Magufuli apeleka Sh1bn Loliondo, apata kikombe cha babu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magufuli apeleka Sh1bn Loliondo, apata kikombe cha babu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Saint Ivuga, Apr 1, 2011.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Apr 1, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,496
  Likes Received: 19,903
  Trophy Points: 280
  Magufuli apeleka Sh1bn Loliondo
  [​IMG]
  Neville Meena na Mussa Juma,

  Samunge; WAZIRI wa Ujenzi, Dk John Magufuli, jana aliingia katika Kijijini Samunge kwa mchungaji Ambilikile Masapila na kupata kikombe cha dawa, kisha kutangaza neema ya kujengwa kwa barabara kuu inayoingia kijijini hapo.

  Magufuli aliuambia umati wa watu uliokuwa ukisubiri zamu yao kunywa dawa kuwa, Serikali itatumia Sh1.05 bilioni kwa ajili kutengenenza barabara hiyo ili iweze kupitika wakati wote kwa lengo la kuwarahisishia usafiri wanaokwenda kunywa dawa kwa Babu Masapila.

  Barabara inayoingia katika kijiji hicho ambacho kimeshuhudia maelfu ya magari yakiingia kila siku tofauti na ilivyokuwa awali, ipo katika hali mbaya kiasi cha baadhi ya maneo kutoruhusu magari kupishana.

  Kwa mujibu wa Magufuli, Serikali ilikwishatoa Sh500/-milioni kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo kuanzia Mto wa Mbu eneo la Kigongoni, Ngaresero, Samunge hadi kuungana na barabara ya kutoka mkoani Mara.

  Dk Magufuli alisema jana ndio aliuagiza uongozi wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads) Makao Makuu kutuma Sh500 milioni ili kuharakisha ujenzi huo.

  "Tayari fedha hizo zimeshatumwa Tanroads mkoani Arusha na Meneja wa Mkoa, Kakoko (Deodatus), niko naye hapa hivyo kazi itakwenda haraka ili watu wanaokuja kwa mchungaji kunywa dawa wasiendelee kuteseka," alisema Dk Magufuli huku akishangiliwa na mamia ya watu waliokuwa wakimsikiliza.

  Waziri pia huyo alisema kwa mamlaka aliyonayo, atawasiliana na uongozi wa Mfuko wa Barabara ili utume fedha za dharura kiasi cha Sh50 milioni kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorogoro kwa ajili ya kufanya matenegenezo mengine ya barabara, wilayani humo.

  Alisema fedha zilizotengwa kwa ajilii ya barabara za nchi nzima kupitia mfuko huo zinafikia Sh286 bilioni katika bajeti ya mwaka 2010/11, na kwamba upo uwezekano mkubwa wa fedha za dharura kupatikana kwa ajili ya matenegenezo ya barabara ya Samunge.

  Matengenezo
  Kwa mujibu wa Magufuli, matengenezo ya barabara hiyo ni muhimu sana kwani awali barabara hiyo kuanzia Mto wa Mbu ilikuwa ikipitisha magari kati ya 20 na 25 kwa siku lakini, sasa yameongezeka hadi 3,500 kwa siku.

  "Nasema barabara hii ni muhimu sana hivyo nakuagiza Meneja wa Tanroads mkoa wa Arusha kuhakikisha mkandarasi aliyepewa kazi ya kutengeneza barabara hii anafanya kazi usiku na mchana ili ikamilike, akizembea fukuza," alisema Magufuli na kuongeza:

  "Sheria namba 17 ya mwaka 1997 na vifungu vyake inatoa mamlaka ya kuondolewa kwa mkadarasi anayezembea. Pia sheria inaelekeza kufikishwa mahakamani kwa wakandarasi wa aina hiyo, na akitiwa hatiani na anaweza kufungwa miaka mitano. Hivyo basi sheria ipo na pale tutakapolazimika tutaitumia".

