Magufuli aponda dhana ya polisi jamii dhidi ya majambazi : Waziri Masha na Mwema mpo!

Magezi

JF-Expert Member
Oct 26, 2008
3,359
692
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, John Magufuli, ameiponda dhana ya polisi jamii inayotumiwa na Jeshi la Polisi katika kupambana na uhalifu kwa maelezo kwamba utaratibu huo hauwezi kusadia mapambano dhidi ya ujambazi.

Magufuli amesema haiwezekani kuhubiri polisi jamii kwa jambazi huku wananchi wakiendelea kuumia, kupoteza maisha na mali zao kutokana na vitendo vya ujambazi.

Aliyasema hayo juzi katika ‘mwalo’ (ufukwe) wa Kigangama wilayani Magu kabla ya kuweka jiwe la msingi la mwalo huo pamoja na kuzindua boti ya doria kwa ajili ya kudhibiti uvuvi haramu katika Ziwa Victoria upande wa wilaya ya Magu.

Alisema anaruhusu boti hiyo itumiwe pia na Jeshi la Polisi katika kupambana na vitendo vya uhalifu ziwani na ndipo alianza kuiponda dhana ya polisi jamii.

“…na nimeona hapa kuna OCD, ataitumia pia kupambana na majambazi ili akikimbilia majini, chukueni hii (boti) mfuate huko huko mkamshike. Na msiendekeze sana suala la polisi jamii. Hakuna jamii sana kwa majambazi. Jambazi lishughulikie tu kikamilifu na siyo polisi jamii,” alisema.

Aliongeza: “Kusikia kwa kenge mpaka damu itoke kwenye sikio na kusikia kwa jambazi mpaka damu itoke kwenye sikio. Utaanza kulielimisha jambazi wakati lenyewe zinawazamisha wananchi majini. Unaanza kulielimisha wakati lenyewe lina SMG."

Waziri Magufuli alienda mbali kwa kusema kuwa angekuwa kwenye wizara husika ya Mambo ya Ndani suala la polisi jamii angelizungumzia kwa wananchi wema tu na siyo kwa majambazi kwani hayo yanapaswa kushughulikiwa hasa.

“Wenye kusikia wamesikia. Ningekuwa mimi huko (Mambo ya Ndani) polisi jamii ningeizungumzia kwa wananchi tu lakini kwa jambazi hakuna cha jamii, unamshughulikia kisawasawa. Nasema wasikie na msemakweli ni mpenzi wa Mungu,” alisema.

Aliongeza: “Endeleeni jamii huku watu wanaumia. Unamkuta mtu ana bomu bado una jamii, unamkuta mtu amemchoma mtu amekimbilia majini bado unang’ang’ania jamii. Unamkuta mtu ametega mawe barabarani ana mapanga amekaa bado unang’ang’ania jamii. Sitaki kuingilia wizara nyingine lakini hayo yananikera.”

Aidha, Waziri Magufuli amewatahadharisha wanasiasa watakaoingiza siasa katika mapambano dhidi ya uvuvi haramu kwa lengo la kujipatia kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Aliongeza kuwa wanasiasa bila kujali kama kuna uchaguzi, wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya uvuvi haramu kwani wao kupitia Bunge ndio wamepitisha Sheria Na. 22 ya mwaka 2003 inayopiga marufuku uvuvi haramu kwa lengo la kunusuru samaki wasitoweke katika maziwa, bahari, mito na mabwawa.

Waziri Magufuli aliweka jiwe la msingi katika ujenzi wa mwalo wa kisasa wa Kigangama ambao utakaogharimu zaidi ya Sh. milioni 600 pamoja na kuzindua boti ya doria kwa wilaya ya Magu yenye thamani ya Sh. milioni 17.7, vyote vikiwa ni misaada kutoka Jumuiya ya Ulaya.

CHANZO: NIPASHE
 
Hakika Dr Magufuli unafaa kuwa rais wa nchi hii ambayo inaongozwa na kipofu. Tanzania ikiwa na mawaziri kama Dr Magufuli 5 tu inaweza kufika mbali. Anaona kama vile waziri wa mambo ya ndani anacheza tu pale anaposema...."Wenye kusikia wamesikia. Ningekuwa mimi huko (Mambo ya Ndani) polisi jamii ningeizungumzia kwa wananchi tu lakini kwa jambazi hakuna cha jamii, unamshughulikia kisawasawa. Nasema wasikie na msemakweli ni mpenzi wa Mungu,"

Kwa kweli natamani Dr Magufuli angeweza hata kugombea urais....
 
Hapo chacha ndo muungwanaa anazidii kutokumpangaa kwenye maeneo yenye kuletaa tijaa haraka kwa jamii (barabara, mambo ya ndani, ardhi, madini,nishati).

Dr Magufuli ni action oriented na zaidi anasoma sana na kujipanga vema kwenye utekelezajiiiiii..mapungufu yake ndo utajirii wake wa kibinadamu.
 
