Amani Msumari
JF-Expert Member
- Aug 21, 2016
- 1,830
- 976
Wanajamvi. Amani kwenu
Leo ni siku nyingine ya kutafakari utendaji mzuri wa Rais Magufuli na serikali yake katika kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 - 2020. Leo tuangalie Sekta ya Kilimo.
Katika jitihada za kuendeleza kilimo, kuliundwa dirisha la kilimo katika Benki ya Uwekezaji (TIB). Akiwa katika miaka yake ya mwisho, mzee Kikwete aliunda benki ya Kilimo. Katika kipindi hiki cha miaka mitano, Rais Magufuli ameendelea kuiimarisha benki ya Kilimo.
Sekta ya Kilimo ni sekta iliyoajiri watanzania wengi zaidi. Ni sekta kubwa. Ninaomba Leo niongelee benki ya Kilimo. Kwa kutambua kuwa wakulima wengi hawakidhi vigezo vya kukopesheka katika mabenki ya biashara, kwa makusudi serikali imeweka utaratibu maalimu wa kuwakopesha wakulima, utaratibu ulio tofauti kabisa na mabenki ya biashara.
Wakulima wadogowadogo wenye mashamba yenye ukubwa wa heka 1 - 50 wanaunda kikundi cha watu 5 - 30. Serikali inawakopesha fedha kw ajili ya kuendeleza kilimo. Fedha inatoka kwa awamu na timu ya Kilimo ya wilaya chini ya afisa kilimo anafanya ufuatiliaji.
Nitatoa mfano wa wakulima wa mihogo wilayani Handeni mkoani Tanga. Hapa vikundi vingi vimepata mikopo na kazi inaendelea. Wakulima wanapata shilingi 1,500,000 kwa heka moja. Fedha hii inatoka kwa awamu kuanzia kuandaa shamba, pembejeo, upandaji, upaliliaji, uvunaji na usafirishaji. Rejesho linafanywa baada ya mavuno kuuzwa. Hii sio hadithi, ni mambo halisi yanayotokea. Mpaka Sasa shilingi bilioni 3.6 zimeshakopeshwa kwa wakulima wilayani Handeni. Hali iko hivi maeneo mengine ya Tanzania.
Nawashauri watanzania wenzangu kufika ofisi za kilimo zilizopo karibu nanyi mpate maelezo ya kina nanyi mfaidike.
Nimelazimika kuandika haya kwasababu mnaulaumu tuu, mnasema hakuna kilichofanyika kwenye kilimo. Tatizo hamfuatilii mambo mnaulaumu tuu huku mkiwa hamna taarifa sahihi.
Mambo yameanza kunoga, mambo yameanza kukaa sawa Ila ni lazima tuwe na subira, Roma haikujengwa ndani ya siku moja. Tinaposema JPM 5 tena, ni mambo kama haya yanayotupa nguvu.
Hongera JPM
Hongera serikali
Hongera CCM
JPM mitano tena #achakaziiendelee