The Boss
JF-Expert Member
- Aug 18, 2009
- 49,229
- 116,840
Watu humu tumejadili uzembe wa serikali kuruhusu watu kujenga mabondeni na pia suala la waliojenga maeneo kama kingo za mito wenye vibali na hati zote.
ikiwemo kupimiwa viwanja na wizara ya ardhi na 'unyama' wa serikali kutaka kuwavunjia bila kuwapa muda wa kwenda mahakamani wala kuwalipa fidia.
Sasa baada ya serikali kusitisha zoezi na kujaribu kutafuta namna sahihi ya kibinaadamu
ya kutatua tatizo hilo.
anasema serikali isiwatazame nyani usoni.
Kweli Tanzania yetu haishi maajabu.
======================
Chanzo: Raia Mwema
ikiwemo kupimiwa viwanja na wizara ya ardhi na 'unyama' wa serikali kutaka kuwavunjia bila kuwapa muda wa kwenda mahakamani wala kuwalipa fidia.
Sasa baada ya serikali kusitisha zoezi na kujaribu kutafuta namna sahihi ya kibinaadamu
ya kutatua tatizo hilo.
anasema serikali isiwatazame nyani usoni.
Kweli Tanzania yetu haishi maajabu.
======================
UKITAKA kuwafukuza nyani watoke kwenye shamba lako fanya hivyo bila kuangaliana nao usoni. Huku kumkoma nyani giledi kunamtaka mtu kutokumuangalia nyani na kudhani ni binamu yake.
Ukianza kumfukuza nyani halafu ukamuangalia usoni utaanza kuona haya na huruma. Utaona haya kwa sababu utaona kama unamfukuza ndugu yako na utaona huruma kwa sababu unajua kabisa kuwa nyani naye ni kiumbe wa Mungu na anahitaji kula yeye na ‘familia’ yake.
Ukishapatwa na hisia hizo mbili ni rahisi kujiuliza kama unamtendea “haki” nyani ambaye alikuwa anakula mazao yako au unamvunjia haki zake za msingi kama mnyama.
Mfano huu wa nyani unaweza usiwe mzuri sana; lakini naweza kabisa kuuhamishia kwa binadamu na bado ukabakia kuwa kweli.
Ukimkuta mtu anaiba shambani kwako na kujaza magunia na hata malori utakuwa ni mtu wa ajabu kama utaamua kuangaliana naye usoni na kutaka kujua hasa sababu za yeye kukufanyia hivyo. La kwanza utaita watu waje kukusaidia kumuweka chini ya ulinzi ili kumkusanya yeye na ushahidi wote ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria.
Akianza kukuelezea habari za kuwa anafanya hivyo ili ailishe familia yake sidhani kama utakubali kirahisi na kumuachilia huru; akidai kumkamata kwako kuna mvunjia haki za binadamu au kuna mdhalilisha sidhani kama utakubali kirahisi.
Ukweli ni kuwa kasi ya Magufuli inaweza kujikuta haiendi mbali katika kurudisha utawala wa sheria na nidhamu katika utendaji wa serikali. Kwa muda mrefu kumekuwa na matatizo makubwa katika suala la kutoa viwanja kwenye maeneo ambayo hayaruhusiwi au yalipangwa kuwa ni ya wazi au maeneo ya mabondeni ambayo ni rahisi kufurika.
Matatizo haya yamekuwa na matokeo katika maisha ya watu wengi na katika utendaji mzima wa serikali. Yamechangia ujenzi holela, milipuko ya magonjwa, matumizi ya rushwa na uvunjwaji wa haki za watu wengine nikiyataja matatizo machache tu kati ya mengi.
Sasa Rais Magufuli na timu yake wanapoingia na kuanza hizi safisha safisha tayari kuna watu wameanza kukosa raha kwa sababu inaonekana kana kwamba wanataka kula wasicholima na kuvuna wasichopanda wao.
Wanataka waachwe kwa muda kwa sababu na wao ni binadamu; kwamba mambo ambayo wao wameyafanya na kusababisha adha kwa watu wengine na hata kwa wao wenyewe siyo hoja kubwa isipokuwa haki yao wao kuendelea kuwepo mahali hapo.