JK of course anaprefer kina Pinda-mtoto wa mkulima kina Shein, Lau Masha watu ambao ni dormant kwakweli in so many ways. Anyone who has better education than him and is actually smarter (sio foji foji za mzumbe) na ana charisma jamaa anamuogopa. Salim anaakili lakini hana charisma ya Magufuli. Of course nae ni mjanja mjanja (dont be fooled) alikua anataka uPM sikunyingi infact mpaka sasa anaona mtandao wanamchafulia.. 2015 lazima akaze sema saivi kabanwa hana jinsi inabidi awe mdogo tuu..
 
Na si unajua JK mzee wa kulipiza visasi... lakini ukweli lazima usemwe alimbania sana Magufuli.
 
JK of course anaprefer kina Pinda-mtoto wa mkulima kina Shein, Lau Masha watu ambao ni dormant kwakweli in so many ways. Anyone who has better education than him and is actually smarter (sio foji foji za mzumbe) na ana charisma jamaa anamuogopa. Salim anaakili lakini hana charisma ya Magufuli. Of course nae ni mjanja mjanja (dont be fooled) alikua anataka uPM sikunyingi infact mpaka sasa anaona mtandao wanamchafulia.. 2015 lazima akaze sema saivi kabanwa hana jinsi inabidi awe mdogo tuu..

Mkuu hapo kwenye red umenichekesha sana inamaana mzumbe kidogo hawajatulia kitaaluma? Lakini mbona mzumbe hiyo hiyo imetoa watu wazuri tu??
 
Kihalalli wala hajambania sana kwani hata kumrejeshaa ilikuwaa ni kumpoozaa achelewee kuufikiria ukubwaa (URAISI)

Ila tatizo la aina ya akina magufuli hawajaifunzii chochote kutokana na historiaa..Ni mhanga mkubwaa wa mtandao japo yumo ndani ya Baraza.
 
Magufuli ndiye so far ninayemuona kuwa na uwezo wa kuipeleka nchi hii mbele na sisi tukawa na GDP kama Botswana au hata vinchi vya central europe ndani ya terms mbili za Urais.
 
Jmushi;atakwenda na serikali 2010-2015,itakuwa hivi:
Rais:Salim Salim
Makamo:Warioba
Waziri Mkuu:Magufuli
Mambo ya nje:Mwakyembe...
Halafu 2015,Salim atataka aendelee,wakati Warioba atapumzika na Magufuli ataendelea kuwa PM mpaka 2020 atakapoachia ngazi Salim,kisha atachukua fomu ya Uraisi na kuwa presidaa to 2030!!!Kama Sheikh Hussein vile,tehe tehe tehe!
 
Sasa hii unataka kusema kama Putin na Medeved.
Lakini ukweli unabakia pale pale wote waliotajwa hapo hamna kitu zaidi ya Magufuli. Magufuli ndiye pekee atayeweza kututoa kwa wakati huu, Tz ya leo haiitaji Rais anayetumia busara nyingiiiiiiiiiiii kufanikisha kitu kidogo. Tunamhitaji magufuli kuwa Rais .
 
Mkuu hapa umeunga unga... Magufuli ametumia Busara kuelewa makosa haya, hakutumia mitulinga. Mafanikio siku zote huja baada ya kutoa maamuzi wa busara, mafanikio ya kazi hutekelezwa na wafuasi wako.
 
Mkamap;soma post yangu namba 8 kwanza.Hiyo uliyo quote ilikuwa ni kuchangamsha baraza,japo katika siasa lolote linaweza kutokea.
Lakini hata hivyo kwa demokrasia changa kama yetu,bado Magufuli anahitaji kujengwa/kujijenga zaidi ili aje aukwae Urais.Anahitaji apewe nafasi nyingine yakumng'arisha zaidi.Kama anafikiria kupigana hukohuko ndani ya CCM,bado anahitaji kujiwekea mizizi ndani ya chama kama wenzake kina Lowasa na Membe.Magufuli anategemea utendaji wake mzuri umvushe,lakini kama nilivyosema kwa siasa za CCM hili halitamsaidia sana.
 
Yeah! wenye uwezo tunawaweka pembeni, Magufuli ndo anauwezo wa kutuliza ghasia yote hasa ya rushwa na kuweka displini ya uongozi, wengine nafikiri hawataweza maana watajidai kufuata sheria sana na wakati huko kwenye sheria kuko corrupted vibaya sana. Huwezi mpeleka Lowasa ktk mahakama ukategemea ushindi sanasana utamlipa wewe fidia kwa mahakama zetu.

tunahitaji NONSENSE leader kwa wakati huu.
 
...Salim anaakili lakini hana charisma ya Magufuli. Of course nae ni mjanja mjanja (dont be fooled) alikua anataka uPM sikunyingi infact mpaka sasa anaona mtandao wanamchafulia.. 2015 lazima akaze sema saivi kabanwa hana jinsi inabidi awe mdogo tuu..

Salim 2015?

Salim huyo mzee ameanza uongozi alivyo balehe tu, alikuwa ubalozini mwaka 1961 akiwa na miaka 19, niko vidudu huyu mzee waziri mkuu, mpaka leo wa nini hawa kina babu hawa?

Magufuli nae anachemsha kama Mrema.
 
Mrema hakuchemsha bali alipingana na sera za kifisadi za CCM za kulindana. CCM hawataki msema ukweli kwani ni chama kinchoendeshwa kwa uongo lakini siku zote njia ya muongo ni fupi.
 
Back
Top Bottom