Elections 2015 Magufuli asema Mafisadi wanamwogopa ndio maana hawataki aingie Ikulu

Mr Chin

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
4,625
1,024



MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Magufuli, amesema mafisadi hawawezi kumpigia kura katika Uchaguzi Mkuu ujao kwa kuwa wanamwogopa.

Dkt. Magufuli aliyasema hayo jana kwenye mkutano wa hadhara,uliofanyika katika Viwanja vya Mvumi Misheni, Jimbo la Mtera,mkoani Dodoma.

"Mafisadi hawawezi kunichagua kwa sababu wananiogopa ila wapo Watanzania wengi

wanaonipenda na kunikubali wakiwemo maskini wenzangu, wanyonge ambao watanipa kura nyingi ili niweze kuwatumikia na kutetea masilahi yao," alisema.

Alimpongeza mwanasiasa mkongwe, Mzee John Malecela kwa ujasiri wake wa kuendelea kubaki CCM licha ya kushindwa katika mbio za kuwania nafasi ya urais miaka iliyopita.

"Mzee Malecela aliwahi kugombea uteuzi wa nafasi ya urais, lakini hakufanikiwa na hakufikiria wala kuthubutu kuhama chama hata siku moja, bado yupo na amekuwa msaada mkubwa," alisema.

Alisema mbali ya kuukosa urais, pia aliangushwa kwenye nafasi ya ubunge wa Jimbo la Mtera na Livingstone Lusinde lakini hakuhama chama. Alisema anawashangaa waliohama CCM baada ya kukosa nafasi.

Aliwaomba Watanzania wamchague aweze kubadilisha maisha yao na kukuza uchumi akiwataka wasikubali kudanganywa na wapinzani ambao hawana sera wala uzoefu wa kuongoza Serikali.

Akizungumzia sera ya elimu bure, alisema hakuna sababu ya kukosa madawati wakati nchi ina rasilimali kubwa ya miti; hivyo alitoa wito kwa Wakurugenzi kukaa mkao wa kufanya kazi.

Livingstone Lusinde

Naye Mjumbe wa Kamati ya Kampeni za CCM na mgombea ubunge Jimbo la Mtera, Lusinde alisema CHADEMA kimepoteza mwelekeo baada ya kuwapokea wanasiasa waliowatuhumu kwa kashfa mbalimbali ndani na nje ya Bunge.
 
haa haa vipi na wale mafisadi waliouza nyumba za serikali kwa bei ya kutupwa na zingine kuwapa nyumba ndogo zao wanamuogopa?
 
Vp kuhusu ufisadi alioufanya yeye wa kununua meli mbovu ya billion 8,vp ufisadi ambao CAG ameouona kwenye wizara yake wa billion 262? Aache ulofa!
 
kiufupi sisi wananchi ndo hatumtaki, asitafute wa kumbebesha zigo lake
 
Eti mafisadi wananiogopa!!!Kwani nchi ina mafisadi wangapi??Nani mwl wa hao anaowaita mafisadi km sio chama chake??
LENGO LETU SIO KUCHAGUA FISADI BALI NI KUIONDOA CCM MADARAKAN NA HILI LIKISHINDIKANA BASI NITAAMINI KABISA MANENO YA MH BEN MKAPA KUWA SISI NI MALOFA,wapumbavu na MAMBUMBUMBU!
 
Asahau kuingia ikulu hatuwezi kumpeleka ikulu mtu mropokaji na mwenye kujaa mihemko

kiongozi lazima awe na hekima

Katika orodha ya wenye hekima Lowasa do ndiyo wa mwisho? Kung'ang'ania kuwa rais ni kukosa hekima tena ni dharau na chuki kwa viongozi waliomlea Lowasa na asivyo na hekima akishindwa kwenye kura atakataa na wafuasi wake watasababisha damu imwagike kwani hata sasa wana mihemko na wamekosa busara na ni waropokaji.
 
Eti mafisadi wananiogopa!!!Kwani nchi ina mafisadi wangapi??Nani mwl wa hao anaowaita mafisadi km sio chama chake??
LENGO LETU SIO KUCHAGUA FISADI BALI NI KUIONDOA CCM MADARAKAN NA HILI LIKISHINDIKANA BASI NITAAMINI KABISA MANENO YA MH BEN MKAPA KUWA SISI NI MALOFA,wapumbavu na MAMBUMBUMBU!
Fisadi ni lowasa na kundi lake la mafisadi kama mbowe,mbatia,mtei na wengine alionao kwenye timu yao.
 
Walipokwaupa kweupe escrow account mafisadi hawakumwogapa?

Magufuli na ccm wanataka kubaki madalakani ili KULINDA UOVU WAO TU, NA SI KWA MASLAHI YA WATZ.

Magufuli anaogopa ataanikwa kwa ufisadi wake wa nyumba za umma na ufisadi kwenye ujenzi wa barabara.
 
Yaani mpaka uchaguzi upite watanzania wapenda mabadiliko tutaitwa kila jina. Tumeitwa wapumbavu, malofa na sasa mafisadi ila mwisho sisi ndiyo tutakuwa MASHUJAA.
 
Inaamaana JK nae anamuogoopa. Mbona kasema akiingia magufuli atapata usingizi. Sasa Fisadi gani anayemuogopa
 
Back
Top Bottom