Kuna ushahidi wa kutosha wa jinsi gani baadhi ya watu wenye uwezo waliweza kujipatia viwanja mahali ambapo haparuhusiwi kujengwa na wakajenga majumba makubwa (siyo mahekalu – hayastahili heshima hiyo).
Majumba haya sasa yanatishiwa kuvunjwa na watu hawa hawa wanatumia tena uwezo wao kujaribu kutafuta namna ya kutoka. Na wapo watu ambao nao hawana uwezo mkubwa sana lakini wana uwezo kidogo wa kucheza na watendaji kwenye halmashauri na wao wakaaamua kujenga kwenye maeneo ambayo si salama na hayapaswi kuwa na ujenzi wa makazi ya watu.
Hawa nao wanapoambiwa watoke wanaanza kulia na kusema “twende wapi twende wapi” na “kwa nini sisi kwa nini sisi”.
Wote hawa ni binadamu na raia na wana haki zao za msingi. Lakini haki zao pia zinapoenda kugongana na haki za watu wengine au za jamii kubwa uamuzi basi si mgumu kuchukua na kusita kuchukua uamuzi huo ni kuwafanya watu wahoji kama tumeamua kweli kubadilika au la.
Watu waliojenga mabondeni na waliojenga kiholela wote wanavunja haki nyingi za raia wengine. Kama mtu mwenye hela aliweza kuchukua eneo la wazi akajenga hoteli kubwa ni kweli hoteli tunahitaji na ni biashara; lakini vipi haki ya watu kuwa na eneo wazi kwa ajili ya mapumziko na maeneo ya kuchezea watoto; vipi haki za watoto wa maeneo hayo ambao sasa hawana maeneo salama ya kucheza wanaishia kucheza kwenye mashimo ya taka au maji machafu au kwenda kwenye viunga vya watu wazima? Haki za watoto hawa nani anazisimamia?
Wale waliojenga mabondeni na kusababisha msongamano na hata kuchangia milipuko ya magonjwa na mambo mengine wanajali vipi haki za watu wengine ambao wanastahili maisha salama na maeneo salama.
Binafsi naamini kama Magufuli ameamua kusafisha nchi afanye hivyo bila kupepesa macho vinginevyo yeye na wenzake watakwama. Watakwama kwa sababu watakuwa wameanza kutazamana na nyani usoni. Ukishaangalia majina ya watu, utajiri wao na malalamiko yao ni vigumu kuona utaweza kumuondoa nani na kwa nini.
Hili ni kweli siyo kwenye mambo ya viwanja tu hata kwenye sehemu nyingine ambazo watu wameanza kusafishwa. Wale waliotumia ofisi zao vibaya (kama tulivyoona bandari na TRA) je waondolewe? Na wao si binadamu? Na wao si wanafamilia? Kwa nini wakamatwe na wawekwe mikononi mwa polisi – watoto wao wataishi vipi? Na watasoma vipi kama wazazi wao watafukuzwa kazi?
Kama tukiangalia vitu hivyo basi hakuna mhalifu atakayekamatwa na hakuna mtendaji yeyote mbovu ambaye atafukuzwa kazi! Wote ni binadamu na wanamahitaji mbalimbali ya kibinadamu.
Ni kwa sababu hiyo natoa wito kwa Magufuli na watendjai wake; ni kweli wajali haki za raia na binadamu. Lakini wanapofanya hivyo wajue pia kuna suala la kuangalia haki kuu zaidi za raia na za binadamu.
Wakianza kuangaliana na wahalifu na waliovunja sheria na kuona machozi yanavyowalenga basi watajikuta wanasita kuchukua uamuzi; na wakisita wamekwisha; watakuwa wanachekacheka na nyani; huku nyani wanakula mahindi; au wanasubiri msimu mwingine wa mavuno.
Magufuli akianza kuyaangalia majipu na kuyapaka rangi mengine yaonekane madoa tu atakwama. Kama alitaka kuwa mtumbua majipu ayatumbue kwani alisema mwenyewe hakuna njia nyingine. Isipokuwa kama hakumaanisha; kwamba alikuwa anazungumzia “baadhi” ya majipu.
Akifanya hivyo - Magufuli atakwama.
Chanzo: Raia Mwema
Last edited by a moderator: