete magufuli anaonekana kuaminika zaidi. Yeye pia anajua hilo. Hivi majuzi alitetereka kidogo na kutoa kauli ya kejeli. Ingawa kupanda kwa nauli kigamboni ni jambo ambalo halikwepeki, haikumpasa magufuli awaambie wananchi wapige mbizi au warudi vijijini kama hawamudu nauli ya shs 200. Walio wengi kigamboni ndiko kukliko vijij vyao sasa warudi wapi? Aombe tu radhi kwani atapungukiwa na nini?
 
kwani kakosea nini kuwaeleza ukweli, acheni siasa kwa mambo madogo magufuri yupo sahii mbona kijana jana kaweza, au nani aliwaambia wakanunue kigamboni, si lazima waje mji wa maraha hawawezi watulie uko uko
 
Nauli ni 200, samahani ya nn si ameeleza ukweli? Au wananchi wa kigamboni ndo leo mmeanza kupandishiwa vitu? Acheni ufinyu wa mawazo.
 
Mbona la Magufuli linakuzwa? Mbona mkuu wa nchi alipowaambia waathirika wa mafuriko Dar kuwa mtu mwenye akili timamu hawezi kuishi mabondeni. Hilo ndio tusi. Ama ya Magufuri aliyosema kama utani, au kwa vile si mtani wa watu wa Dar?
 
Kama huna nauli piga mbizi, kwishney... Tatizo wabongo mmezoea viongozi waongo wanaouma na kupulizia na wanafiki kwa kushindwa kuwaambia ukweli ndio maana mnaona kuambiwa ukweli ni kejeli...

Hakuna kuomba msamaha na mapato yamepaa mara mbili pale kivukoni, wakinunua kivuko kingine kwa own sources ni nyie ndio mtakaonufaika acheni mawazo ya Dr Dr Dr Dr Dr Kikwete kuwa mtapata vivuko vya msaada pindi Alina iliyozeeka ikiwazamisha
 
Alivyo na kichwa kama cha Kambare hana hata mwelekeo wa kuomba msamaha!

Kichwa cha Kambare ni wewe hapo unayependa kudanganywa kijinga.

Hivi hao wakazi wa Kigamboni walivyomzomea munaona ni sawa?

Mkuki kwa nguruwe lakini kwa binadamu ni mchungu mno.

Way to go Magufuli, semaaaa usiogope semaaaa.
 
Msijali WAKUU, tutasahau baada ya muda mfupi kama kawaida yetu. Kwani la mafuriko nani anakumbuka kwa sasa?

hebu jiulize, KUNA BAADHI YA STATEMENTS HAPA CHINI NI ZA KUKERA SANA NA DHARAU KWA WANANCHI NA KUONYESHA DHARAU. SIKUMBUKI KUSIKIA HATA MMOJA AKIOMBA SAMAHANI. BADALA YAKE, LEO HII BAADHI YAO MWAPO KATIKA KUPIGA VITA UFISADI. Dr. Pombe ana lipi la ajabu?

  1. B. Mramba Waziri--- Ndege ya Raisi Lazima Inunuliwe ikiwezekana hata Wananchi Wale Nyasi..
  2. Ben Mkapa Raisi -- Ununuzi wa Migodi kwa Njia Za Ajabu na Watu wana Wivu wa Kijinga!
  3. Jk-- Huyu naona ajali kitu tumuache kesi zake ni kubwa tuiachie mahakama kuu- Kelele zenu hazinifanyi nishindwe kulala!
  4. Mkulo -- Kila mwananchi atabeba Msalaba Wake... Serikali haimo
  5. Jk-- sizitaki kura za wafanyakazi
  6. Sofia Simba-- Wanawake Wanyimeni Waume zenu! ''xoxoxoxo'' Wakiwapigia kura Wapinzani
  7. Mwantumu Mahiza -- Waliomaliza vyuo na kukosa ajira waanzishe miradi ya kufuga kuku inalipa sana.
  8. Nape - -Tutawashikisha ukuta.
  9. Masaburi -- Wabunge wa DSM wanafikiria kwa Makalio
  10. Wassira -- Mnaulizia mvua kwani nani kawaambia mimi ni waziri wa mvua?
  11. Riz1wani Mtoto wa Kiongozi -- Mimi si Fisadi Naishi Kimjini mjini Nina kipande kidoogo cha Uwanja wa Urithi na Toyota Collola Hayo ma Vogue mnayoniona nayo si yangu Bongo tunaishi kimjini mjini.. Lake Oil sio Yetu.
  12. Mkapa--Waandishi wa tz upeo wao mdogo ndio maana nafanya mahojiano na waandishi wa nje
  13. Pinda --Vihela vyenyewe vidogo vinaishia kuwapa wapiga kura wetu wanapokuja dodoma.
  14. Kikwete: foleni dar es salaam ni ishara ya maisha bora .
15. OCD Arusha - Wakazi wa Arusha ni mapanya. "sualala Lowassa ni ajali ya kisiasa tu" -JK
16.
Kilavu Akiwaambia Wanachadema -- Mmemuachia Nyani alinde Mahindi yenu...
17. Mimi naKikwete hatukukutana Barabarani"
18. JSMalecela (J4)----Nendeni kuzimu ndiko hakunaSHIDA-
19. Sumaye:Ukitaka biashara yako ifanikiwe UJIUNGE na CCM;
20. Msuya:Kila mtu atabeba msalaba wake mwenyewe
 
Kama mtu hana shs 200 anapanda pantoni kwenda wapi? kuomba omba?
 
Magufuri asipoomba msamaha ataheshimika, kwani aliowambia wapige mbizi ni watani zake, na pinda asipoingia mkenge wa wabunge wa kushusha nauli, Pombe ataheshimika zaidiiiiiiiiii
 
Kati ya mawaziri wote ktika serikali ya dr kikwete magufuli anaonekana kuaminika zaidi. Yeye pia anajua hilo. Hivi majuzi alitetereka kidogo na kutoa kauli ya kejeli. Ingawa kupanda kwa nauli kigamboni ni jambo ambalo halikwepeki, haikumpasa magufuli awaambie wananchi wapige mbizi au warudi vijijini kama hawamudu nauli ya shs 200. Walio wengi kigamboni ndiko kukliko vijij vyao sasa warudi wapi? Aombe tu radhi kwani atapungukiwa na nini?

Mi nadhani ataheshimika zaidi asipoomba msamaha.
 
Kati ya mawaziri wote ktika serikali ya dr kikwete magufuli anaonekana kuaminika zaidi. Yeye pia anajua hilo. Hivi majuzi alitetereka kidogo na kutoa kauli ya kejeli. Ingawa kupanda kwa nauli kigamboni ni jambo ambalo halikwepeki, haikumpasa magufuli awaambie wananchi wapige mbizi au warudi vijijini kama hawamudu nauli ya shs 200. Walio wengi kigamboni ndiko kukliko vijij vyao sasa warudi wapi? Aombe tu radhi kwani atapungukiwa na nini?
Aombe radhi watanzania hasa Nyumba alizoshinikiza zikauzwa hii ya kigamboni mbona kosa dogo tu watanzania tunahitaji maelezo ya kina kuhusu nyumba walizipora
 
Magufuli hana haja ya kuomba radhi...ameshawaambia wabunge wa Dar waichukue panton waiendeshe na kuisimamia wenyewe ....kelele za nini?
 
kupiga mbizi si tusi ni ushauri wa namna kukabiliana na tatizo. Ningekuwa magufuli ningewaambia 'mkafie mbali'
 
Ndiyo maana nchi hii maendeleo yetu ni haya tuliyonayo, watu wanapenda sana lugha na kauli za kuzunguka na kuzungushwa zungushwa, ambazo zinawafanya mbaki na uhakika wa namba katika kikosi cha wajinga na wapumbavu.
Hivi mlitaka Magufuli asemeje? Kuwa "kama hamna nauli tafadhali ombeni lift, mnaweza kusaidiwa kama watakubali"
hamuoni kuwa ni rahis sana alivyosema "pigeni mbizi" straight to the point, a lot of time have been served hapo, au hatulioni hilo kwa kuwa hatujui thamani ya muda?
Hatutaki tuambiwe ukweli, munapenda sana kubembelezwa, anyway msijali viongozi wa kuwabembelezi na kuwa danganya-danganya tayari mnao, watawabembelezini na mtasinziaa mpaka mikono yao itapapasa makal.io yenu pumbav.u.
Grow up, see and face the reality.
Kuna waliotetewa mabondeni, wote tumeona.
 
Sioni sababu ya MH MAGUFULI haja ya kuomba msamaha na kuendekeza mambo ambayo hayana maana. ukweli ni kwamba kama
kuna mtu hawezi kulipa nauli ya TSHS 200/= maana yake ni kwamba analazimisha kuishi DAR,DAR IS NOT HIS ENERGY LEVEL he/she MUST GO WHERE HE/SHE BELONGS.Wanasiasa wanaiharibu nchi hii.wakazi wa dar siyo special kuliko wengine wanako lipa zaidi ya shs 500/ kuvuka kutoka upande mmoja kwenda upande wa pili kwa kivuko.NASISITIZA WABUNGE WA DAR WANAPENDA
CHEAP POPULARITY HAWAFAI HATA KIDOGO.MAGUFULI DO NOT APOLOGIZE YOU ARE QUITE OK.AND IN FACT SURVIVAL IS FOR THE FITTEST,IF LIVING IN DAR IS EXPENSIVE TRY MTWARA, LINDI OR MIKESE.
 
Mbona la Magufuli linakuzwa? Mbona mkuu wa nchi alipowaambia waathirika wa mafuriko Dar kuwa mtu mwenye akili timamu hawezi kuishi mabondeni. Hilo ndio tusi. Ama ya Magufuri aliyosema kama utani, au kwa vile si mtani wa watu wa Dar?

Hata wafanyakazi washaambiwa akili za mbayuwayu lakn wakafurahia tu..
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom