Yaliyojiri wakati wa hafla jiwe la msingi ujenzi wa meli mpya, chelezo na ukarabati wa meli Ziwa Victoria za Mv Victoria na Mv Butiama

elivina shambuni

JF-Expert Member
May 31, 2018
461
295
1575788435447.png


WATU na taasisi wameguswa na uamuzi wa serikali kujenga daraja la aina yake la Kigongo-Busisi wilaya Misungwi kwa kumhakikishia Rais John Magufuli kuwa naye bega kwa bega wakimsihi aendelee kuchapa kazi bila kujali kelele.

Aidha, daraja hilo refu kuliko yote katika Afrika Mashariki na la sita katika Afrika, limeelezewa kwamba litakapokamilika, wanaovuka watatumia dakika nne badala ya saa mbili na nusu zinazotumika sasa kuvuka kati ya Kigongo na Busisi kutokana na wingi wa magari.

Hayo yalielezwa jana Rais Magufuli alipoweka jiwe la msingi la mradi huo ambao Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (Tanroads), Patrick Mfugale alieleza serikali ilivyoanza muda mrefu na namna wafadhili walivyogoma kuanza ujenzi. Miongoni mwa waliopewa nafasi na Rais Magufuli kuzungumza ni Mbunge wa Misungwi, Charles Kitwanga aliyemwambia, “Mungu akujalie afya njema na sisi tulio pembeni tuko pamoja na wewe tutakufia.

” Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mwanza, Anthony Diallo alimuomba Rais Magufuli kuendelea kuchapa kazi akisema, “sisi tupo nyuma yako tutakutetea mahala ambapo kutakuwa na matatizo.” Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema mradi huo ni historia kubwa na unathibitisha uthubutu wa hali ya juu.

Akielezea daraja hilo, Mtendaji Mkuu wa Tanroads, Mfugale alisema daraja litafupisha urefu wa eneo hilo la Busisi na Kigongo linalotenganishwa na Ziwa Victoria hivyo badala ya saa mbili na nusu, watu na magari yatatumia dakika nne. Daraja litakuwa na urefu wa kilometa 2.3, upana wa meta 28.45 na litakuwa la njia nne. Litakuwa na nguzo 67 na likikamilika litakuwa na ubora kwa zaidi ya miaka 100 ijayo.

Daraja hilo litajengwa na kampuni ya CCECC na China Railway Construction Engineering Group (CRCEG) zote za China kwa gharama ya Sh bilioni 699.2 likitarajiwa kukamilika baada ya miaka minne. Litakamilika baada ya miezi 48; ni pamoja na muda wa kujiandaa wa miezi mitatu.
 
SERIKALI mkoani Tabora imetoa muda wiki mbili kwa Kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) kuhakikisha wamelipa adhabu ya milioni 40 wanazodaiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) baada ya kuchelewesha michango ya watumishi wao.

Kauli hiyo imetolewa jana katika Kijiji cha Karangasi wilayani Uyui na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri baada ya kutembelea Kampuni hiyo ili kutatua mgogoro uliokuwepo baina yao na wafanyakazi kuhusu michango ya NSSF.
Alisema ndani ya kipindi hicho Kampuni hiyo inatakiwa kushirikiana na NSSF, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) na Ofisi yake kuhakiki orodha ya watumishi wa kampuni hiyo ambao wanafanyakazi mkoani Tabora ili kuwa na uhakika wa malipo ya NSSF yanayopaswa kulipwa kila mwezi.

Mwanri alisema ndani ya kipindi hicho Kampuni ya CCECC itakiwa kuandaa mikataba ya watumishi wao na kuwasilisha makato na michango kwa ajili ya NSSF za watumishi wao wanayodaiwa na nakala ya vibali vya watumishi wa nje wanaofanyakazi Mkoani humo.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema ni jukumu la Kampuni zozote zinazotekeleza majukumu yake mkoani humo kuhakikisha zinazingatia Sheria za Nchi ikiwemo ya kuwasilisha michango ya asilimia 10 anazokatwa mtumishi na asilimia 10 anayopaswa kumchangia na kulipa asilimia 1 kwa ajili ya WCF. Alisema nje ya hapo mwajiri huyo atahesabika anavunja Sheria za Nchi.

Naye Meneja wa NSSF Mkoa wa Tabora Shimo Mussa alisema Kampuni hiyo imekuwa ikitoa taarifa za uongozi na hivyo kuwasababishia kupoteza rasilimali za Shirika ikiwemo matumizi ya muda na mafuta kufuatilia michango ya watumishi.
Aliongeza kuwa wakati mwingine wamediriki kujificha pindi wanapogundua kuwa watumishi wa NSSF wanakwenda kufuatilia michango na stahili za watumishi.

Mussa alisema Kampuni hiyo ya CCECC iliwasilisha orodha ya watumishi zaidi ya 530 lakini ambao michango yao imefikishwa kwenye Shirika na tena kwa kuchelewa ni milioni 76 ambayo ni sawa na wafanyakazi 126.
Alisema kwa takwimu hizo zaidi ya wafanyakazi 400 hawajulikani walipo na michango yao bado hajapelekwa na kuongeza kuwa ni jukumu la mwajiri yoyote anapokuwa amepunguza watumishi kuandika barua NSSF.
Baadhi ya watumishi walidai wamefanyakazi miezi zaidi ya minne lakini hawana mikataba ya kazi, michango yao ya NSSF inakatwa lakini haiwasiliswi sehemu husika, hawalipwi masaa ya ziada ya kazi na Mwajiri amekuwa akiwabagua wakati wa utoaji wa huduma matibabu.

Kampuni ya CCECC inakazi ya kukarabati reli ya Kati kutoka Dar es salaam hadi Isaka mkoani Shinyanga.@elivina shambuni,
 
elivina shambuni, Sawa nijambo nzuri sana kupata maendeleo ila hicho nikipaumbele cha kanda ya ziwa kuna tatizo makubwa la kuvuka hapo kweli kiasi kwamba nchi itumie karibu 700bn......ambozo ingeziweka kwenye kilimo au afya na elimu hizo wilaya zingefaidika kuliko dalaja la kuvuka mgambo wakati kuna vivuuko zaidi ya vitano hapo busisi na Kamanga vipo vivuko.....
 
badala ya saa mbili na nusu zinazotumika sasa kuvuka kati ya Kigongo na Busisi


Sad

Nilivuka hapo kwa kama sikosei 30 minutes mwaka 2003, lakini sasa mtu anayetoka Mwanza kwenda Shy anasafiri muda sawa na huyo wa Kigongo - Busisi
 
Maccm yana kiwanda cha ku manufacture tonnes za uongo
Wakati tuko ndani ya ccm tulikuwa tunashangilia tu na kupiga vigelegele sasa tuko upinzani ndio tunaiona hiyo taasisi inavyomhujumu mtanzania.
 
Sad

Nilivuka hapo kwa kama sikosei 30 minutes mwaka 2003, lakini sasa mtu anayetoka Mwanza kwenda Shy anasafiri muda sawa na huyo wa Kigongo - Busisi
Kwasasa kwa ferri mpya ambayo imegharimu pesa kubwa nidakika 15-20tu kuvuka sasa hiyo ferri mpya pamoja na kugharimu pesa nyingi itakaa bila kazi dalaja likiisha hiyo ndo poor economic planning ya nchi hi
 
Sawa nijambo nzuri sana kupata maendeleo ila hicho nikipaumbele cha kanda ya ziwa kuna tatizo makubwa la kuvuka hapo kweli kiasi kwamba nchi itumie karibu 700bn......ambozo ingeziweka kwenye kilimo au afya na elimu hizo wilaya zingefaidika kuliko dalaja la kuvuka mgambo wakati kuna vivuuko zaidi ya vitano hapo busisi na Kamanga vipo vivuko.....
Ni lazima kuwekeza kila mahali. Hata kwenye miundo mbinu na afya kunahitaji uwekezaji.
 
Kwasasa kwa ferri mpya ambayo imegharimu pesa kubwa nidakika 15-20tu kuvuka sasa hiyo ferri mpya pamoja na kugharimu pesa nyingi itakaa bila kazi dalaja likiisha hiyo ndo poor economic planning ya nchi hi
Maeneo yanayohitaji feri ni hapo tu nchi nzima. Daraja la kilombero lilipoisha feri ilizamishwa? Baada ya daraja la kigamboni kuisha feri haipo tena.?
 
Ni lazima kuwekeza kila mahali. Hata kwenye miundo mbinu na afya kunahitaji uwekezaji.
Mkuu hapa naongelea kipaumbele katika wilaya husika hizo sengerema na miswingwi hali yao ya uchumi ni mbaya na raia wao masikini sana.....kuliko hilo dalaja wangeziweka hizo pesa kwenye miradi ambayo inagusa maisha ya watu walio wengi
 
1575791112871.png


RAIS John Magufuli ameweka jiwe la msingi katika mradi wa daraja la Kigongo-Busisi wilaya ya Misungwi na kusema ujenzi wake ni uthibitisho mwingine kwamba nchi si masikini bali watanzania wakiamua wanaweza.

Alisema Sh bilioni 699.2 za mradi huo ni kodi za wananchi zinazoimarisha uhuru wa nchi na kufanya iheshimike duniani kutokana na kufanya uamuzi wake yenyewe. Magufuli ambaye alieleza alivyonusurika kufa maji katika eneo hilo katika miaka ya 1990, alisema wapo watu waliopoteza maisha kwa kuzama majini kutokana na ajali za mitumbwi wakivuka baada ya feri kuharibika.

Aidha, katika uzinduzi huo uliofanyika eneo la Kigongo-Busisi mkoani Mwanza, Rais Magufuli amehimiza Watanzania kutunza amani akisema maendeleo yaliyopo ni matokeo ya kushikamana. Tanzania tajiri “Kwangu ujenzi wa daraja hili ni uthibitisho mwingine kwamba nchi yetu si masikini na watanzania tukiamua tunaweza,” alisema Rais Magufuli akisisitiza Watanzania kutembelea kifua mbele kwa kuwa fedha zinazotumika ni kodi zao.

Alisisitiza, “Sh bilioni 699.2 ni fedha nyingi na zote zimetolewa na serikali yenu, hatujaomba mkopo, hatujaomba msaada, hatujampigia magoti mtu, hatujamlilia mtu, ni fedha zenu Watanzania.” Rais alisema kodi zinazokusanywa ndizo zinatumika kujenga reli, kutoa elimu bure, zilizojenga zaidi ya vituo 352 vya afya, bwawa kubwa la Nyerere litakalozalisha megawati za umeme 2,115. “Ndiyo maana nimekuwa nikiwaambia tutembee kifua mbele, sisi Watanzania ni matajiri siyo masikini,” alisema.

Alihimiza wananchi kulipa kodi na kusisitiza kwamba licha ya kuwezesha kutekeleza miradi ya maendeleo na kijamii, pia zinaimarisha uhuru wa nchi na kufanya iheshimike duniani.

“Kutokana na kodi zetu, tunafanya maamuzi sisi wenyewe.” Magufuli alivyonusurika Akizungumzia umuhimu wa daraja hilo la Busisi- Kigongo, Rais Magufuli alirejelea tukio la miaka ya 1990 ambalo watu 12 wa familia moja walikufa maji wakati wakivuka kwa mitumbwi baada ya kivuko kilichokuwapo kupata matatizo. “Siku feri ilipokuwa ikiharibika ni lazima upande mitumbwi,” alisema.

Akisimulia alivyonusurika, Magufuli alisema alipofika Busisi, aliambiwa feri ya MV Geita iliyokuwa ikitoa huduma katika eneo hilo imeharibika na kushauriwa apande mtumbwi umvushe hadi ng’ambo (Kigongo). Kwa mujibu wa Rais, alizingatia kwamba hana uzoefu wa kuogelea, asingeweza kuvuka kwa mtumbwi hivyo aliamua kuzunguka kwa kupita kivuko cha Kamanga.

Alisema alipofika Mwanza mjini, aliambiwa miongoni mwa watu waliopanda mitumbwi siku hiyo, watu zaidi ya 12 walifariki wakati wakivuka. Licha ya vifo vya ajali mitumbwi, Rais alisema wapo wengine (wagonjwa) kutoka maeneo mbalimbali kwenda Hospitali ya Bugando, Mwanza walipoteza maisha wakisubiri feri kabla ya kuvuka baada ya kukuta ama haipo au imeharibika. Waliodhani haiwezekani Akieleza uamuzi wa kujenga daraja hilo, Magufuli alisema unatokana na ahadi alizotoa mwaka 2015 wakati akiomba kura.

Alisema, “nikiwa uwanja wa Kirumba (Mwanza) nikiomba kura, nilisema nitajenga daraja na wapo ambao walisema hili haliwezekani.” “Wapo watu ambao hawakuamini hiki,” alisema na kusisitiza kuwa alitoa ahadi hiyo akiamini kwamba itawezekana kwa kuwa tayari kulikuwa na madaraja makubwa 77 yaliyokwishajengwa nchini na isitoshe, walioshiriki walikuwapo miongoni mwao akiwa ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (Tanroads) Mfugale aliyeandaa michoro ya madaraja mbalimbali.

Akimshukuru Mfugale kwa kuandaa mchoro wa daraja hilo la Busisi-Kigongo haraka baada ya kutakiwa kufanya hivyo, Magufuli alisema, “nashukuru kwa kutangaza haraka zabuni hii kwa sababu wangechelewa wakasubiri urais wangu ukaisha, ajeye angeweza kufuta huu mradi.”

Alipongeza pia Bunge chini ya Spika Job Ndugai akisema lilipopelekewa mapendekezo, mradi ulipitishwa. Akieleza furaha ya mradi huo, Magufuli alisema mafanikio yanatokana na kuminya fedha za mafisadi. Rais Magufuli alisisitiza kuwa ni mtumishi wa Watanzania na ataendelea kutumika kadri wanavyoona anafaa.

Alisema miradi mbalimbali inayotekelezwa ni matokeo ya ushirikiano wa pamoja. Tutunze amani “Maendeleo tunayoona yanaendana kwa sababu tumeamua kushikana pamoja, vyombo vya ulinzi na usalama vinafanya kazi,” alisema na kuhimiza Watanzania kutunza amani kwa kuepuka kubaguana kwa misingi ya dini, sura au hali.

Alisema wakati nchi ikijiandaa kusherehekea miaka 58 ya uhuru (wa Tanganyika) kesho, wananchi hawana budi kudumisha amani na upendo maendeleo yaendelee kuonekana. “Penye amani pana maendeleo.” Ataka kasi ya ujenzi Alimtaka wakandarasi , Kampuni ya CCECC kutoka China na China na China Railway Construction Engineering Group (CRCEG) kujenga usiku na mchana ukamilike mapema. “Naomba makandarsi wasimamie vizuri mradi huu, hizi ni fedha za Watanzania masikini.

Fedha yao waliyokusanya wameamua kuweka uwekezaji hapa ndiyo maana nawaomba wakishaanza, kwa sababu fedha ya kulipa asilimia 50 tayari ipo imewekwa. Fedha ya kulipa fidia nayo ipo,” alisema.

Fidia kupisha mradi Rais Magufuli alisisitiza kwamba wote watakaoguswa na mradi huo watalipwa fidia na kusema zaidi ya Sh bilioni 3.145 zimetengwa kwa ajili hiyo ya wanaostahili; ambao ni waliofuatwa na barabara. Mradi huo ni kiungo muhimu cha usafiri kati ya Mwanza na mikoa mingine ya kanda ya ziwa pamoja na nchi jirani ikiwamo Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Uganda. Utakapokamilika utachochea shughuli za uzalishaji hususani kilimo, uvuvi, ufugaji, biashara na utalii.
 
Kwasasa kwa ferri mpya ambayo imegharimu pesa kubwa nidakika 15-20tu kuvuka sasa hiyo ferri mpya pamoja na kugharimu pesa nyingi itakaa bila kazi dalaja likiisha hiyo ndo poor economic planning ya nchi hi


Labda wataihamishia kwingine
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom