Magufuli aponda dhana ya polisi jamii dhidi ya majambazi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,319
33,125
Magufuli%2820%29.jpg

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, John Magufuli.



Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, John Magufuli, ameiponda dhana ya polisi jamii inayotumiwa na Jeshi la Polisi katika kupambana na uhalifu kwa maelezo kwamba utaratibu huo hauwezi kusadia mapambano dhidi ya ujambazi.
Magufuli amesema haiwezekani kuhubiri polisi jamii kwa jambazi huku wananchi wakiendelea kuumia, kupoteza maisha na mali zao kutokana na vitendo vya ujambazi.
Aliyasema hayo juzi katika ‘mwalo’ (ufukwe) wa Kigangama wilayani Magu kabla ya kuweka jiwe la msingi la mwalo huo pamoja na kuzindua boti ya doria kwa ajili ya kudhibiti uvuvi haramu katika Ziwa Victoria upande wa wilaya ya Magu.
Alisema anaruhusu boti hiyo itumiwe pia na Jeshi la Polisi katika kupambana na vitendo vya uhalifu ziwani na ndipo alianza kuiponda dhana ya polisi jamii.
“…na nimeona hapa kuna OCD, ataitumia pia kupambana na majambazi ili akikimbilia majini, chukueni hii (boti) mfuate huko huko mkamshike. Na msiendekeze sana suala la polisi jamii. Hakuna jamii sana kwa majambazi. Jambazi lishughulikie tu kikamilifu na siyo polisi jamii,” alisema.
Aliongeza: “Kusikia kwa kenge mpaka damu itoke kwenye sikio na kusikia kwa jambazi mpaka damu itoke kwenye sikio. Utaanza kulielimisha jambazi wakati lenyewe zinawazamisha wananchi majini. Unaanza kulielimisha wakati lenyewe lina SMG."
Waziri Magufuli alienda mbali kwa kusema kuwa angekuwa kwenye wizara husika ya Mambo ya Ndani suala la polisi jamii angelizungumzia kwa wananchi wema tu na siyo kwa majambazi kwani hayo yanapaswa kushughulikiwa hasa.
“Wenye kusikia wamesikia. Ningekuwa mimi huko (Mambo ya Ndani) polisi jamii ningeizungumzia kwa wananchi tu lakini kwa jambazi hakuna cha jamii, unamshughulikia kisawasawa. Nasema wasikie na msemakweli ni mpenzi wa Mungu,” alisema.
Aliongeza: “Endeleeni jamii huku watu wanaumia. Unamkuta mtu ana bomu bado una jamii, unamkuta mtu amemchoma mtu amekimbilia majini bado unang’ang’ania jamii. Unamkuta mtu ametega mawe barabarani ana mapanga amekaa bado unang’ang’ania jamii. Sitaki kuingilia wizara nyingine lakini hayo yananikera.”
Aidha, Waziri Magufuli amewatahadharisha wanasiasa watakaoingiza siasa katika mapambano dhidi ya uvuvi haramu kwa lengo la kujipatia kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Aliongeza kuwa wanasiasa bila kujali kama kuna uchaguzi, wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya uvuvi haramu kwani wao kupitia Bunge ndio wamepitisha Sheria Na. 22 ya mwaka 2003 inayopiga marufuku uvuvi haramu kwa lengo la kunusuru samaki wasitoweke katika maziwa, bahari, mito na mabwawa.
Waziri Magufuli aliweka jiwe la msingi katika ujenzi wa mwalo wa kisasa wa Kigangama ambao utakaogharimu zaidi ya Sh. milioni 600 pamoja na kuzindua boti ya doria kwa wilaya ya Magu yenye thamani ya Sh. milioni 17.7, vyote vikiwa ni misaada kutoka Jumuiya ya Ulaya.



CHANZO: NIPASHE
 
Magufuli kweli ni askari wa miavuli. Hana longo longo kama wansiasa wengine. Lakini tatizo lake huwa hajui jimbo lake la uchaguzi liko mkoa gani. Jimbo lake la Chato liko mkoa wa Kagera lakini ni nadra kumsikia akiwa mkoani Kagera. Kila mara yuko Mwanza na miradi yake mingi ni Mwanza.
 
Back
Top Bottom