  Magufuli aliuagiza uongozi wa Halmashauri ya Ngorogoro kuwasilisha maombi ya dharura ya fedha za matengenezo ya barabara katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) ili kuwezesha matengenezo ya barabara nyingine kufanyika.

  "Tukiacha barabara ya kuja huku, nimetembelea barabara zenu katika wilaya ya Ngorongoro, kwa kweli ni mbaya sana hivyo zinahitaji matengenezo,"alisisitiza.

  Juzi Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Eliasi Ngorisa, aliliambia Mwananchi kwamba halmashauri yake ilikuwa imeomba kiasi cha Sh400 milioni kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya kuifanyia matengenezo ya dharura barabara zinazoingia kijijini Samunge.

  Dk Magufuli pia alimwelekeza Meneja wa Tanroads mkoani Arusha kuandaa mpango wa matengenezo ya barabara za Ngorongoro na kuwasilisha mapendelezo yake serikalini kwa ajili ya utekelezaji wake.

  "Kaandike mpango huo sasa na ulete ili tuone jinsi ya kufanya, kama hujui kuandika tafuta watu wakusaidie," alisema Magufuli na kusababisha umati wa watu
  kuagua kicheko.

  Waomba msaada
  Tofauti na viongozi wengine waliowahi kufika kwa mchungaji Mwasapila, Waziri Magufuli aliruhusu maswali kutoka kwa wananchi waliokuwa wakimsikiliza.

  Wengi wao walilalamikia hali mbaya ya mazingira. "...pamoja na kwamba wewe si Waziri wa Afya, lakini tunajua unatoka Serikalini, tunaomba utusadie maana afya zetu zipo hatarini. Huwezi kuamini kwani huko barabarani unakuta mtu anajisaidia haja kubwa hapo,na mtu mwingine anakula chakula, kwa kweli hali ni mbaya tunaomba msaada,"alisema Nicholas Mwangoka.

  Akijibu hoja hiyo, Waziri Magufuli alisema atawasilisha taarifa yake kwa Waziri Mkuu ambaye yupo mkoani Arusha na kwamba anaamini kupitia njia hiyo waziri wa sekta ya afya atafikishiwa ujumbe ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa.

  Mapema mchungaji Mwasapila kupitia kwa msaidizi wake, aliomba Serikali ijenge daraja katika mto wa Samunge ambao umekuwa kikwazo cha magari kuingia kijijini hapo kwani hufurika kila mvua zinaponyesha.

  Pia mchungaji huyo alimshukuru Waziri huyo kwa ahadi aliyoitoa akisema kuwa hatua hiyo inamtia moyo kuendelea kutoa tiba kwa wagonjwa wanaofika nyumbani kwake.

  "Nakushukuru sana kwa ujio wako na yale uliyoyasema, unatupa matumaini,unatupa moyo, asante tunashukuru sana," alisema Masapila.

  Foleni yapungua Samunge
  Katika hatua nyingine, foleni ya magari ambayo ilikuwa zaidi ya kilometa 30 kutoka eneo analotolea tiba mchungaji Masapila sasa imepungua.

  Kupungua kwa foleni hiyo kumetokana na utaratibu mpya wa kuingiza magari katika kijiji cha Samunge ambao unatarajiwa kuanza leo, pia kutokana na kasi ya mchungaji huyo katika kugawa dawa.


  Tacaids yawaasa wagonjwa
  Ellen Manyangu anaripoti kutoka Dar es Salaam kuwa, Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (Tacaids), imewataka wagonjwa waliokunywa dawa ya Mchungaji Masapila kutoacha kuendelea na dozi walizopewa hospitalini kwa kuwa dawa hiyo haijathibitika kutibu Ukimwi.

  Mratibu wa tume hiyo Dk Bwijo Bwijo alisema jana kuwa utafiti bado unaendelea kujua endapo kikombe hicho cha babu, kinaweza kutibu magoonjwa yanayoelezwa.

  Alisema hayo jana alipokuwa akizungumza katika mjadala ulioandaliwa na Kituo cha Radio Clouds FM na kufanyika katika hoteli ya Kempisky jijini Dar es Salaam jana asubuhi.

  Akizungumza katika mjadala huo, Dk Bwijo alisema dawa ya Mchungaji Masapila bado inafanyiwa utafiti ili kuthibitisha kama inatibu, hivyo wananchi hawapaswi kuacha kutumia dawa za kitabibu ghafla.

  Kwa mujibu wa Bwijo, jitihada za kuthibitisha ubora wa dawa hiyo bado zinaendelea kwa ufadhili wa Shirika la Afya Duniani (WHO) na Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Kudhibiti Ukimwi (UNAIDS).

  "Wagojwa wote walioko kwenye matibabu ya dawa za kitaalamu na wamekunywa kikombe cha dawa ya babu wasiache kutumia dawa zao mpaka itakapothibitishwa kuwa dawa hiyo ni halali na inatibu," alisema Dk Bwijo.

  Mwenyekiti Mstaafu wa Mtandao wa Wanaoishi na Ukimwi Afrika (TANEPHA), Alex Margery, alisema suala la Loliondo limejaa sura ya Ukimwi na kutahadharisha kuwa watu wasiache kutumia dawa za kitaalamu kwa kuwa dawa ya babu bado haijathibitishwa.

  Alisema walishajitokeza watu mbalimbali katika nchi za Kenya na Afrika Kusini na kutoa dawa zilizoaminika kuwa zinatibu maradhi sugu ikiwemo ukimwi, lakini baadaye zilisababisha watu wengi kufa kutokana na kuacha kutumia dawa za kitaalamu kwa imani kuwa wamepona.

  "Hili ni jambo la hatari sana hasa kwa jamii yetu kwani wagonjwa wanaacha kutumia dawa za kisayansi zilizothibitishwa kutibu, au kupunguza makali ya maradhi waliyonayo kwa imani kikombe cha dawa wanachopewa Loliondo kinawaponyesha…, "alitahadharisha Margery.

  Aliongeza dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi ARV zilikuwa katika dozi kubwa ya vidonge 14 kwa siku moja, lakini kadri siku zinavyoongezeka dozi hiyo inapungua na hivi sasa ni kidonge kimoja kwa siku.
  Mtaalam wa Afya ya Jamii na Ukimwi, Dk Bennect Fimbo, alisema awali ugonjwa wa Ukimwi ulikuwa tishio kwa jamii kwa vile hawakuwa na uhakika wa mtu kuishi nao muda mrefu lakini, hivi sasa mtu anaweza kuishi nao kwa muda wa miaka 20.

  Aliongeza kuwa mti wa Mugariga unaotumiwa na babu kama dawa umefanyiwa utafiti kwa muda mrefu, hivyo inapaswa uchunguzi wa ziada ufanyike ili kubaini mti huo unatibu magonjwa yapi na dozi yake.

  Kandoro aweka udhibiti
  Kutoka Mwanza Frederick Katulanda na Sheila Sezy wanaripoti kuwa, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro, amewaagiza wasafirishaji wa watu wanaokwenda kutibiwa kwa Mchungaji Masapila kuwaorodhesha watu wote ili kuweka kumbukumbu.

  Akizungumza jana katika kikao chake na wamiliki a mabasi, Kandoro alisema Serikali imepanga utaratibu maalum ikiwa ni pamoja na kuweka vizuizi kwa lengo la kupunguza msongamano na kuwezesha wagonjwa kumfikia babu haraka zaidi.

  Alisema Serikali imetambua kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la watu wanaoenda Loliondo kwa ajili ya matibabu hayo hivyo utaratibu huo mpya utasaidia kupunguza msongamano.

  Alifahamisha kuwa kuanzia sasa magari yote yanayotoka Mwanza na Kagera na wageni kutoka nchi za Rwanda, Uganda na Burundi kwenda Loliondo, wanapaswa kujiandikisha jijini Mwanza na kuacha majini yao katika kizuizi cha Magu.

  Magari yatakayoruhusiwa kuondoka na kupita katika vizuizi ni yale yenye nguvu maalumu (four wheel drive) na mbasi. Malori ya aina yote hayaruhusiwi kwenda huko, alisema.

  Akizungumzia suala la nauli kuwa juu, Kandro alisema serikali haitaingilia utozaji wa nauli bali kuhakikisha inaboresha mazingira ya Loliondo na kwamba nauli zitashuka zenyewe
   
 2. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #2
  Apr 2, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  mzee wa amri barabara itajengwa faster sana
   
 3. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #3
  Apr 2, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Hongera tacaids!
   
 4. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #4
  Jul 21, 2015
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,670
  Likes Received: 21,902
  Trophy Points: 280
  Miaka michache iliyopita kulizuka hadaa kuwa huko Loliondo yupo Babu mmoja anatibu na kutoa kina ya maradhi mbalimbali kama Ukimwi, BP, nk nk kwa tiba ya "kikombe".
  Watu wengi wepesi wa akili na kuhadaika kirahisi walijazana huko huku wakiwaaminisha wengine kuwa ile ilikuwa ni tiba madhubuti. Lakini baadae hata wataalamu walidhibitisha kuwa ile ilikuwa HADAA tuu.
  Mmoja wa watangaza nia kugombea Urais Mhe Magufuli alifumwa na kamera akifakamia kikombe kama tiba ya maradhi ambayo haya julikani.
  Ile ilikuwa hadaa, jee huyu akipewa nafasi ya juu zaidi ataweza kuzishinda hadaa za wajanja?
  ImageUploadedByJamiiForums1437474440.502759.jpg
  Hawa ni viongozi wenzake walioshiriki kupata kikombe
  ImageUploadedByJamiiForums1437474483.637311.jpg
  ImageUploadedByJamiiForums1437474497.516719.jpg
   
 5. MADAM T

  MADAM T JF-Expert Member

  #5
  Jul 21, 2015
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 3,675
  Likes Received: 943
  Trophy Points: 280
  Unamchakaza!
   
 6. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #6
  Jul 21, 2015
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,670
  Likes Received: 21,902
  Trophy Points: 280
  Hapana mkuu, nataka tujiulize tuu
   
 7. M

  Mchili JF-Expert Member

  #7
  Jul 21, 2015
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hii imetoka wapi hapa leo? unataka kutuambia nini
   
 8. Nkobhe

  Nkobhe JF-Expert Member

  #8
  Jul 21, 2015
  Joined: Jan 26, 2015
  Messages: 453
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  unafiki huo Wa cdm mmeanza
   
 9. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #9
  Jul 21, 2015
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,481
  Likes Received: 788
  Trophy Points: 280
  Hapana huo sio unafiki kama ni unafiki tuwekee picha ya Mbowe, Dr.Slaa, Tundu Lissu, Mnyika wakiwa Samunge kwa babu wakinywa hiyo dawa
   
 10. Baba Mbwa

  Baba Mbwa JF-Expert Member

  #10
  Jul 21, 2015
  Joined: May 31, 2015
  Messages: 717
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 60
  duuh! babu yupo?
   
 11. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #11
  Jul 21, 2015
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,071
  Likes Received: 7,553
  Trophy Points: 280
  Serikali nzima ilipiga kikombe cha babu. Mkuu yeye alitangulia kimya kimya kabla haijawa aired to the public.
   
 12. N

  NOD JF-Expert Member

  #12
  Jul 21, 2015
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 388
  Likes Received: 251
  Trophy Points: 80
  On a serious note, ni vigumu Tanzania kuendelea mbele kama una viongozi wenye ufinyu wa mawazo kama hawa. Mara wako Nigeria, mara hili, mara lile, just to show you that we still have a long way to go and move Tanzania forward especially being blessed with all the resources we have. It is painful kama kweli kuna a visionary leader and serious one for the future of our country to think beyond cheap politics and small mind of this level. Hawa sio wagonjwa physically but mentally and spiritually which is a main requirement for leaders who can move Tanzania from where it is now to the next level. I am afraid to say we have another ten years of nothing regardless of the good natural environment to support positive growth and changes in our country.

   
 13. m

  mikeimani JF-Expert Member

  #13
  Jul 21, 2015
  Joined: Jun 20, 2015
  Messages: 1,984
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Zilipoanza taarifa za uwepo wa hicho kikombe na maajabu yake nilipinga. Na nikaawaambia watu time will tell. And time has told.

  Kama haina madhara kwa afya haina tatzo. Wanasiasa mara ingine ni watu wa aina hii
   
 14. hazole1

  hazole1 JF-Expert Member

  #14
  Jul 21, 2015
  Joined: Jan 3, 2015
  Messages: 3,964
  Likes Received: 3,092
  Trophy Points: 280
  Huyu mzee ivi anaumwa ugonjwa gani? au ndio haya magonjwa ya kisasa kwasababu yule mzee huwa simuelewagi anahasira za ajabu ajabu unaweza ukute tayari anakakichwani
   
 15. k

  kanone JF-Expert Member

  #15
  Jul 21, 2015
  Joined: Oct 10, 2013
  Messages: 6,197
  Likes Received: 373
  Trophy Points: 180
  mpumbavu wewe, kamwabie kilema wa mkono slaa ndo akanywe kikombe sio jembe letu magufuli,
  mpuuzi mkubwa
   
 16. k

  kanone JF-Expert Member

  #16
  Jul 21, 2015
  Joined: Oct 10, 2013
  Messages: 6,197
  Likes Received: 373
  Trophy Points: 180
  ni kilema wa mkono ndo ugonjwa wake huyo mzee,
   
 17. k

  kanone JF-Expert Member

  #17
  Jul 21, 2015
  Joined: Oct 10, 2013
  Messages: 6,197
  Likes Received: 373
  Trophy Points: 180
  nafikiri ungetuwekea picha za yule kilema wa mkono anaanguka chooni na kiarusi juu tungekuelewa.
   
 18. N

  Ndusty JF-Expert Member

  #18
  Jul 21, 2015
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  Suala ni kwamba Magufuli akiwa kama waziri wa ujenzi kipindi hicho kuidhinisha mabilioni ya fedha kwa ajili ya barabara ya kwenda kwa mganga wa kienyeji haikuwa sahihi.kama serekali ilitengeneza hiyo barabara kutoka mto wa mbu mpaka samunge yuko wapi huyo mzee wa kikombe kwa sasa?kama hayupo ile barabara ina umuhimu gani kwasasa kama ilijengwa kwa kusaidia wanaokwenda kupata kikombe?mbona kuna vijiji vyenye uhitaji wa barabara nzuri za kusafirisha mazao yao ambayo ni muhimu kwa manufaa ya wananchi na serekali lakini hawajawahi kujengewa barabara.na haya mazao yapo kila mwaka na yataendelea kuwepo.kwanini magufuli alisisitiza kujenga barabara ya kwenda samunge huku akijua kabisa kikombe cha babu kilikuwa ni usanii tuu?leo anataka tumpe uraisi...really??????????like i said before kwa wana JF,waongo,wafitini,walaghai,mafisadi nk wataisikia ikulu kwenye bomba..be blessed and GOD bless Tanzania!
   
 19. h

  honoget JF-Expert Member

  #19
  Jul 21, 2015
  Joined: Aug 16, 2013
  Messages: 1,720
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  huyu anaumwa ufisadi na ukurupukaji
   
 20. Mmawia

  Mmawia JF-Expert Member

  #20
  Jul 21, 2015
  Joined: Aug 20, 2013
  Messages: 56,571
  Likes Received: 21,661
  Trophy Points: 280
  Hivi magufuri kitendo cha kwenda kupata kikombe kwa babu mwasapile kule samunge alipona au hakupona,nakama hakupona anatwambiaje kuhusu afya yake?
   
Loading...